Rasmi kwa ridhaa yangu mwenyewe nimeamua kuacha pombe Eeeh Mwenyezi Mungu nisaidie

Hiki ni kichwa cha panzi aiseeee,yaani eti pombe isababishe nisiendeleee kulipandisha ghorofa langu la loshen 8 wakati mchongo wa hela ya
Kulijenga niliupata ulevini na sio kanisani au msikitini?
 
Lidhaa = Ridhaa
Pombe huwezi kuiacha kirahisi hivyo Kijana
 
Majuto ya pombe huja baada ya tukio la kuumiza lakini utarudi tu. Ushauri mwepesi, achana na pombe za makundi, jifunze kunywa kwa kiasi na fanyia hilo mazoezi kwa kujiwekea kipimo na kukiheshimu.

Kama ukinywa huwezi kujizuia kufanya maovu kama uzinzi au kunywa kupitiliza bora uache kabisa!

Usiache pombe kwa majuto ya muda, jipange ujue kinachokufelisha! Pombe ni sawa na bunduki, mtu akishaua sio bunduki ndio iliyoua!

Yupo jamaa yangu kabla hajaanza kunywa husali kuomba anywe kwa kiasi tena hana aibu, mbele ya kadamnasi anapiga ishara ya msalaba na kuomba! Anasema imemsaidia maana kadri anavyokunywa dhamiri inamsuta na alishaapa kuwa pombe haitamtawala.

Usipojua mzizi wa tatizo utaacha kwa muda tu. Yupo rafiki yangu mwingine amekaa 5 years bila kuonja pombe lakini mkewe kujifungua akajipongeza kwa wine ndio akafungulia balaa hadi leo. Huyu aliacha bila kuchunguza mzizi wa tatizo.

Wengine ni tatizo la kifamilia unakuta pombe ni tatizo linawatesa ( roho ya ulevi). Unaweza kujiapiza kuacha pombe kumbe ni spirit unahitaji deliverance otherwise utarudi tu.
 
Mimi bia zilikuwa zinanimalizia sana hela. Sasa hivi toka tarehe 13 juni sijagusa, nakunywa konyagi ya 8000 na soda ya 600 na simalizi.
Nikifika kwa mangi naagiza nyagi napiga, ikishapanda kichwani inayobaki naondoka nayo naitumia kama breakfast asubuhi.
 
Una hangover kali tu wewe... Njoo after 3 months utupe mrejesho.
 
Heri yako wewe umeona, wengine akili na mwili havishirikiani (akili ni tofauti na mwili).
 
👍
 
Mkuu kua serious, kuacha pombe sio rahisi kama bao la kwanza
 
Hapa kwenye familia kuna ka ukweli fulani kwetu pombe ni kama maji ya kunywa
 
- Pombe imenifanya kutokuwa mwaminifu kazini, nimekuwa mwizi nguli ili mradi tu nipate hela ya kulewa.
Hili wala usiisingizie pombe kawaida yetu wabongo ni watu wa kupiga kinachofata sasa piga ufanye maendeleo ya maana.
 
achana na pombe za makundi, jifunze kunywa kwa kiasi na fanyia hilo mazoezi kwa kujiwekea kipimo na kukiheshimu.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
inayobaki naondoka nayo naitumia kama breakfast asubuhi

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…