PreGE2025 Rasmi, Mahakama yapiga marufuku shughuli zote za CHADEMA

PreGE2025 Rasmi, Mahakama yapiga marufuku shughuli zote za CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Kutoka Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepigwa marufuku kufanya shughuli zozote zile za kiutendaji na oparesheni mpaka hapo kesi ya msingi iliyofunguliwa na aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Zanzibar Saidi Issa Mohamed na wenzake wawili (2) dhidi ya Baraza la Wadhamini na Katibu Mkuu wa CHADEMA itakaposikilizwa

Jaji Hamidu Mwanga anayesikiliza kesi hiyo namba 8323/2025 amesema zuio hilo la muda linakuja kufuatia maombi yaliyowasilishwa Mahakamani hapo na Mawakili wa waleta maombi wakiongozwa na Wakili Gido Thomas Simfukwe ambao waliiomba Mahakama kuweka zuio hilo hadi kesi ya msingi inayoanza kusikilizwa Juni 24.2025 isikilizwe, ambapo kwenye kesi ya msingi waleta maombi wanadai kuwa CHADEMA imekuwa ikiitenga Zanzibar katika masuala mbalimbali ikiwemo mgawanyo wa raslimali fedha nk

Akitangaza uamuzi huo, Jaji Mwanga amesema suala hilo ni la kisheria na haliitaji ubishani kwa sababu limefafanuliwa vyema kwenye sheria ya vyama vya siasa,

Wakati maamuzi hayo yanatolewa, upande wa utetezi (CHADEMA) haukuwa na mwakilishi yeyote Mahakamani, hiyo ni baada ya aliyekuwa Wakili wake Jebra Kambole kutangaza kujiondoa kwenye shauri hilo hatua iliyopelekea Mahakama kuendesha kesi kwa upande mmoja,

Kwa muktadha huo, ni wazi sasa shughuli za kisiasa za ndani (kiutendaji) na za oparesheni kama vile mikutano ya hadhara, vikao vya CHADEMA, vimezuiliwa kwa muda.




View attachment 3363251

Hii ndio picha ya Hakimu wa Mahakama Kuu Hamidu Mwanga aliyetoa uamuzi wa kuipiga CHADEMA marufuku

View attachment 3363259

Source: Jambo TV
Tanganyikakumamayo😬
No reforms no election 💯 ⚒️
October tutakuwepo 😎
 
Mahakama hizi zilizokaa na kesi ya kina Mdee zaidi ya miaka motatu bila kutoa hukumu? Mkuu unaamini bado watu ni wajinga?

Mkuu ukishajua mbinu za adui ni kujitahidi kuruka mitego yake ,target ya msajili na sirikali ni kuiua CDM sasa hizo ni baadhi ya mbinu zao za kukidhoofisha ,ili uruke viunzi vyao ni kujitahidi kwenda nao nginja ngija na si kushindana nao hasa kwenye issue za kisheria/taratibu/kanuni maana wao wameshika MPINI.
 
Back
Top Bottom