Rasmi nimehamishia ibada nyumbani sababu ya unafiki wa viongozi wa dini

Watakwambia muda bdo wanasubiri dhiki kuu.km mziki wa samia wameshndwa dhiki kuu watauweweza?fikiri hakuna wasabato waliouawa? wameshndwa nn kusema neno hata ya kufariji waumini wao na kulaani yal4yotokea?wanashndwa hata mzee wa upako.
Sindio hapo sasa ,Mimi nimewaambia ukweli ,
 
Hamia kanisani kwangu ndugu uniletee mimi kimbaumbau hizo sadaka, kuliko kuendelea kupelekea hao vitambi kama stoo za Yusufu kule Misri, mimi sinaga unafiki maana huwa nawachana fleshi tu humu hata wakiweka kiraka nachana tena na nyote ni mashahidi humu.
 
Kutokana na haya yanayotokea katika nchi yetu, tumeona TEC wakitoa msimamo wao msimamo wa kusimamia haki, kutetea wanyonge na kusimama na Watanzania bila woga.

Maandiko yanasema👇👇
“Fungua kinywa chako kwa ajili ya bubu… hukumu kwa haki, mtetee mnyonge na maskini.” (Mithali 31:8–9)
“Jifundisheni kutenda mema; tafuteni haki; mkemeni mnyanyasaji.” (Isaya 1:17)

Tuwaseme tuwasemavyo TEC na wakatoliki kwa mapungufu Yao ila kwenye hili Mungu atawalipa tu ,

Lakini sehemu ninayosali mimi, sikuona hata kiongozi mmoja wa dini akitoa neno la pole, wala kukemea ukandamizwaji wa haki kwa watu wanaoonewa.
Maandiko yanasema 👇
“Ole wao wachungaji wanaojilisha nafsi zao na kuwaacha kondoo.” (Ezekieli 34:2)

Nilifanya mjadala na baadhi ya viongozi wa dini na wadau kwenye group za dini. Madai yao yalikuwa

• “Huu sio muda wa kusema.”
• “Kanisa halijihusishi na siasa.”
• “Muda ukifika tutasema.”

Lakini Biblia inatuonya kuhusu viongozi wa dini wanaokaa kimya wanapoona maovu.

“Walinzi wao ni vipofu… wachungaji wasio na ufahamu, kila mmoja anatamani faida yake.” (Isaya 56:10–11)

Kiukweli porojo zilikuwa nyingi… Nikawabana kwa hoja kwa sababu binafsi napenda haki. Naumia sana kumuona mtu akionewa kimyakimya.

Nimewahi kuwa ngazi ya juu kwenye kampuni moja, na nilihakikisha kila mfanyakazi anatendewa haki, walipata stahiki zao, hawakunyanyaswa, walikula chakula cha hadhi. Mpaka leo miaka miwili baada ya kuondoka bado hawajawahi kunisahau., am proud kwakweli

Ninachotaka kusema ni hiki…

Niliona unafiki mkubwa kutoka kwa baadhi ya viongozi wa kanisa. Nikawaambia wazi

“Mnasema siasa si ya kanisa, lakini wanasiasa wakija hapa mnawaombea. Wakileta zawadi mnazipokea. Lakini wakikosea hamuwakemei. Huu ni unafiki.”

Yesu mwenyewe aliwakemea viongozi wa dini wa aina hii ,alisema 👇
“Ole wenu walimu wa sheria na Mafarisayo wanafiki…” (Mathayo 23:27)
“Watu hawa huniheshimu kwa midomo, lakini mioyo yao iko mbali nami.” (Mathayo 15:7–8)

Mitume na manabii kama Eliya hawakufanya hivyo hawakunyamaza walipokutana na dhuluma.

Nikawapa mfano wa jinsi TEC wanavyosimama na walioonewa wanavyokemea mabaya, utekaji, rushwa na dhuluma.

Nikawaambia..👇

“Mnafikiri Mungu atawaacha hawa wanaolia na kutetea haki? Kamwe!”
“Teteni maskini na yatima… waokoeni wasio na nguvu na wahitaji.” (Zaburi 82:3–4)
“Haki na itiririke kama maji.” (Amosi 5:24)

Kuna mfano Yesu alitoa wa mtu aliyepigwa na majambazi.

Lakini walipopita Kuhani na Mlawi(Hawa ni viongozi wa dini wa juu kabisa wanaoijua Torati vizuri sana) walimpita na kumuacha.
Hawa ndio viongozi wa dini ambao walipaswa kutetea haki lakini wakaacha mtu akifa.

Lakini Msamaria, ambaye kwa Wayahudi alionekana najisi, ndiye aliyemsaidia, akamfunga majeraha, akampandisha juu ya punda wake, akampeleka nyumba ya wageni na kugharamia matibabu yake.

Yesu alionesha wazi👇👇

Mara nyingi wanaojiita viongozi wa dini ndio wa mwisho kutenda haki, na wasioheshimiwa ndio hutimiza mapenzi ya Mungu.,

🤝 Nawapongeza TEC

Kiukweli niwapongeze sana TEC.
Wakatoliki, simameni imara.
Viongozi wenu wamesimama na ukweli, wakati makanisa mengi yameamua kunyamaza kimya.

Kwa upande wa Waislamu, sehemu kubwa ya masheikh wameamua kuwa wasemaji wa watawala japo sio wote.

Maamuzi Yangu Mimi

Kwa sababu ya kuona unafiki huu wa viongozi wa dini mahali ninaposali, nimeamua jambo moja:

NITAHAMISHA IBADA YA MUNGU NYUMBANI KWANGU ,UZURI MIMI NI MWANATHEOLOJIA ,....

Ibada yangu, ya familia yangu, na Mungu wangu mwenyewe.

Kwa nini?

Kwa sababu uhusiano wa Mungu na mwanadamu ni binafsi.
Jengo siyo linalofanya Mungu awepo ni mioyo ya wanaomwita kwa ukweli.

“Kwa maana walipo wawili au watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo kati yao.” (Mathayo 18:20)

Na Biblia inaonyesha wazi kuwa ibada za mitume na Wakristo wa kwanza zilifanyika majumbani:

• “Walikuwa wakiumega mkate majumbani.” (Matendo 2:46)
• “Sikuacha kuwafundisha hadharani na nyumbani kwa watu.” (Matendo 20:20)
• “Salimuni kanisa lililo nyumbani kwao.” (Warumi 16:5)
• “Na lile kanisa lililo nyumbani kwao.” (Wakolosai 4:15)

Ibada ya nyumbani ni ya kibiblia kabisa si jambo jipya.,

Kuhusu Sadaka

Mimi ni muumini wa kuwasaidia:

• watoto yatima
• wajane
• wafungwa
• wasiojiweza

“Dini iliyo safi mbele za Mungu ni hii: kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao.” (Yakobo 1:27)
“Amtendeaye fadhili maskini anamkopesha Bwana.” (Methali 19:17)
“Mliowatendea hawa wadogo, mmeni tendea mimi.” (Mathayo 25:35–40)

Sadaka yangu haitapitia kwa viongozi wanaotafuta faida—itaenda kwa wahitaji moja kwa moja, kama Biblia inavyofundisha.

Kwa sasa, nimeamua rasmi kuhamishia ibada nyumbani kwangu na familia yangu.
Tutapanga ratiba, tutasoma Neno, tutaomba, tutaimba na Mungu atakaa pamoja nasi.

Kwa sababu
Mungu haishi kwenye majengo anaishi katika mioyo ya wanaotenda haki na kusema kweli.

Amen
Hujachelewa jomba, karibu Kanisa Moja Takatifu Katoliki la Mitume!
 
Inaonekana ushahama kwng tu cz ulianza kwa kina shekhe ila bdo uliendelea kutafuta palipo na ukwel hadi umejagundua kuwa mwenyew tu unaweza kufanya ibada na ikapokelewa....ila kwa kwel RC wameondoka na point zao 3 kwq kuonesha kwamba hawayumbishwi
 
Wamekuwa na tabia za bakwata
Napingana na wewe, hawana tabia za bwakwata ila hawasemi chochote kuhusu siasa coz wameamua kutojifungamanisha na wanasiasa.

Kazi ya kanisa ni kuonya watu dhidi ya maovu yao na utume. Hiyo ndio kazi ya kanisa, siasa tuwaachie wanasiasa, ila wakikengeuka waonywe. Binafsi nakubali wanachofanya TEC kwa asilimia fulani, sio 100%.
 
Uko sawa tu mbona Mkuu.
Hospital kubwa na ya Dini kama KCMC mpaka Leo hawajaongea kama walipokea miili au majeruhi wa Maandamano ya 29 Oktoba,2025 ni kimyaaa hakuna nywinywinywi Wala....Pana Siri Gani hapooo??!
 
Kutokana na haya yanayotokea katika nchi yetu, tumeona TEC wakitoa msimamo wao msimamo wa kusimamia haki, kutetea wanyonge na kusimama na Watanzania bila woga.

Maandiko yanasema👇👇
“Fungua kinywa chako kwa ajili ya bubu… hukumu kwa haki, mtetee mnyonge na maskini.” (Mithali 31:8–9)
“Jifundisheni kutenda mema; tafuteni haki; mkemeni mnyanyasaji.” (Isaya 1:17)

Tuwaseme tuwasemavyo TEC na wakatoliki kwa mapungufu Yao ila kwenye hili Mungu atawalipa tu ,

Lakini sehemu ninayosali mimi, sikuona hata kiongozi mmoja wa dini akitoa neno la pole, wala kukemea ukandamizwaji wa haki kwa watu wanaoonewa.
Maandiko yanasema 👇
“Ole wao wachungaji wanaojilisha nafsi zao na kuwaacha kondoo.” (Ezekieli 34:2)

Nilifanya mjadala na baadhi ya viongozi wa dini na wadau kwenye group za dini. Madai yao yalikuwa

• “Huu sio muda wa kusema.”
• “Kanisa halijihusishi na siasa.”
• “Muda ukifika tutasema.”

Lakini Biblia inatuonya kuhusu viongozi wa dini wanaokaa kimya wanapoona maovu.

“Walinzi wao ni vipofu… wachungaji wasio na ufahamu, kila mmoja anatamani faida yake.” (Isaya 56:10–11)

Kiukweli porojo zilikuwa nyingi… Nikawabana kwa hoja kwa sababu binafsi napenda haki. Naumia sana kumuona mtu akionewa kimyakimya.

Nimewahi kuwa ngazi ya juu kwenye kampuni moja, na nilihakikisha kila mfanyakazi anatendewa haki, walipata stahiki zao, hawakunyanyaswa, walikula chakula cha hadhi. Mpaka leo miaka miwili baada ya kuondoka bado hawajawahi kunisahau., am proud kwakweli

Ninachotaka kusema ni hiki…

Niliona unafiki mkubwa kutoka kwa baadhi ya viongozi wa kanisa. Nikawaambia wazi

“Mnasema siasa si ya kanisa, lakini wanasiasa wakija hapa mnawaombea. Wakileta zawadi mnazipokea. Lakini wakikosea hamuwakemei. Huu ni unafiki.”

Yesu mwenyewe aliwakemea viongozi wa dini wa aina hii ,alisema 👇
“Ole wenu walimu wa sheria na Mafarisayo wanafiki…” (Mathayo 23:27)
“Watu hawa huniheshimu kwa midomo, lakini mioyo yao iko mbali nami.” (Mathayo 15:7–8)

Mitume na manabii kama Eliya hawakufanya hivyo hawakunyamaza walipokutana na dhuluma.

Nikawapa mfano wa jinsi TEC wanavyosimama na walioonewa wanavyokemea mabaya, utekaji, rushwa na dhuluma.

Nikawaambia..👇

“Mnafikiri Mungu atawaacha hawa wanaolia na kutetea haki? Kamwe!”
“Teteni maskini na yatima… waokoeni wasio na nguvu na wahitaji.” (Zaburi 82:3–4)
“Haki na itiririke kama maji.” (Amosi 5:24)

Kuna mfano Yesu alitoa wa mtu aliyepigwa na majambazi.

Lakini walipopita Kuhani na Mlawi(Hawa ni viongozi wa dini wa juu kabisa wanaoijua Torati vizuri sana) walimpita na kumuacha.
Hawa ndio viongozi wa dini ambao walipaswa kutetea haki lakini wakaacha mtu akifa.

Lakini Msamaria, ambaye kwa Wayahudi alionekana najisi, ndiye aliyemsaidia, akamfunga majeraha, akampandisha juu ya punda wake, akampeleka nyumba ya wageni na kugharamia matibabu yake.

Yesu alionesha wazi👇👇

Mara nyingi wanaojiita viongozi wa dini ndio wa mwisho kutenda haki, na wasioheshimiwa ndio hutimiza mapenzi ya Mungu.,

🤝 Nawapongeza TEC

Kiukweli niwapongeze sana TEC.
Wakatoliki, simameni imara.
Viongozi wenu wamesimama na ukweli, wakati makanisa mengi yameamua kunyamaza kimya.

Kwa upande wa Waislamu, sehemu kubwa ya masheikh wameamua kuwa wasemaji wa watawala japo sio wote.

Maamuzi Yangu Mimi

Kwa sababu ya kuona unafiki huu wa viongozi wa dini mahali ninaposali, nimeamua jambo moja:

NITAHAMISHA IBADA YA MUNGU NYUMBANI KWANGU ,UZURI MIMI NI MWANATHEOLOJIA ,....

Ibada yangu, ya familia yangu, na Mungu wangu mwenyewe.

Kwa nini?

Kwa sababu uhusiano wa Mungu na mwanadamu ni binafsi.
Jengo siyo linalofanya Mungu awepo ni mioyo ya wanaomwita kwa ukweli.

“Kwa maana walipo wawili au watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo kati yao.” (Mathayo 18:20)

Na Biblia inaonyesha wazi kuwa ibada za mitume na Wakristo wa kwanza zilifanyika majumbani:

• “Walikuwa wakiumega mkate majumbani.” (Matendo 2:46)
• “Sikuacha kuwafundisha hadharani na nyumbani kwa watu.” (Matendo 20:20)
• “Salimuni kanisa lililo nyumbani kwao.” (Warumi 16:5)
• “Na lile kanisa lililo nyumbani kwao.” (Wakolosai 4:15)

Ibada ya nyumbani ni ya kibiblia kabisa si jambo jipya.,

Kuhusu Sadaka

Mimi ni muumini wa kuwasaidia:

• watoto yatima
• wajane
• wafungwa
• wasiojiweza

“Dini iliyo safi mbele za Mungu ni hii: kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao.” (Yakobo 1:27)
“Amtendeaye fadhili maskini anamkopesha Bwana.” (Methali 19:17)
“Mliowatendea hawa wadogo, mmeni tendea mimi.” (Mathayo 25:35–40)

Sadaka yangu haitapitia kwa viongozi wanaotafuta faida—itaenda kwa wahitaji moja kwa moja, kama Biblia inavyofundisha.

Kwa sasa, nimeamua rasmi kuhamishia ibada nyumbani kwangu na familia yangu.
Tutapanga ratiba, tutasoma Neno, tutaomba, tutaimba na Mungu atakaa pamoja nasi.

Kwa sababu
Mungu haishi kwenye majengo anaishi katika mioyo ya wanaotenda haki na kusema kweli.

Amen

Kuleta hoja za uongo za kupinga uislamu na kutukana mtume wetu pia umewacha ??
 
Back
Top Bottom