PreGE2025 Rasmi, Mahakama yapiga marufuku shughuli zote za CHADEMA

PreGE2025 Rasmi, Mahakama yapiga marufuku shughuli zote za CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Kutoka Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepigwa marufuku kufanya shughuli zozote zile za kiutendaji na oparesheni mpaka hapo kesi ya msingi iliyofunguliwa na aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Zanzibar Saidi Issa Mohamed na wenzake wawili (2) dhidi ya Baraza la Wadhamini na Katibu Mkuu wa CHADEMA itakaposikilizwa

Jaji Hamidu Mwanga anayesikiliza kesi hiyo namba 8323/2025 amesema zuio hilo la muda linakuja kufuatia maombi yaliyowasilishwa Mahakamani hapo na Mawakili wa waleta maombi wakiongozwa na Wakili Gido Thomas Simfukwe ambao waliiomba Mahakama kuweka zuio hilo hadi kesi ya msingi inayoanza kusikilizwa Juni 24.2025 isikilizwe, ambapo kwenye kesi ya msingi waleta maombi wanadai kuwa CHADEMA imekuwa ikiitenga Zanzibar katika masuala mbalimbali ikiwemo mgawanyo wa raslimali fedha nk

Akitangaza uamuzi huo, Jaji Mwanga amesema suala hilo ni la kisheria na haliitaji ubishani kwa sababu limefafanuliwa vyema kwenye sheria ya vyama vya siasa,

Wakati maamuzi hayo yanatolewa, upande wa utetezi (CHADEMA) haukuwa na mwakilishi yeyote Mahakamani, hiyo ni baada ya aliyekuwa Wakili wake Jebra Kambole kutangaza kujiondoa kwenye shauri hilo hatua iliyopelekea Mahakama kuendesha kesi kwa upande mmoja,

Kwa muktadha huo, ni wazi sasa shughuli za kisiasa za ndani (kiutendaji) na za oparesheni kama vile mikutano ya hadhara, vikao vya CHADEMA, vimezuiliwa kwa muda.
Huu ni ushindi mkubwa sana kwa Chadema huu ni ushindi mkubwa sana kwa No reform No Election huu ni ushindi mkubwa kwa wapigania Haki mana imejidhihirisha dhahiri shahiri kua CDM imekua tishio kwa wanaonufaika na rasilimali za watamganyika wanaogopa wananchi wanavyofumbuliwa macho tusihidhunike hata kidogo hii ndio njia ya ukombozi wankweli tunaelekea kuzuri.Tumshukuru alieshauri haya nakuruhusu yatokee Dunia imejua wananchi wanaona nani haitakii mema nchi yetu


No reform No Election
 
Mihimili ya DOLA (vyombo vyetu /,State apparatu), MAHAHAKAMA, BUNGE vimetekwa na kundi la wakoloni wachache wa chama dola kongwe CCM.

Sasa kwa kuwa hakuna tena utawala bora wala sehemu ya kutetea haki za jamii, ni njia moja iliyobaki kwa maridhiano, mazungumzo, haki kupitia mfumo wa haki jinai vyote imeshindikana

Ni wakati wa njia nyingine nje ya mifumo hiyo ikiyotekwa na watawala itabidi kutumika.

Nguvu ya umma tu ndiyo itaweza kuleta mabadiliko yaani reforms .
 
Back
Top Bottom