Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Mambo mengine ni mazingira. Ukiwa katika mazingira ya wanywaji ni vigumu kuepuka kunywa.Hongera, wengine tunajaribu lkn tunashindwa, ukijitahidi sana mwezi, siku nikifungulia Sasa lazima nifidie hicho kipindi ambacho nilipumzika, yaani ni balaa tupu....sijui nakwama wapi?
Mengine ni uwezo wa mtu binafsi kuepuka vishawishi.
Kwa upande wangu sina tatizo la mazingira wala la uwezo wangu binafsi kuepuka kunywa.
Kwa mfano, kila nikiamua kuacha kunywa, ni lazima niwe na pombe nyumbani. Sasa hivi nina Scotch, nina Vodka, nina Tequila, nina wine nina beer ndani ya nyumba. Tena nyingine naziona kila siku.
Tena kama beer kuna friji la garage kila nikifungua naona beer baridiii.
Lakini nazipotezea tu.