PreGE2025 Rasmi, Mahakama yapiga marufuku shughuli zote za CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Kutoka Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepigwa marufuku kufanya shughuli zozote zile za kiutendaji na oparesheni mpaka hapo kesi ya msingi iliyofunguliwa na aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Zanzibar Saidi Issa Mohamed na wenzake wawili (2) dhidi ya Baraza la Wadhamini na Katibu Mkuu wa CHADEMA itakaposikilizwa

Jaji Hamidu Mwanga anayesikiliza kesi hiyo namba 8323/2025 amesema zuio hilo la muda linakuja kufuatia maombi yaliyowasilishwa Mahakamani hapo na Mawakili wa waleta maombi wakiongozwa na Wakili Gido Thomas Simfukwe ambao waliiomba Mahakama kuweka zuio hilo hadi kesi ya msingi inayoanza kusikilizwa Juni 24.2025 isikilizwe, ambapo kwenye kesi ya msingi waleta maombi wanadai kuwa CHADEMA imekuwa ikiitenga Zanzibar katika masuala mbalimbali ikiwemo mgawanyo wa raslimali fedha nk

Akitangaza uamuzi huo, Jaji Mwanga amesema suala hilo ni la kisheria na haliitaji ubishani kwa sababu limefafanuliwa vyema kwenye sheria ya vyama vya siasa,

Wakati maamuzi hayo yanatolewa, upande wa utetezi (CHADEMA) haukuwa na mwakilishi yeyote Mahakamani, hiyo ni baada ya aliyekuwa Wakili wake Jebra Kambole kutangaza kujiondoa kwenye shauri hilo hatua iliyopelekea Mahakama kuendesha kesi kwa upande mmoja,

Kwa muktadha huo, ni wazi sasa shughuli za kisiasa za ndani (kiutendaji) na za oparesheni kama vile mikutano ya hadhara, vikao vya CHADEMA, vimezuiliwa kwa muda.

View attachment 3363251

Hii ndio picha ya Hakimu wa Mahakama Kuu Hamidu Mwanga aliyetoa uamuzi wa kuipiga CHADEMA marufuku

View attachment 3363259

Source: Jambo TV
No reforms, No elections. CCM imeshikwa pabaya sana
 
Sema mtu yoyote anayefurahia Aya Mambo nakua na Mashaka na Utimamu wake Kweli unaweza furahia aya Mambo unapigana na Mtu aliyefungwa kamba alafu unajiona Una nguvu huko ni Kujidanganya hunaweza kufunga watu Magereza lakini huwezi kufunga Mawazo ya watu ni ngumu huwezi kuzuia Nyakati mara nyingi Nyakati Usema
 
Shekh sio kweli kwamba waislam wanatumika kinachotokea ni watu wachache mno kwa tamaa zao za kidunia wameamua kutumika na hawa watu wapo kwenye imani zote hata wakristo na madhehemu mengine unamzungumziaje Malasusa wa kkkt ni muislamu yule?kwenye hili km taifa tuungane kukemea kwa pamoja tusiganyike kumpa adui nguvu hakuna Mtanzania yoyote mwenye akili. timamu anayefurahia haya yanayoendelea hao wachache wanatumika kwa maslai yao wala sio kwa maslai ya uislam
 
Kutoka Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepigwa marufuku kufanya shughuli zozote zile za kiutendaji na oparesheni mpaka hapo kesi ya msingi iliyofunguliwa na aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Zanzibar Saidi Issa Mohamed na wenzake wawili (2) dhidi ya Baraza la Wadhamini na Katibu Mkuu wa CHADEMA itakaposikilizwa

Jaji Hamidu Mwanga anayesikiliza kesi hiyo namba 8323/2025 amesema zuio hilo la muda linakuja kufuatia maombi yaliyowasilishwa Mahakamani hapo na Mawakili wa waleta maombi wakiongozwa na Wakili Gido Thomas Simfukwe ambao waliiomba Mahakama kuweka zuio hilo hadi kesi ya msingi inayoanza kusikilizwa Juni 24.2025 isikilizwe, ambapo kwenye kesi ya msingi waleta maombi wanadai kuwa CHADEMA imekuwa ikiitenga Zanzibar katika masuala mbalimbali ikiwemo mgawanyo wa raslimali fedha nk

Akitangaza uamuzi huo, Jaji Mwanga amesema suala hilo ni la kisheria na haliitaji ubishani kwa sababu limefafanuliwa vyema kwenye sheria ya vyama vya siasa,

Wakati maamuzi hayo yanatolewa, upande wa utetezi (CHADEMA) haukuwa na mwakilishi yeyote Mahakamani, hiyo ni baada ya aliyekuwa Wakili wake Jebra Kambole kutangaza kujiondoa kwenye shauri hilo hatua iliyopelekea Mahakama kuendesha kesi kwa upande mmoja,

Kwa muktadha huo, ni wazi sasa shughuli za kisiasa za ndani (kiutendaji) na za oparesheni kama vile mikutano ya hadhara, vikao vya CHADEMA, vimezuiliwa kwa muda.

View attachment 3363251

Hii ndio picha ya Hakimu wa Mahakama Kuu Hamidu Mwanga aliyetoa uamuzi wa kuipiga CHADEMA marufuku

View attachment 3363259

Source: Jambo TV
Kwenye hili hata kipofu ataliona😷😷.
 
Kutokana na hali ya Udikteta uliopo kwenye nchi hii, Uamuzi huu wala siyo kitu cha ajabu hata kidogo, ilitegemewa kwamba lazima Uamuzi wa namna hii ungechukuliwa. Siyo Kitu Cha ajabu na wala haishangazi.

Hata Chama Tawala nchini Afrika Kusini Cha ANC nacho kiliwahi kutangazwa kuwa eti ni Kundi la Kigaidi na Utawala dhalimu wa Makaburu. Lakini kutokana mbinu kali Sana walizokuwa wakizitumia Watu wa ANC katika kupambana na Utawala wa Makaburu, hatimaye ANC iliibuka kidedea na kupata ushindi mnono ambao umewaingiza madarakani nchini humo hadi leo hii.

Jambo la muhimu zaidi kwa CHADEMA Sasa hivi wanapaswa watumie mbinu zilizo sahihi katika kupambana na CCM, wafuate nyayo za Watu wa ANC.
 
Kuna sehemu nilisikia kama tetesi Mwaka Jana, kulikuwa na mpango wa kuifutia Usajili CDM

Miezi 14 sasa naona wale jamaa walikuwa wanamaanisha walichokisema.

Tuendelee kuiombea Nchi yetu 🙏🙏
 
Back
Top Bottom