Rasmi Putin aonesha sample za noti mpya za BRICS. Je, huu ndio mwisho wa US Dollar?

Rasmi Putin aonesha sample za noti mpya za BRICS. Je, huu ndio mwisho wa US Dollar?

Tunahamia Cryptocurrency, unaleta mambo ya noti
Hapo sasa jdo utajua counter kutoka kwa wenye akili...mtoa mada anasema kuwa USA amenyanyasq watu na Dollar yake, sasa watu wanaleta njia ileile ya manyanyaso alafu tunashangilia...bado upatikanaji wa hiyo sarafu ikawa shida kama US Dollar vilevile.
USA akileta digital currency itakuba balaa tena.
 
Zikishaa kuwa mbili kila mtu atachagua aende wapi
 
Rais wa Urusi, Vladimir Putin, wakati yupo kwenye mkutano mkuu wa BRICS uliofanyika Kazan aliwashangaza washiriki kwa kugawa sampuli za noti mpya za Benki ya BRICS, ishara inayodaiwa kuwa mwisho wa enzi kwa Dola ya Marekani kama sarafu ya akiba duniani.

Noti hizo za BRICS, ambazo zimeonekana kwa mara ya kwanza katika hafla hiyo ya kimataifa, zimeibua mjadala mkubwa kuhusu mustakabali wa mfumo wa fedha wa dunia.

Sarafu hiyo mpya inasemekana kuungwa mkono na bidhaa halisi kama dhahabu na mafuta, tofauti na Dola ya Marekani ambayo ni sarafu ya "fiat" isiyo na dhamana ya moja kwa moja ya mali.

Sarafu ya BRICS Kuipiku Dola ya Marekani?

Wachambuzi wanaeleza kuwa uzinduzi wa sarafu ya BRICS huenda ukawa mwanzo wa kipindi kipya cha kutoitegemea Dola ya Marekani katika biashara za kimataifa.

Wanaonya kuwa sarafu hiyo mpya inaweza kupunguza sana ushawishi wa kiuchumi wa Marekani ulimwenguni, hasa kutokana na ukweli kwamba nchi nyingi zinaweza kuacha kutumia Dola kama sarafu ya kibiashara.

Sio mwisho wa dollar lakini ni njia mbadala na rahisi na imara ya kuhamisha pesa kutoka nchi moja hadi nyingine pasipo haja kupitia mfumo wa SWIFT na kutumia dollar.
Itapunguza gharama za kuhamisha pesa, kuondoa udhalilishaji wa vikwazo vya nchi za magharini.
 
Safi sana, lakini safari bado ndefu Kwa maana ndo kwanza imetambulishwa,mpaka kuingia kwenye matumizi inahitajika muda na juhudi za kutosha sana, na ni mapema mno kusema kwamba huu ndo mwisho wa us dollar.
 
Kwa hali ilivyo utaona jinsi nchi zitakavyo miminika hapo kujiiunga na hiyo block kuonyesha kuwa watu wamechoka na ukiritimba wa dollar
Yani niache kuchukua Dollar nichukue takataka.
Sasa hivi ndo unaoona takataka nakumabia kuna siku itaiona dhahabu
 
Yani niache kuchukua Dollar nichukue takataka.
Wewe ni mtu masikini kabisa hapa duniani,tena unatokea kwenye bara masikini kabisa,Tena unatokea kwenye nchi masikini kabisa na ninaamini unatokea kwenye mkoa masikini kabisa na inawezekana ukezaliwa kwenye familia masikini kabisa.
Wewe binafsi usipochukua Pesa yao hao BRICS wala hauna madhara yoyote kwao,ni kua haupo kabisa katika Dunia hii.
Huna lolote la kuwapunguzia.
Lakini kaa nikuambie USA wenyewe matumbo moto.
 
Ukiwa mbumbumbu wa uchumi, unaweza kuamini kuwa hiyo sarafu itaidhoofisha dola kiurahisi, lakini kama una uelewa japo wa kawaida wa uchumi wa Dunia, utajua kuwa hakuna lolote la pekee:

West Afrca block wana curreny yao, je, hiyo imepunguza uthamani wa dola katika mataifa hayo?
European Union wana sarafu yao, je, imeifanya dollar kutokuwa na thamani?

Kinacholinda uthamani wa dola ni ukubwa wa uchumi wa marekani. Huko Brics, jumlisha uchumi wa mataifa yote wanachama, uchumi wake bado ni chini ya uchumi wa Marekani ikiwa pekee yake:

USA GDP 2024 $29 trillion
BRICS
China GDP 2024 $13trillion
Russia GDP 2024 $2trillion
Brazil GDP 2024 $2 trillion
India GDP 2024 $ 4 trillion
Wakati USA pekee yake in GDP 29 trillion, nchi zote za Brics ukiziweka pamoja, jumla ya GDP yao haifiki hata $25 trillion!!
 
That is wishcasting!

The US is still king.

If the Euro couldn’t do it [with a much higher combined GDP and advanced economies of its members], then, whatever that BRICS currency is, ain’t got no chance against the $US.

💵 is and will be king for a long time.
 
Ukiwa mbumbumbu wa uchumi, unaweza kuamini kuwa hiyo sarafu itaidhoofisha dola kiurahisi, lakini kama una uelewa japo wa kawaida wa uchumi wa Dunia, utajua kuwa hakuna lolote la pekee:

West Afrca block wana curreny yao, je, hiyo imepunguza uthamani wa dola katika mataifa hayo?
European Union wana sarafu yao, je, imeifanya dollar kutokuwa na thamani?

Kinacholinda uthamani wa dola ni ukubwa wa uchumi wa marekani. Huko Brics, jumlisha uchumi wa mataifa yote wanachama, uchumi wake bado ni chini ya uchumi wa Marekani ikiwa pekee yake:

USA GDP 2024 $29 trillion
BRICS
China GDP 2024 $13trillion
Russia GDP 2024 $2trillion
Brazil GDP 2024 $2 trillion
India GDP 2024 $ 4 trillion
Wakati USA pekee yake in GDP 29 trillion, nchi zote za Brics ukiziweka pamoja, jumla ya GDP yao haifiki hata $25 trillion!!
💯%.

Kama Euro imeshindwa, hiyo currency ya developing [not developed] countries ndo itaweza?

Abadan asilani!
 
Back
Top Bottom