GE2025 Rasmi: Pingamizi la Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya Mpina lakubaliwa. Tume yamnyoa, ACT yakosa mgombea urais

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Hakuwa anayajua

After all, ACT imekuwa Chaguo la 3 la Mpina baada ya CCM na CDM

Mwanzoni Mpina alikuwa aende CDM iwapo ingeshiriki Uchaguzi huu

Ndiyo maana alianza kuvaa nguo zinazo shabihiana na Kombati za CDM zile nyeusi

Wanasiasa wajanja Sana mkuu , kwanza sio kawaida yake mpina kukaa kimya.

A na B yanaweza kuwa majibu kaamua kuipa Ccm 99.9% either kwa kujua au kwa kutokujua.
 
Ni kweli usemacho Mkuu

Hata ile kauli ya Nchimbi akiwa Kisesa, huenda ni mwanzo wa safari ya Mpina kurudi alipotoka (CCM)
Hao akina Mpina , Zitto , Mbowe n.k

Ukifatilia there's so many things to lose .

Wengi unakuta ni wafanyabiashara ambao wanafaidika na mfumo wa Ccm indirect na direct kuanzia Kodi n.k

Hata wakikosoa , wanakosoa Ila hawana uwezo wa kui challenge Sana Serikali kwakuwa wanajua wataweka biashara zao hatarini .

Mfanyabiashara mkubwa au wa kati anapoingia katika siasa wengi wanaingia kimkakati haijalishi iwe Ccm au upinzani .
 
Tume imekubali pingamizi lililowasilishwa na Ndugu Hamza Saidi Johari Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya uteuzi wa Ndugu Luhaga Joelson Mpina kuwa mgombea wa kiti cha Rais kupitia Chama cha ACT-Wazalendo.

Hivyo, jina la Ndugu Luhaga Joelson Mpina, mgombea wa kiti cha Rais kupitia Chama cha ACT-Wazalendo limeondolewa kwenye orodha ya wagombea wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.

Soma Pia: Mpina ashinda kesi kuenguliwa kuwa mgombea Urais

Aidha, mapingamizi yaliyowekwa wa Mgombea wa CCM, Samia Suluhu Hassan yametupiliwa mbali.

View attachment 3472514

View attachment 3472515View attachment 3472516
Kwanini Mgombea wa 100bn hataki mpinzani WA kweli kwenye uchaguzi huu 2025 .
Je ana mapungufu Gani kiasi kwamba anaona hawezi kushindana na na ntu, au ana Nia ipi ya Mama Tanzania.

Na mwenye kutafsiri Sheria ni Mahakama au hiyo tume.

Na je hizo Kanuni za Vyama zipo juu ya Sheria kuu au katiba yetu juu Haki ya mtu kushiriki na kuchaguliwa
 
Hao akina Mpina , Zitto , Mbowe n.k

Ukifatilia there's so many things to lose .

Wengi unakuta ni wafanyabiashara ambao wanafaidika na mfumo wa Ccm indirect na direct kuanzia Kodi n.k

Hata wakikosoa , wanakosoa Ila hawana uwezo wa kui challenge Sana Serikali kwakuwa wanajua wataweka biashara zao hatarini .

Mfanyabiashara mkubwa au wa kati anapoingia katika siasa wengi wanaingia kimkakati haijalishi iwe Ccm au upinzani .
Nakuelewa sana Mkuu

Ndiyo maana zimetumika mbinu nyingi kuidhohofisha CDM Mwaka huu hadi ile ya kuomba mgawanyo wa Mali

Kosa la Kimkakati, anayeomba mgawanyo wa mali amehama na Chama kabisa 🙌
 
Yes , ni ujio wa Lissu ndo umeleta changamoto.

Aina ya maisha ya lissu yanamfanya kuwa mpinzani wa kweli - Ila Kama angekuwa Ana run kampuni na biashara kadhaa , wangetumia silaha ya kumuua kiuchumi .

Na kikawaida hofu ya kufirisika huwa ni kubwa na hapa Ccm wamekuwa wakitake advantage .

So Lissu has nothing to lose yale mambo yake msingi kwake yapo secured Kama Mke , watoto n.k.

MTU Kama Lissu angepatika wakati ndo tunaanza mfumo wa vyama vingi Vya siasa tungekuwa tumeitoa Ccm madarakani au Ccm kingekuwa chama chenye uwajibakaji mkubwa.
 
Tume imekubali pingamizi lililowasilishwa na Ndugu Hamza Saidi Johari Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya uteuzi wa Ndugu Luhaga Joelson Mpina kuwa mgombea wa kiti cha Rais kupitia Chama cha ACT-Wazalendo.

Hivyo, jina la Ndugu Luhaga Joelson Mpina, mgombea wa kiti cha Rais kupitia Chama cha ACT-Wazalendo limeondolewa kwenye orodha ya wagombea wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.

Soma Pia: Mpina ashinda kesi kuenguliwa kuwa mgombea Urais

Aidha, mapingamizi yaliyowekwa wa Mgombea wa CCM, Samia Suluhu Hassan yametupiliwa mbali.

View attachment 3472514

View attachment 3472515View attachment 3472516
Ni ujinga wa kiwango Cha Juu. Hebu fikiria
1. Tume imekataa kupokea fomu za Mpina.
2. Mahamakama yatengua uamuzi wa tume.
3. Tume imepokea na kumteua ndugu Mpina.
4. Tume imeondoa jina la Mpina baada ya pingamizi.
Which is which. Sinema na sarakasi tupu.
Anyway Mungu yachukue yote madharimu haya
 
Yes , ni ujio wa Lissu ndo umeleta changamoto.

Aina ya maisha ya lissu yanamfanya kuwa mpinzani wa kweli - Ila Kama angekuwa Ana run kampuni na biashara kadhaa , wangetumia silaha ya kumuua kiuchumi .

Na kikawaida hofu ya kufirisika huwa ni kubwa na hapa Ccm wamekuwa wakitake advantage .

So Lissu has nothing to lose yale mambo yake msingi kwake yapo secured Kama Mke , watoto n.k.

MTU Kama Lissu angepatika wakati ndo tunaanza mfumo wa vyama vingi Vya siasa tungekuwa tumeitoa Ccm madarakani au Ccm kingekuwa chama chenye uwajibakaji mkubwa.
Umesema sahihi kabisa Mkuu

Maendeleo ya Nchi yetu, yanapatikana Kwa mwendo wa kinyonga kutokana na wimbi la Viongozi wanaotuongoza kuwa wafanyabiashara

Bahati mbaya hata waliopo upinzani tangu Mwaka 95, wamekuwa wa aina hiyo ndiyo maana imekuwa vigumu

Lissu amekuja kuleta tumaini kidogo, japo changamoto anayopitia ni uungwaji Mkono

Hapati support ya kutosha kuanzia Kwa Wananchi na Vyombo vyenyewe vya Dola
 
KUHUSU UAMUZI WA PINGAMIZI ZA UTEUZI WA WAGOMBEA WA KITI CHA RAIS KWA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
DAR ES SALAAM, Tarehe 15 Septemba, 2025

Kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 37 cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya Mwaka 2024 kikisomwa pamoja na kanuni ya 22 ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani za Mwaka 2025, tarehe 13 Septemba, 2025, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ilipokea jumla ya mapingamizi matatu (03) dhidi ya uteuzi wa Ndugu Luhaga Joelson Mpina mgombea wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha ACT Wazalendo na tarehe 14 Septemba, 2025, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ilipokea pingamizi moja (01) dhidi ya uteuzi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan mgombea wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).

Tume katika kikao chake kilichofanyika tarehe 15 Septemba, 2025 imefanya uamuzi wa mapingamizi hayo manne (04) yaliyowasilishwa mbele yake, ambapo mapingamizi matatu (03) yamekataliwa na moja (01) limekubaliwa kama ifuatavyo:-

1. Mapingamizi yaliyokataliwa
Tume imekataa na kuyatupilia mbali mapingamizi matatu (03) kama ifuatavyo:-

i. Pingamizi lililowekwa na Ndugu Almas Hassan Kisabya mgombea wa kiti cha Rais kupitia Chama cha NRA dhidi ya Ndugu Luhaga Joelson Mpina mgombea wa Kiti cha Rais kupitia Chama cha ACT Wazalendo

Tume imekataa na kutupilia mbali pingamizi lililowekwa na Ndugu Almas Hassan Kisabya mgombea wa kiti cha Rais kupitia Chama cha NRA dhidi ya uteuzi wa Ndugu Luhaga Joelson Mpina kuwa mgombea wa kiti cha Rais kupitia Chama cha ACT-Wazalendo.

ii. Pingamizi lililowekwa na Ndugu Kunje Ngomale Mwiru mgombea kiti cha Rais kupitia chama cha AAFP dhidi ya Ndugu Luhaga Joelson Mpina mgombea wa Kiti cha Rais kupitia Chama cha ACT Wazalendo.

Tume imekataa na kutupilia mbali pingamizi lililowekwa na Ndugu Kunje Ngombale Mwiru mgombea wa kiti cha Rais kupitia Chama AAFP dhidi ya uteuzi wa Ndugu Luhaga Joelson Mpina mgombea wa kiti cha Rais kupitia Chama cha ACT-Wazalendo.

iii. Pingamizi lilowekwa na Ndugu Luhaga Joelson Mpina mgombea kupitia Chama cha ACT-Wazalendo dhidi ya Dkt. Samia Suluhu Hassan mgombea wa kiti cha Rais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Tume imekataa na kutupilia mbali pingamizi lililowekwa na Ndugu Luhaga Joelson Mpina dhidi ya uteuzi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan mgombea wa kiti cha Rais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).

2. Pingamizi lililokubaliwa
Tume imekubali pingamizi lililowasilishwa na Ndugu Hamza Saidi Johari Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya uteuzi wa Ndugu Luhaga Joelson Mpina kuwa mgombea wa kiti cha Rais kupitia Chama cha ACT-Wazalendo.

Hivyo, jina la Ndugu Luhaga Joelson Mpina, mgombea wa kiti cha Rais kupitia Chama cha ACT-Wazalendo limeondolewa kwenye orodha ya wagombea wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.

"KURA YAKO HAKI YAKO JITOKEZE KUPIGA KURA"

View attachment 3472511View attachment 3472512View attachment 3472513
Huu nao ni upumbavu
 
ZITO NI DALALI YUPO KWENYE KUNDI LA WAHUNI.ANAJUA KINACHOENDELEA.
 
Umesema sahihi kabisa Mkuu

Maendeleo ya Nchi yetu, yanapatikana Kwa mwendo wa kinyonga kutokana na wimbi la Viongozi wanaotuongoza kuwa wafanyabiashara

Bahati mbaya hata waliopo upinzani tangu Mwaka 95, wamekuwa wa aina hiyo ndiyo maana imekuwa vigumu

Lissu amekuja kuleta tumaini kidogo, japo changamoto anayopitia ni uungwaji Mkono

Hapati support ya kutosha kuanzia Kwa Wananchi na Vyombo vyenyewe vya Dola
True , naona hapewi sapoti ya kutosha Ila udhaifu mkubwa tulionao watz huwa hatushikirii jambo moja.

Mfano tukisemama tukomae na harakati ya NRNE hata miaka mitano lazima tungekuwa tumepata majibu hata Kama sio asilimia miamoja.

Ila katikati ya NREN ANAKIBUKA mtu kama polepole na yeye anataka kuondoka na hii ajenda .

Kitu ambacho kinaua nguvu .

Inawezekana Polepole akawa sahihi na Gwajima akawa sahihi Ila Kama walipata nafasi ya kubadilisha mambo na kukaa na mkuu wa nchi

Sifikirii Kama walishindwa kumshawishi kuwatendea Fair Chadema mwaka 2020.

Tangu 1992 tulikuwa na partial democracy Ila mwaka 2020 tumeizika democracy kwa 100%

Na mratibu mkuu alikuwa polepole na Bashiru.

Kwahiyo Mimi ningependa watu Kama Lissu na wafuasi wao wasimpe nafasi kubwa Sana polepole Ila wamsikilize tu.
 
Changamoto ya hii Nchi kujua yupi ni Kiongozi halisi, yupi anatumika imekuwa vigumu

Maana kuna watu walishapambana zamani kuweka mifumo inayowatii

Ngoja tuone miaka 15 ijayo Mungu akitupa uhai, huenda hivi anavyovipanda Lissu vikaota
 
Yes -Lissu yupo sahihi Ila akomae na ajenda moja over period of time .

Tunaweza tusifanikiwe Leo Ila tukafanikiwa baadae ikiwa watakaofaidika sio sisi hata wajukuu n.k
 
Kabisa, tumwombee jamaa asichoke

Maana Kwa upuuzi wa Siasa zetu za Simba na Yanga pamoja na kuletewa connection watu wakidinyana sioni tukipambania Nchi yetu
 
Hakika mkuu na huo mchezo wa Kanyama hauna mwenyewe kila mtu anataka aone mdinyano mpya .

Ndo maana siasa zetu zinahitaji Sana moyo ukiingia mtaani watu wapo busy na mambo tofauti na siasa .

Zile siasa za 2015 kurudi 2010 chini ya Dr Slaa kwa sasa zimekufa .
 
Back
Top Bottom