Rasmi nimeacha kuangalia mechi za Chelsea FC

Rasmi nimeacha kuangalia mechi za Chelsea FC

Attachments

  • 5A9C84F4-9FCF-4DEC-9B78-2E95081633AC.jpeg
    5A9C84F4-9FCF-4DEC-9B78-2E95081633AC.jpeg
    81.8 KB · Views: 1
Kila timu iliwahi pitia msoto flani hivi.

Kuna msimu Gunners tulipitia, aisee.
 
Acha uoga Jombaa, mimi Manchester United yangu mbovu sana ila siwezi kuacha kuiangalia timu ninayoipenda sana. Matokeo mabovu yanakera ila mpira ndio burudani yangu.
Burudan gan unapata as united fan ?m
 
huyu sio shabiki wa blues mtu kama hafamu ajern roben kacheza chelsea anawezaje kupata uchungu wa timu kaanza kuitazama chelsea ya kina james
Naikumbuka Chelsea ya akina Darmian Duff, Gudjohsen n.k, pasi tatu tu kutokea kwa kipa wako golini kwako...Arjen Robben bado kabisaa hapo, Mourhinho msaidizi wa Van Gal pale Barca enzi hizo nadhani...akaja Porto, akajipatia umaarufu kumpiga United mpaka kubeba NDOO; Lois Saha akisaidia kwa mbaali mechi ile.

Nilisimama kushabikia mpira misimu miwili mbele baada ya Sir kustaafu kimaajabu ajabu!
 
Chealsea kuna kama kalaana
Maana wachezaji wazuri wapo
 
Naikumbuka Chelsea ya akina Darmian Duff, Gudjohsen n.k, pasi tatu tu kutokea kwa kipa wako golini kwako...Arjen Robben bado kabisaa hapo, Mourhinho msaidizi wa Van Gal pale Barca enzi hizo nadhani...akaja Porto, akajipatia umaarufu kumpiga United mpaka kubeba NDOO; Lois Saha akisaidia kwa mbaali mechi ile.

Nilisimama kushabikia mpira misimu miwili mbele baada ya Sir kustaafu kimaajabu ajabu!
Umeona kaka ona united Washambuliaji wake nao Dont you miss Demitri babatov?
 
Wana sports leo ilikuwa mfululizo wa kipigo kwetu wana blues, kiukweli huwa naumia sana sasa kwa kuwa sisi huu msimu hatuna timu kabisa

Yaani usajili wote ni majeruhi na flop nimeamua kujiweka pembeni kwanza maana nitakua sina amani kabisa

Mpaka siku nikijaliwa kuingia kabsa Stamford Bridge

Poleni sana pia na nyie “Nyumbu”
Hii Chelsea mashabiki tuivumilie tu, tatizo limekuwa kubwa kutokana na majeruhi ya wachezaji wengi. Timu inabadirika kila siku na huwezi kumlaumu kocha. Hiyo timu wachezaji ambao hawajakaa majeruhi ni wawili watatu Jackson ambaye hakuna kitu, Silva, Disasi, Mudryk, Sterling. Wachezaji wanacheza michezo miwili wanaumia sijui ni laana ya ABRAMOVICH. Ila tatizo linguine sugu hakuna mshambuliaji, hata mechi ya Wolves ingeisha mapema mnoo. Chelsea ndiyo timu inayoongoza Kwa kukosa magoli ya wazi kwenye ligi, kabla ya mchezo wa wolves nafasi 36, ukiongeza za mchezo huo zinafika 40. Kocha aletewe straika tuu wa maana kama Phiri.
 
Umeona kaka ona united Washambuliaji wake nao Dont you miss Demitri babatov?
Naam...moja ya washambuliaji wa kukumbukwa! Rud Van Nestrloy, Andy Cole na Dwight Yorke ndo washambuliaji wa kwanza kwanza mimi kuwafaidi kucheki...Treble, kabla nikiwafagilia Bafana bafana, sijui club enzi hizo.

Michezo inaoneshwa ITV, wakina Babayaro, Sunday Oliseh wa Super Eagle.

Ile WC ya 1998 ndo ilikuwa ya mwisho kwa soka la vipaji, kila timu tamu! Argentina ya akina Emmanuel Batistuta, Ortega n.k
 
Naungana na wewe mkuu,kuanzia jana nimestaafu mpaka pale timu itaamua kuwa serious, siwezi kila siku ni kuumia tu
 
Ile ni dhuluma ya wazi kabisa dhidi ya wawekezaji kutoka nje. Maana aliyeivamia urusi ni Putin! Sasa kwa nini zitaifishe mali za Warusi?

Mimi siyo mtu wa kuunga mkono mambo ya kijinga.
Tajiri ana dual citizenship mkuu
Jews vs Russian
 
Tajiri ana dual citizenship mkuu
Jews vs Russian
Kwa hiyo Taifa lake mama kati ya Urusi na Israel ni lipi? Israel, au Urusi? Na hivyo vikwazo pamoja na kudhulumiwa hiyo timu ya Chelsea kumetokana na yeye kuwa na dual citizenship, au ni kwa sababu yeye ni tajiri wa Urusi?
 
Mlimkwapua Liverpool wakina caicedo na yule mwenzake airport mkashangilia na ma-hope ya kutosha, leo hii 😅😅😅😅
 
Kwa hiyo Taifa lake mama kati ya Urusi na Israel ni lipi? Israel, au Urusi? Na hivyo vikwazo pamoja na kudhulumiwa hiyo timu ya Chelsea kumetokana na yeye kuwa na dual citizenship, au ni kwa sababu yeye ni tajiri wa Urusi?
Sababu ilikua yy ni rafiki wa karibu wa putin

ukiacha hivo Russia inaongozwa na Rais ndio lakn uchumi wa nchi uko chin ya hao matajir ambao ni kina Roman

Kuna biashara pia amekua akifanya Roman ambazo kwa upande furan Roman ibra anahusika kwenye vita indirect
 
Back
Top Bottom