Rasmi, Nigeria yatangaza kuuza mafuta yake kwa kutumia sarafu yake ya Naira badala ya Dola Marekani

Rasmi, Nigeria yatangaza kuuza mafuta yake kwa kutumia sarafu yake ya Naira badala ya Dola Marekani

China yenyewe kashindwa kutoka kwenye mfumo wa dollar, na ndo anaongoza kufanya export duniani kote!!
Fatilia takwimu, hadi Sasa china kapunguza reserve kubwa ya dollar. Futatilia Saudia ndo utaona jinsi wanavyopunguza utegemezi wa dollar taratibu. Hawawezi kutokana haraka, ni process inachukua taratibu. Matumizi ya $ yanazidi kuporomoka kila siku, labda nikupe hii mpya, kwasasa unaweza lipia gari Japan kwa kutumia Yen huna haja ya dollar.
 
Utazinunua Naira kwa dola benki kuu ya Nigeria ndipo ununue mafuta yao

Watapata faida mara mbili kukuzia Naira na kukuuzia mafuta

Hiyo itapandisha thamani ya Naira ya Nigeria

Wako sahihi sana kwa hiyo hatua
Umemjibu vizuri.
Ila Mtanzania ni fundi wa kubisha aisee.anabishia Hadi maandishi ualiyotoka Nigerian
 
Hixo hatua wauziane wenyewe humo ndani na Naira zao, international trade zina masharti mengine.

Watamuuzia urusi na China hayo mafuta?

Wape muda utasikia.

Masikini huwa tukishiba tuna lala tunasahau njaa huwa ina rudi tena kwa kasi sana.
Russia amesha move on tayari, haangaiki na $.
 
Ipo siku tutafanya TU naamini katika makubwa yaliyo mazuri
Tatizo mfumo huu wa kibepari unafany wote tuigombanie dollar, bandarini gharama unalipa kwa dollar,nyumba za vigogo zinapangishwa kwa dollar
Hadi baadhi ya viongozi wako wana account nje ya nchi za dollar, apart from story za kisiasa ni ngumu kwa nchi tegemezi kujiamulia au kutoka kwenye mfumo wa mabeberu
Magufuli alithubutu lakini ndio hivyo yakatokea yaliyotokea, kupambana na mfumo ni ngumu sana, hii mifumo wameijenga ili usitoke ,na ukijaribu kutoka utatolewa wewe na wananchi wako watatiwa upepo watashangilia tu kama gaddafi alivyotolewa
 
Russia amesha move on tayari, haangaiki na $.
Ka move on su kabanwa?

Akilegezewa vikwazo anarufi mbio.

Mfungwa kukwambia tuliisha zoea na kufurahia maisha gerezani haimaanishi hapendi uhuru.
Inamaanisha ka adopt hali anayolazimishwa kuiishi.
 
Sifa zote hizo lakini bado uchumi wao hauridhishi...
 
Unafikiri ni sababu zipi ambazo zinapelekea tuna high demand ya $?
Marekani kama super power wa dunia ameweka mifumo yote ya kukopesha ,kutoa huduma etc kwa dollar
TAnzania na third world countries tuna import almost everything, jusi nimeshangaa kumbe hadi nondo za kujenga sky scrappers tuna import achana na bidhaa nyingine za ujenzi, kwa hiyo yule ghorofa obviously atapiga mahesbu yake kwa usd ili apate faida baada ya kuinvest
Serikali inakopa kwa dollar na ili ilipe itabidi iwe na reserve kubwa bot ya dollar kuweza kulipa madeni yake na kuwezesha kuimport bidhaa kwa wananchi wake maana dollar ndio major currency inayotumika kwenye soko la kimataifa, leo hata ukitaka kitu china mchina atakupa quotation ya dollar
Kwahiyo demand ni kubwa mno mno
 
Ka move on su kabanwa?

Akilegezewa vikwazo anarufi mbio.

Mfungwa kukwambia tuliisha zoea na kugurahia maisha gerezani haimaanishi hapendi uhuru.
Inamaanisha ka adopt hali anayolazimishwa kuiishi.
Ni kweli ni hana option siyo kwamba anapenda ingawa russia ni taifa kubwa yupo kwenye level za marekani huko, amejitosheleza na yeye ana resources nyingi ambazo zinategemewa na europe yote ikiwemo gas, mafuta, coal, ngano etc kwahiyo kidogo anaweza kumudu ,ila kwa nchi ambayo ina madeni na ina import 90% ya bidhaa ni impossible kuikwepa dollar
 
Tatizo mfumo huu wa kibepari unafany wote tuigombanie dollar, bandarini gharama unalipa kwa dollar,nyumba za vigogo zinapangishwa kwa dollar
Hadi baadhi ya viongozi wako wana account nje ya nchi za dollar, apart from story za kisiasa ni ngumu kwa nchi tegemezi kujiamulia au kutoka kwenye mfumo wa mabeberu
Magufuli alithubutu lakini ndio hivyo yakatokea yaliyotokea, kupambana na mfumo ni ngumu sana, hii mifumo wameijenga ili usitoke ,na ukijaribu kutoka utatolewa wewe na wananchi wako watatiwa upepo watashangilia tu kama gaddafi alivyotolewa
Hawa wenzetu walio weza kutoka wametumia njia gani
 
Marekani kama super power wa dunia ameweka mifumo yote ya kukopesha ,kutoa huduma etc kwa dollar
TAnzania na third world countries tuna import almost everything, jusi nimeshangaa kumbe hadi nondo za kujenga sky scrappers tuna import achana na bidhaa nyingine za ujenzi, kwa hiyo yule ghorofa obviously atapiga mahesbu yake kwa usd ili apate faida baada ya kuinvest
Serikali inakopa kwa dollar na ili ilipe itabidi iwe na reserve kubwa bot ya dollar kuweza kulipa madeni yake na kuwezesha kuimport bidhaa kwa wananchi wake maana dollar ndio major currency inayotumika kwenye soko la kimataifa, leo hata ukitaka kitu china mchina atakupa quotation ya dollar
Kwahiyo demand ni kubwa mno mno
Kwa Sasa hv mchina anataka yuan
 
Hawa wenzetu walio weza kutoka wametumia njia gani
Kama nchi gani iliyofanikiwa kutoka successfully ukiacha russia ambaye yupo kwenye vikwazo na ana export bidhaa zake ulaya yote, na amejitosheleza uzalishaji bidhaa
 
Kwa Sasa hv mchina anataka yuan
Juzi nimeagiza mzigo china nimepewa quotation kwa dollar, ingawa mchina anabalance lazima uwe na reserve ya dollar kwa sababu ndio inayotumika kwenye soko la kimataifa, hata hapa bongo kuna watu wanatembea na dollar kama wachina
Ingawa kwao demand siyo high kama sisi maana wanazalisha sana ,wana export sana , china ana import vitu vichache sana , ingawa still anahitaji dollar ili anunue vitu kama dhahabu ,mafuta etckwenye soko la kimataifa
 
Hahaha ya Sisi hizo Naira tutazitoa wapi?
Waongo tu hao wanajazana upepo, hata Nigerians hawayaki Hizo Naira, wana zibadili kwa dollor na kutunza dollar.
Wanajidanganya kwa muda mfupi na kujipa matumaini tu.
Inawezekana, wata print noti zao nyingi, ili uzipate utabadilisha kwa fedha za kigeni; kwa namna moja ama nyingine watakuwa wameimarisha sarafu yao na itakuwa na uhitaji mkubwa.
 
Kama nchi gani iliyofanikiwa kutoka successfully ukiacha russia ambaye yupo kwenye vikwazo na ana export bidhaa zake ulaya yote, na amejitosheleza uzalishaji bidhak

Kama nchi gani iliyofanikiwa kutoka successfully ukiacha russia ambaye yupo kwenye vikwazo na ana export bidhaa zake ulaya yote, na amejitosheleza uzalishaji bidhaa
Sasa kama Russia kaweza kwanini sisi tusiweze ni swala la muda TU madhari lonauwezekano wa kufanyika litafanyika TU hata kama litachukua muda kiasi gani. Pili ni china nae kafanya hvy
 
Watanzania bana sijui tukoje! Nigeria ndio wameamua kutumia mfumo huo kwa malengp ya kuimarisha sarafu yao,watanzania tunapinga tunasema haiwezekani! Hawa watu wamekaa chini wametathimini wakaona inawezekana ndio maana wakatoa tangazo. Sisi tunaongea maneno matupu kuwa haiwezekani.

Uzuri wameongelea ununuzi wa mafuta ghafi tu sio kila bidhaa itafanyika kwa naira. Na hawajasema kuwa wanaitupilia mbali dola bali wanafanya biashara ya ya mafuta kwa naira.

Ikitokea wamejaribu na wasifanikiwe, bado wataonekana ni majasiri sababu wamedhubutu tofauti na sisi ambao hata kujitambua tu ni shida. Tuwape moyo wanapojaribu kujitoa kwenye makucha ya hao wanyonyaji sio kuwakatiksha tamaa.
 
Back
Top Bottom