Rasmi nimeamua kuachana na betting. Kubet ni kutafuta umasikini na ufukara

Betting is easier carabao inapoanza. Uefa na Europa zinapoanza.

Mwanzoni mwa ligi.

Also usikimbilie kuziba pengo la hasara. Ukijiona unalose dawa siyo kubet na kubet kucover hii hasara.

Anyway, hua nabet ili kujua kama timu niliyoifuatilia for some time itaact vile nimetarajia so hua naweka amounts comedy.
 
Kweli mkuu betting hapana, ninaroho ngumu lakini nimesarenda
Hahaha umefuata nilichofanya. Mimi nilikuwa nabet japo haikuwa kazi ila stake zangu zilikuwa zimeshiba kuanzia 50,000 na kuendelea mpaka lak kadhaa huko. Kuna siku nilipigwa kipigo kitakatifu ilikuwa mwaka juzi, nikataka rudisha nilichopigwa nikapewa tena. Nikaapa kuwa sitobet tena na toka siku hiyo mwaka juzi sijawahi kubet tena.
 
Weka mbali na watoto betting, haitoi kila mtu kwenye maisha nawaona watu kila siku wamejaa betting na nje hamna hata IST mbovu ikiwa imepaki
Betting inaamisha pesa kutoka kwa masikini kwenda kwa masonko.
 
Hizo hela za betting ungeamua kununua vitu vya geto, ungekuwa mbali sana.
Kamari haiwezi kukutoa kimaisha. Vijana wengi mnadanganyana sana vijiweni.
Fanya kazi na Mungu ataibariki kazi ya mikono yako
Kabisa ndugu betting ni disaster
 
Jambo la maana bora kutumia kidogo ulichonacho kuliko kutamani vikubwa ,visivyowezekana
 
Nmekusukiliza kwa umakini mkubwa sana ndgu.kwanza pole sana. mkuu kuna watu wana kunja mpaka 4m kila week kupitia betting. kuna watu wameecha kazi kabisa wao wana bet tu. tatizo hawaji kutoa shuhuda humu

kwenye betting kuna masoko zaid ya 170. kwenye hayo wewe endelea kujitafuta uone soko litakalo ku favour wew. Hauwez kufikia kutengeneza pesa nzuri ya mfululizo kama hujajuwa soko lipi kwako ni sahihi. Mimi nna maika 2 ya kuliwa. Nmefail chuo sababu ya stress za betting (sio kudiscow). kwa nilivo kuona umesoma uchumi au statistics kwa kupita comments zako humu

kuwa mvumilivu na mtulivu tu.kuna pesa nyingi sana ipo humo kwenye betting nadhan hujajuwa soko lako unaloliweza.mimi juzi nmepoteza 2.5m. kijinga tu hyo ni faida niliyotengeneza


zingatia yafuatayo
i) nidhamu
ii) kutokuwa na tamaa
iii)kumbuka ukipata faida kufanya kitu au miradi inayo onekana.mfano umepata milion 5 nunua boda boda fasta zianze kufanya kazi.siku uki drop zina kuinua
iv)kuwa na limit ya kubet na malengo
v) betting inahitaji uwekeze pesa sio ikupe pesa.ni investment ka investments nyingine.pale huend kuchota pesa pale unawekeza

NB
kila la kheri mkuu.gamble what you afford to loose
 
Mnaoiponda betting hamna lolote, ni wivu tu! Watu tunaweka mikeka tunaliwa sanaaa, lakini sometime tunamdaka mhindi vile vile, imagine stake ya 20k inakuletea 10m hata upigwe vipi lazma wewe ni winner tu! Huwez fananisha betting na tatu mzuka au biko. Madrid kafungwa unaona kabsaa! Siyo zile za kuzungusha gurudumu
 
Kumbe Bado Unaendeshwa Na Maono Ya Bahat Basi Cheza Biko.

Bahat Ni Kitu Cha Ziada Tu Kene Maisha, Betting Ni Kazi Ndo Maana Tunawekeza Muda Na Pesa. Kubali Tu Mzee Hujui Kubet Ulikuwa Unatuchangia Wengine
Ni Suala La Muda Tuu... Kuna siku utatamani kumeza haya maandishi
 
Man Ungelijua Kila Kazi Inachangamoto Zake Na Kila Biashara Haikosi Hasara Usingekuwa Na Maneno Mengi. Kwa Ufupi Ulifanya Kitu Usichokijua, Betting Haimtaki Mtu Mwenye Kichwa Cha Kufugia Nywele
Acha Kudanganya Watu.... Betting Uwezekano was Kupoteza Ni Mkubwa Sana kuliko kupata... Jifanye Mjanja Tena Wewe Ni Suala la Muda Tuu utakuja Kajinyonga Endelea Kuendekeza Kamari... Usijisifu eti Ni Mjanja Hakuna Mtu Mwenye Akili atawekeza Akili yake Kwenye Kamari... Wengi wetu Ni Wahanga Tumeshaona Madhara ya Huu Upumbavu .....
 
Mkuu umeongea kwa uchungu sana inaonekana umesulubiwa sana kama mimi.[emoji23]
 
500k!!!. Kuna mawili
1. Wewe ni papaa mwenye fweza zakutosha
2. Una roho ngumu sana.
 
Hivi yule alieshinda NUSU BILLION utamwambia nini kuhusu betting akuelewe?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…