Chris wood
JF-Expert Member
- Dec 21, 2020
- 1,667
- 5,043
- Thread starter
-
- #201
Daa sijawahi kuona mtu analiwa 20M na bado yuko happy.Tatizo lako unafanya betting kama kazi,ikutoe kimaisha,kitu ambacho kamwe hakiwezekani!!
Wenzako wanafanya betting kama starehe tu,analiwa 20M na still yuko happy hana hata wasiwasi! Hivi unajua betting wanafanya matajiri, mchezo akipigwa anapigwa kweli,na akibutua, anabutua kweli!
Bora kukimbia ndugu.Betting ni nouma , watu wanapigwa Sana kwenye betting sema hawakwambii wanakwambia Tu mwanangu Jana nimeweka 3000 nikapiga laki mbili , Ila ukimwangalia jamaa hata Kula yake ni ya shida , aisee mi nilijarbu nilikula vitasa si vya nchi hii nikaamua kurun away
Akijilipua kama hivyo mara 3 kwisha habari yake.Huyu mwamba kajilipua haswaaa.
Kama bado uko chuo, soma sana mdogo anguMze
Mzee baba achana na betting,tuachie Sisi tunayo upepo nayo mpaka najutia shule nlienda kufanya nn
PSG kachana, ilikua niamke na pesa ya idd...beti pesa ambayo upo tayari kuipoteza mkuu,..Mimi leo nimeliwa Laki Tatu. Nilichogundua betting sio njia ya kutokea kimaisha. Betting hutakiwi kuifanya kama kazi. Yote kwa yote betting ni hasara.
Ahaaaaaa hii sentesi ndio imeniacha hoi sanaBaada ya vipigo kuzidi, huwa kuna msemo wanasema sikiliza wataalamu inaonekana strategies unazotumia sio salama, Hao wanaojiita watalamu watakwambia usiweke timu nyingi weka timu chache ,"tafuta odds mbili halafu tia laki," Aloo huo msemo ndio umenifukia kabisa hadi sasa naandika hapa sina hata mia mbovu.
Na mimi kwa kauli hii rasmi naachaHata mimi nakubaliana na wewe leo kuwa Betting ni laana tena laana mbaya sana.
Kuna jamaa namfahamu alianza Betting tangu mwaka 2007 wakati huo wengi wenu mlikuwa hata hamjui Betting ni kitu gani.
Ni miaka karibia 14 imepita na jamaa amefilisika kabisa , amechoka mbaya sana, mpaka sura yake imeharibika, amezeeka kabla ya wakati.
Nilikutana naye mwezi uliopita sikuamini kama ni yeye kwa jinsi alivyochakaa. Kwa sababu alikuwa ni rafiki yangu wa karibu sana, ikabidi anieleze ukweli wake kuwa kilichomfilisi na kumkongoroa ni betting.
Kwa kifupi jamaa anajuta na anasema kwa kipindi cha miaka 14 amepoteza mamilioni ya pesa kwenye sports betting na online casino.
Kama wewe umeamua kuacha, umefanya uamuzi sahihi kabisa.
Ukiweza kuacha basi acha kabisa ndugu yangu. Tokea siku nimekutana na jamaa yangu hata mimi nimeacha kabisa na sitaki tena kusikia ujinga wa Betting.Na mm kwa kauli hii rasmi naacha
Tupe hizo mbinu mkuuLabda Kama unaweka direct win ndo zinawaua wengi lakin kuna mbinu nying za kupata pesa ukiachana na direct win
Kwenye uzi wa kuacha betting, watu wanatoa hasara za betting...mwamba umewaona wazinguaji..unaomba mbinu, safi sanaaTupe hizo mbinu mkuu
Betting ni hasara, imelalia upande mmojaKipimo halisi cha kuacha bet sio kwa jaziba ukiwa umeshapigwa hivi. ukibahatika kupata pesa tena hicho ndio kipimo, ukiwa nazo pesa ukajikana nilizo nazo zanitosha na ni jasho langu kule namtengenezea muhindi njia unaweza sema unaacha betting.
Mi mpaka sasa nina damage kubwa sana kupitia betting pesa kubwa nimewahi shinda mara moja ni milioni 3,250,000TZS six numbers kwenye keno meridian bet, mpira nashinda pesa ndogo ndogo nishawahi kusanya 1.3Mil sema mpaka sasa bado ngoma ni nzito.
Ni hasara kubwa sana ndugu. Bora ulevi wa pombe kuliko ulevi wa kubetMimi leo nimeliwa Laki Tatu. Nilichogundua betting sio njia ya kutokea kimaisha. Betting hutakiwi kuifanya kama kazi. Yote kwa yote betting ni hasara.
Nimeshajaribu karibia kila aina ya mchezo na option tofauti tofauti hakuna unafuuuWale wazee wa spin, keno, farasi huko betshop hapafai, mpira nao kuna muda unakuwaga nuksi unatafuta odds 2 tu au 3 unatia laki lakini bado ni maumivu unacheza timu tatu zinakupa 2 odds ila wapi?
Kweli ndugu betting inafirisi kila kitu, fedha,Muda, unaweza jikuta unazeeka huku pesa yote umefaidisha haya makampuniHata mimi nakubaliana na wewe leo kuwa Betting ni laana tena laana mbaya sana.
Kuna jamaa namfahamu alianza Betting tangu mwaka 2007 wakati huo wengi wenu mlikuwa hata hamjui Betting ni kitu gani.
Ni miaka karibia 14 imepita na jamaa amefilisika kabisa , amechoka mbaya sana, mpaka sura yake imeharibika, amezeeka kabla ya wakati.
Nilikutana naye mwezi uliopita sikuamini kama ni yeye kwa jinsi alivyochakaa. Kwa sababu alikuwa ni rafiki yangu wa karibu sana, ikabidi anieleze ukweli wake kuwa kilichomfilisi na kumkongoroa ni betting.
Kwa kifupi jamaa anajuta na anasema kwa kipindi cha miaka 14 amepoteza mamilioni ya pesa kwenye sports betting na online casino. Kama wewe umeamua kuacha, umefanya uamuzi sahihi kabisa.
Shida ninayoiona hapa ni kurukia betting kwa pupa kwa imani kuwa inaenda kukufanya kuwa milionea kwa sekunde chache. Hiyo mentality ndio inaangamiza vijana wa kitanzania. Kuna principles za kujifunza katika betting na inatakiwa kuwa na nidhamu kubwa sana ili kufikia mafanikio. Ndio maana nakua na kiu ya kujifunza mbinu mbalimbali za betting. Pia tambua kuwa betting ni bahati kwa asilimia zaidi ya 80, so ukiweka juhudi za kujifunza, ukatambua miiko yake na ukawa na nyota ya bahati, then, one day itakuwa YES.Kwenye uzi wa kuacha betting, watu wanatoa hasara za betting...mwamba umewaona wazinguaji..unaomba mbinu, safi sanaa