Rasmi nawaondoa simba kwenye mbio za ubingwa 2021-2022

simba haiwezi kua kama africa lion ila tabia ya kuingilia uhuru wa watu wa jeuri ya pesa hauna afya kwa team yetu, bila upuuzi ule tungeendelea kumshuhudia chama msimu huu.
Mkuu wewe ni mwanasoka kweli,povu linakutoka ivo kwa mechi moja tu.

Tutarudi hapa tena nkuoneshe hii,

Nakuapia simba inaenda kua hatari kuliko ilivyokua msimu huu,

Chama mwenyew mara zote hizi game za hawa utopolo wakamiaji hajawai kushine kabisa, na ulidondoaha point nying kwa azam pia.

Matokeo ya jana its just football.
 
Siyo kweli usemayo ,, bali Simba wataetea taji lao vizuri na kulibeba tena kwa mara ya tano mfululizo.
 
Walau wewe umeongea kimichezo kidogo. Japo Simba wapo sawa kumuuza Chama na Miqson, . Kiufupi ubora wa mtu hauji kwa kufanya yaleyale na watu walewale , ubora ni ku maintain ubora wako katika vipindi vyote kwa mbinu tofauti hata wakati ambao unaemtegemea akiwa hayupo.

Pia Simba kufungwa na yanga si kigezo cha ubora au udhaifu wake na halikadharika yanga kufungwa na Simba. Ufupi ni kwamba Simba kufungwa na yanga ni njema sana kwa Maslahi ya mechi zijazo mana kila mchezaji atajiona hajui na atakuwa mwenye kuanza upya na kutaka ku provewrong kwa mashabiki ubora wake kila mechi.

Tofauti na ushindi ambao ungetengeneza himaya ya baadhi ya wachezaji kwa mapambo na sifa nyingi kwenye magazeti na kujikuta wamemaliza kama ilivyokuwa kwa Morrison
 
Uelewa wako kwenye mpira ni mdogo kama wangu au mapenzi yako yamebebwa kwa ushabiki wenye kutaka ushindi kila siku bila kukubari mchakato. Zingatia yafuatayo

1: Ukiangalia takwimu za jana baada ya Mechi Yanga alichomshinda Simba ni Magori na kona tu (wataalamu mtanisahihisha) ila kunzia ball position, on target, pasi , clean shit, na utulivu Simba kaongoza. Sasa unatumia kigezo gani ku criticise uwezo wa wachezaji wa Simba?.

2: Yanga ilivyocheza jana ndio ilivyocheza July 3 na ndio ilivyocheza November 7 mwaka jana ambapo Mwamba na konde walikuwepo. (Namaanisha mfumo wa kushambulia kwa kasi na kuzuwia kwa wingi.) Unachotakiwa kujua Yanga inayocheza na Simba ni tofauti na itakayocheza na Namungo au Biashara.

3: ukiangalia performance ya mchezaji mmoja mmoja Simba wanachokosa ni striker mwenye maamuzi, uwezo na bahati yakufunga magori ambalo ndo tatizo lao miaka yote toka Chama yupo (wanatengeneza nafasi nyingi wanatumia chache)jana katengeneza nafasi nyingi kuliko yanga na yanga kapata chache katumia.ukiskia Simba kafunga gori 3 jua kakosa 8. Kama unakumbuka ile mechi ya Kaizer Cheef kwa mkapa kama wangekuwa wanamtu ninaemzungumzia wangeshinda saba.

4: Bado mapema sana sana sana ku judge uwezo wa wacheza wakati hata ligi haijaanza(shida mpira wetu unaongozwa na propaganda sana) . Mwaka jana Yanga kacheza mechi 10 hajafungwa muda ambao Simba akiwa kafungwa mara mbili ila nani katwaa ubingwa?. Hebu tuache mihemko tujifunze kuwa wavumilivu yani mechi moja tu tushaoona timu moja ndo inajuuuuuuuwa na nyingne haiijuuuuuwi?. Bado mapema sana.
 
Sisi hatujaumia kufungwa na yanga tu,ila tunaumia kuwa hatutafanya vzr kimataifa kwani wachezaji hawana kabisa fighting spirit.

Ni kama wako academy tu wakijiandaa kufuzu mafunzo.Wanacheza wame relax kama vile wao ni mastaa sana.

Nasubiri dhihaka nyingine baada ya kutolewa CAF championship.

 
Uelewa wako kwenye mpira ni mdogo kama wangu au mapenzi yako yamebebwa kwa ushabiki wenye kutaka ushindi kila siku bila kukubari mchakato. Zingatia yafuatayo...
Jana simba walionyesha mpira mbovu
 
Kwani nkuulize swali.. chama ndio alikuwa mfungaji bora au hawakuwepo simba ilipofungwa na yanga mechi zilizotangulia.? Pili hata kina chama na Luis mwanzo mliwabeza mkaja kuwaelewa baadae tulia utajua hujui kunywa mtori nyama utazikuta
mkuu ukichukua jumla ya magoal na assist za chama kwa misimu 3 alokua simba hakuna mchezaji anaemfikia wala kumkaribia kwenye ligi yetu.
 
mkuu ukichukua jumla ya magoal na assist za chama kwa misimu 3 alokua simba hakuna mchezaji anaemfikia wala kumkaribia kwenye ligi yetu.
Walio mleta chama ndio hao hao.wamemuuza na kutuletea wengine hivyo hata yeye mwanzo.alisua sua tujipe muda chukulia city alianza vibaya ila now anauwasha balaa
 
ukichukua magoal aloyatengeneza chama(assist+magoal) ndani ya misimu 3 hakuna mchezaji anaemfikia wala kumkaribia, inshort chama alikua na dunia yake kwenye ligi yetu.
[emoji419][emoji419]
 
Dah hoja ya mwisho ni fikirishi sana, unakataa mkataba mnono wa mabilioni kutoka Azam unaenda kusaini mkataba wa mamilioni milioni
 
Watu hawalalamikii matokeo bali performance ya timu. Kwanza kwenye mapinduzi hawakuwepo chama na Miquissone. Kinacholalamikiwa ni namna timu jana inavyopigiwa mpira biriani huku washabiki wa Simba wakishikilia moyo kwa woga. Lakini mechi za nyuma wakiwepo wakina chama, Yanga hata Kama wameshinda wanaomba mpira uishe. Mashabiki wa Yanga amani hawana mpaka kipenga cha mwisho ndio wanashukuru
 
Shida ya simba sio chama wala luis ata kama watakosa ubingwa wale wachezaji waliosajili simba mfano sacko na yule kanoute ukiwaangalia ni wachezaji wazur ila tatzo la simba walifanya zalau na mazoea lazma mwaka huu wajute asa ktk mechi kubwa ,timu ikikaa miaka minne adi mitano pamoja ikafanya vzur si rahisa sana kuendelea kufanya vzur usipoziba matatzo ata kipind chama na luis wapo bado simba walikua na matatzo kama unafuatilia mechi za simba zile ngum kuna mechi wanapoteza morali inatokea mara nying kwa sababu ya kuchoka pia na kujiamin sana simba mwaka uliopta matatzo yao yalikua karbu kila idara nyuma wana matatzo yao bek za pemben zimechoka sana wamecheza sana mwaka huu sikutegemea kama wataendelea kufanya vzur zaid ktk eneo la kiungo mkabaji ule ukabaj wa lwanga kwa timu za kawaida sana ila timu inayokua na viungo wazur lwanga sio mzur kwa kukaba maana umbo lake umr wake unamfanya asiwe na kasi ya kusoma atar mara nyng anacheza faulo akikutana na viungo shap nilijiulza sana simba wanajiamin nn kutosajili mchezaj aina ya aucho ikiwa wana tatzo eneo ilo ,eneo la umaliziaji nalo ndio usiseme unaweza kumlaum mugalu anakosa magol ila shida ata hao wengine ndio wale wale hakukua na sababu ya kuendelea na mugalu na kagere msimu mmoja wapo angempisha mtu mwngine mzur zaid ambae nafas tatu moja ataitumia ,mwaka huu simba wamesajili wachezaji lkn hawakuangalia kuziba matatzo ya mwanzo kwanza wamesajil tu wachezaj kwa kusema uyu mzur anafaa ,ukija kuongeza na mapengo ya chama na luis ndio balaa zaid mwaka huu liwe funzo tukubal mechi kubwa nying tutaumia
 
...Polani mkuu, wenzio watakuita Uto.
 
Simba ya msimu huu ni kupigwa tu,sikupenda wale wachezaji kuondoka.They were the game changers
Hata kama wangebaki na timu ingepoteza bado maneno kwa wapiga domo yasingekosekana.

Nyie ndo hadi timu ishinde muanze kutamba kuwa mnakikosi bora.

Hivi unakumbuka yanga walikuwa wanasema nini wiki 2 nyuma?

Waulize leo wanavyoiona timu yao,kama vile ndo imeshaweka rekodi ya ubingwa.

Tuupe muda muda huku tukiona nini timu inafanya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…