hamis77
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 18,678
- 27,653
Kutokana na haya yanayotokea katika nchi yetu, tumeona TEC wakitoa msimamo wao msimamo wa kusimamia haki, kutetea wanyonge na kusimama na Watanzania bila woga.
Maandiko yanasema👇👇
“Fungua kinywa chako kwa ajili ya bubu… hukumu kwa haki, mtetee mnyonge na maskini.” (Mithali 31:8–9)
“Jifundisheni kutenda mema; tafuteni haki; mkemeni mnyanyasaji.” (Isaya 1:17)
Tuwaseme tuwasemavyo TEC na wakatoliki kwa mapungufu Yao ila kwenye hili Mungu atawalipa tu ,
Lakini sehemu ninayosali mimi, sikuona hata kiongozi mmoja wa dini akitoa neno la pole, wala kukemea ukandamizwaji wa haki kwa watu wanaoonewa.
Maandiko yanasema 👇
“Ole wao wachungaji wanaojilisha nafsi zao na kuwaacha kondoo.” (Ezekieli 34:2)
Nilifanya mjadala na baadhi ya viongozi wa dini na wadau kwenye group za dini. Madai yao yalikuwa
• “Huu sio muda wa kusema.”
• “Kanisa halijihusishi na siasa.”
• “Muda ukifika tutasema.”
Lakini Biblia inatuonya kuhusu viongozi wa dini wanaokaa kimya wanapoona maovu.
“Walinzi wao ni vipofu… wachungaji wasio na ufahamu, kila mmoja anatamani faida yake.” (Isaya 56:10–11)
Kiukweli porojo zilikuwa nyingi… Nikawabana kwa hoja kwa sababu binafsi napenda haki. Naumia sana kumuona mtu akionewa kimyakimya.
Nimewahi kuwa ngazi ya juu kwenye kampuni moja, na nilihakikisha kila mfanyakazi anatendewa haki, walipata stahiki zao, hawakunyanyaswa, walikula chakula cha hadhi. Mpaka leo miaka miwili baada ya kuondoka bado hawajawahi kunisahau., am proud kwakweli
Ninachotaka kusema ni hiki…
Niliona unafiki mkubwa kutoka kwa baadhi ya viongozi wa kanisa. Nikawaambia wazi
“Mnasema siasa si ya kanisa, lakini wanasiasa wakija hapa mnawaombea. Wakileta zawadi mnazipokea. Lakini wakikosea hamuwakemei. Huu ni unafiki.”
Yesu mwenyewe aliwakemea viongozi wa dini wa aina hii ,alisema 👇
“Ole wenu walimu wa sheria na Mafarisayo wanafiki…” (Mathayo 23:27)
“Watu hawa huniheshimu kwa midomo, lakini mioyo yao iko mbali nami.” (Mathayo 15:7–8)
Mitume na manabii kama Eliya hawakufanya hivyo hawakunyamaza walipokutana na dhuluma.
Nikawapa mfano wa jinsi TEC wanavyosimama na walioonewa wanavyokemea mabaya, utekaji, rushwa na dhuluma.
Nikawaambia..👇
“Mnafikiri Mungu atawaacha hawa wanaolia na kutetea haki? Kamwe!”
“Teteni maskini na yatima… waokoeni wasio na nguvu na wahitaji.” (Zaburi 82:3–4)
“Haki na itiririke kama maji.” (Amosi 5:24)
Kuna mfano Yesu alitoa wa mtu aliyepigwa na majambazi.
Lakini walipopita Kuhani na Mlawi(Hawa ni viongozi wa dini wa juu kabisa wanaoijua Torati vizuri sana) walimpita na kumuacha.
Hawa ndio viongozi wa dini ambao walipaswa kutetea haki lakini wakaacha mtu akifa.
Lakini Msamaria, ambaye kwa Wayahudi alionekana najisi, ndiye aliyemsaidia, akamfunga majeraha, akampandisha juu ya punda wake, akampeleka nyumba ya wageni na kugharamia matibabu yake.
Yesu alionesha wazi👇👇
Mara nyingi wanaojiita viongozi wa dini ndio wa mwisho kutenda haki, na wasioheshimiwa ndio hutimiza mapenzi ya Mungu.,
🤝 Nawapongeza TEC
Kiukweli niwapongeze sana TEC.
Wakatoliki, simameni imara.
Viongozi wenu wamesimama na ukweli, wakati makanisa mengi yameamua kunyamaza kimya.
Kwa upande wa Waislamu, sehemu kubwa ya masheikh wameamua kuwa wasemaji wa watawala japo sio wote.
Maamuzi Yangu Mimi
Kwa sababu ya kuona unafiki huu wa viongozi wa dini mahali ninaposali, nimeamua jambo moja:
NITAHAMISHA IBADA YA MUNGU NYUMBANI KWANGU ,UZURI MIMI NI MWANATHEOLOJIA ,....
Ibada yangu, ya familia yangu, na Mungu wangu mwenyewe.
Kwa nini?
Kwa sababu uhusiano wa Mungu na mwanadamu ni binafsi.
Jengo siyo linalofanya Mungu awepo ni mioyo ya wanaomwita kwa ukweli.
“Kwa maana walipo wawili au watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo kati yao.” (Mathayo 18:20)
Na Biblia inaonyesha wazi kuwa ibada za mitume na Wakristo wa kwanza zilifanyika majumbani:
• “Walikuwa wakiumega mkate majumbani.” (Matendo 2:46)
• “Sikuacha kuwafundisha hadharani na nyumbani kwa watu.” (Matendo 20:20)
• “Salimuni kanisa lililo nyumbani kwao.” (Warumi 16:5)
• “Na lile kanisa lililo nyumbani kwao.” (Wakolosai 4:15)
Ibada ya nyumbani ni ya kibiblia kabisa si jambo jipya.,
Kuhusu Sadaka
Mimi ni muumini wa kuwasaidia:
• watoto yatima
• wajane
• wafungwa
• wasiojiweza
“Dini iliyo safi mbele za Mungu ni hii: kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao.” (Yakobo 1:27)
“Amtendeaye fadhili maskini anamkopesha Bwana.” (Methali 19:17)
“Mliowatendea hawa wadogo, mmeni tendea mimi.” (Mathayo 25:35–40)
Sadaka yangu haitapitia kwa viongozi wanaotafuta faida—itaenda kwa wahitaji moja kwa moja, kama Biblia inavyofundisha.
Kwa sasa, nimeamua rasmi kuhamishia ibada nyumbani kwangu na familia yangu.
Tutapanga ratiba, tutasoma Neno, tutaomba, tutaimba na Mungu atakaa pamoja nasi.
Kwa sababu
Mungu haishi kwenye majengo anaishi katika mioyo ya wanaotenda haki na kusema kweli.
Amen