PreGE2025 Rasmi, Mahakama yapiga marufuku shughuli zote za CHADEMA

PreGE2025 Rasmi, Mahakama yapiga marufuku shughuli zote za CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Mahakama imeonyesha ni kea nmna gani inatumiwa na Serekali na CCM kuihujumu CHADEMA. Hilinni pigo kubwa kwa wapenda mabadiliko. Hii kesi haitaisha mpaka uchaguzi mkuu upite.
Ccm/serekali 5-0 Chadema.

NoReformNoElection
 
wananchi watazidi kuchukia watawala, maana wanaziona hizi Hila waziwazi.

hizi figisu hazilisaidii taifa kwa chochote zaidi kuichafua mioyo ya watu zaidi na zaidi.

nchi haina Bunge, Mahakama haziko huru!
 
CCM inajisifu Ina wanachama 13mil, Sasa uoga wote huu wa nini?
Kuwa chama tawala sio kuwa lazima uachie vyama vingine viendeshwe kiholela kuteka haki za Wazanzibari

Kwa hiyo mlitaka kwa kuwa CCM chama tawala kina mamilioni ya wanachama nyie wachache wa bara mpore haki za Wazanzibari?
 
Kuwa chama tawala sio kuwa lazima uachie vyama vingine viendeshwe kiholela kuteka haki za Wazanzibari

Kwa hiyo mlitaka kwa kuwa CCM chama tawala kina mamilioni ya wanachama nyie wachache wa bara mpore haki za Wazanzibari?
Wako wangapi kwanza? Haki gani acheni ukuda nyie maviciciem
 
Mnapoteza muda kutumia njia za kidemokrasia kuiondoa ccm madarakani. Njia ipo moja tu na nadhani kila mtu anaijua.

Ni Kweli kabisa kwa zaidi ya 100%.

Mimi mara nyingi sana humu kwenye mtandao huu nimekuwa nikieleza wazi wazi kabisa kwamba Chadema ni Chama sahihi, lakini mbinu wanazotumia katika kupambana na CCM siyo sahihi hata kidogo.They are completely wrong in selecting the proper way of dealing with CCM.
 
Kutoka Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepigwa marufuku kufanya shughuli zozote zile za kiutendaji na oparesheni mpaka hapo kesi ya msingi iliyofunguliwa na aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Zanzibar Saidi Issa Mohamed na wenzake wawili (2) dhidi ya Baraza la Wadhamini na Katibu Mkuu wa CHADEMA itakaposikilizwa

Jaji Hamidu Mwanga anayesikiliza kesi hiyo namba 8323/2025 amesema zuio hilo la muda linakuja kufuatia maombi yaliyowasilishwa Mahakamani hapo na Mawakili wa waleta maombi wakiongozwa na Wakili Gido Thomas Simfukwe ambao waliiomba Mahakama kuweka zuio hilo hadi kesi ya msingi inayoanza kusikilizwa Juni 24.2025 isikilizwe, ambapo kwenye kesi ya msingi waleta maombi wanadai kuwa CHADEMA imekuwa ikiitenga Zanzibar katika masuala mbalimbali ikiwemo mgawanyo wa raslimali fedha nk

Akitangaza uamuzi huo, Jaji Mwanga amesema suala hilo ni la kisheria na haliitaji ubishani kwa sababu limefafanuliwa vyema kwenye sheria ya vyama vya siasa,

Wakati maamuzi hayo yanatolewa, upande wa utetezi (CHADEMA) haukuwa na mwakilishi yeyote Mahakamani, hiyo ni baada ya aliyekuwa Wakili wake Jebra Kambole kutangaza kujiondoa kwenye shauri hilo hatua iliyopelekea Mahakama kuendesha kesi kwa upande mmoja,

Kwa muktadha huo, ni wazi sasa shughuli za kisiasa za ndani (kiutendaji) na za oparesheni kama vile mikutano ya hadhara, vikao vya CHADEMA, vimezuiliwa kwa muda.




View attachment 3363251

Hii ndio picha ya Hakimu wa Mahakama Kuu Hamidu Mwanga aliyetoa uamuzi wa kuipiga CHADEMA marufuku

View attachment 3363259

Source: Jambo TV
Mambo gani hayo tena jamani kwani zile mbinu 1001 zimefeli
 
Rule of Law ,kama member wa chama amefungua kesi ni lazima CDM ifuate taratibu za kesi na zinavyotaka ,kama wameambiwa walete docs ni lazima kuleta ili mahakama iamue ukileta uharakati kwenye mahakamana lazima utapigwa RUNGU.
HIzo ni hujuma za makusudi za ccm dhidi ya CDM kupitia dola. Vuguvugu la kisiasa linawapa hofu na wananchi wameelimika na wanazidi kuelimika na kuona wanavyofanywa wajinga.
 
Back
Top Bottom