Rasmi Putin aonesha sample za noti mpya za BRICS. Je, huu ndio mwisho wa US Dollar?

Rasmi Putin aonesha sample za noti mpya za BRICS. Je, huu ndio mwisho wa US Dollar?

Shida miongoni mwao kuna wanafiki, USA akianza crackdown watakaa pembeni na kumuacha Russia peke yake.
 
Sio kweli sarafu ya BRICS countries ni note bali iliyokua proposed ni digital currecy ambayo 1=1 na chinese yuan. Afu hio picha ya putin kashika note ni edit. Hiyo note ilikua proposed na professor wa kirusi. Lakini BRICS countries wakasema wanakwenda digital(hata nchi za kiarabu ziko kwenye mpango wa kutengeneza digital system za malipo ya mafuta ambazo zinaweza kusomana na za china na brics digital currency n.k)
 
China haitegemei USA na Iran ndio kabisa haitegemei USA.
Japo sijajua kama ameingia bricks rasmi huyu Iran.
Wewe unaota? Unajua ni nani amewekeza kwa kiasi kikibwa China? Unajua soko kubwa laChina katika thamani liko wapi? Unajua ni kwa nini serikali ya China ndiyo inayoongoza katika kununua treasury bills za Serikali ya Marekani?
 
Hata kuishusha thamani US Dollar ni muhimu sana mkuu.Marekani wameionea sana dunia kwa kutumia dola yao mkuu,na hiyo haikubaliki kabisa.
We unaona hilo likiwezekana?
 
Wewe unaota? Unajua ni nani amewekeza kwa kiasi kikibwa China? Unajua soko kubwa laChina katika thamani liko wapi? Unajua ni kwa nini serikali ya China ndiyo inayoongoza katika kununua treasury bills za Serikali ya Marekani?
Mkuu ungefuguka basi,you seem to know something, but you are keeping it to yourself.Waekimishe watu,most people are ignorant of the Chinese Mushroom Economy.
 
Currency ndio kwanza inakua introduced hata kufanya kazi bado unaanza kuleta ushindani.
Wabongo bana fikra zao!
Una teseka ukiwa wapi !?


Ina maana wewe unajua Sana kuliko Putin na washirika wake !?

Hata kuunda sindano Tu hauwezi halafu unataka uwakosoe watu wanao ipasua kichwa USA na washirika wake

Ila wabongo 🚮🚮🚮😁😁😁😁
 
Kwa hatua BRICS waliyofikia,the US Dollar is no more,labda wa-initiate vita kubwa ya Dunia to destroy the World Economy.Mkuu ikiwa hata renowned World Economists wanakubali hili who are we to say no.

Halafuu, kumbuka the power of the US Dollar is based on it being a World Currency.Kama that is not the case anymore and countries are trading in the BRICS currency,it is only natural that the US Dollar value will crumble.Afterall nani atataka kutumia a Fiat Currency kama a currency pegged to a commodity is available,atakuwa lunatic.
 
Ndugu zangu wabongo tusitazame mambo ya kifedha kwa macho ya kisiasa. Hivi Waafrika hatukomii tuu kuforce siasa kwenye mambo ya fedha. Mifano ipo mingi na raia wengii wamelia kwa maono mafupi ya viongozi wao.

Jinsi mfanyabiashara anatazama fedha ni jambo la kujua kama wataka kufahamu pesa. Kwanza, pesa inabidi iwe stable, isiyoyumba yumba kupanda na kushukaa. Na ili pesa iwe stable inatokana na uimara wa nchii, hasa hasa taasisi za nchi. Tukumbuke viongozi wanakufa ila Taasisi hazifii, sasa ndugu zangu chukulia mfano huu; tuseme una million 100 za brick mara baada ya mwaka Putin kafariki anakuja kiongozi mpya wa urusi anasema russia inaacha kutumia io pesa kwa kuwa Russia ana taasisi zisizo na nguvu hilo jambo linapita bila kupingwa. Ivi hayo makaratasi utabadilishana na nani?
 
Viongozi wa Afrika wapowapo tu hawanainitiatives zozote. Hawajui kuwa dunia inaenda kubadilika kabisa. Waache ichawa wa Marekani, China, Urusi nk. Waunde umoja wao wa kiuchumi vinginevyo sisi Afrika tutakuwa wasindikizaji.
 
Wewe unaota? Unajua ni nani amewekeza kwa kiasi kikibwa China? Unajua soko kubwa laChina katika thamani liko wapi? Unajua ni kwa nini serikali ya China ndiyo inayoongoza katika kununua treasury bills za Serikali ya Marekani?
Hehehehe!
Najua kama kawaida yako kuvamia mada usizokua na ujuzi nazo.
Westerners ikiwemo USA wamewekeza sana tu China.
Ila thamani ya walichowekeza hakifikii thamani ya makampuni ya ndani na ya serikali ya China.
China imeshaweka replacement ya huo uwekezaji wa wageni hapo China.
Na hao wazungu wamewekeza hapo China kwanza kabisa kufuata soko,pili kufuata cheap skilled laboures.
Ila haimaanishi kuwa hao westerners ndio wanashikilia uchumi wa China.
Kama ingekua hivyo basi ile trade war na USA Trump angeshashinda ila akashindwa mbele ya China.
Usisahau kuwa hao wazungu kuna raw materials kama rare earth metals,chuma n.k wanafuata China kwa bei rafiki zaidi.
Ondoa APPLE/IPHONE wachina washaweka mbadala wa OPPO,XIAOMI,VIVO,HUAWEI.
Ondoa makampuni mengine China imeshaweka mbadala,hadi makampuni ya uundaji magari.
Ni sehemu gani unadhani USA anaweza kumshikilia China!?
Jibu HAKUNA.

Kuhusu treasury bill sijui kwanini China ananunua sana USA.
Maana hata dollar reserve China anayo kubwa kuliko hata USA yenyewe.
Tujiulize pia kwa nini!??
 
Una teseka ukiwa wapi !?


Ina maana wewe unajua Sana kuliko Putin na washirika wake !?

Hata kuunda sindano Tu hauwezi halafu unataka uwakosoe watu wanao ipasua kichwa USA na washirika wake

Ila wabongo 🚮🚮🚮😁😁😁😁
Broo umeelewa kwanini nimemjibu hivyo jamaa!??
Jamaa aliuliza kati ya dollar na hela ya Brics ukiambiwa uchague utachukua ipi!?
Ndio nikamjibu Brics bado haijaanza kufanya kazi UNASHINDANISHAJE NA DOLLAR!?
Maana yangu atulie sarafu ya Brics ianze kufanya kazi halafu baadae ndio aulize hilo swali.
Maana ni sawa uanze kushindanisha silaha ambayo China ndio kwanza ametoka kuiunda kiwandani labda na ATACMS ya USA,ilhali ya China bado haijawa operational kama ya USA.
 
Tukio linaloendelea hivi Sasa Kazan Urusi ni kubwa mno hapa duniani.
Lakini huwezi ona vyombo vya Magharibi vikilitangaza kwa uzito wake.
Lakini yote kwa yote Putin kapindua meza.
Walimwekea vikwazo vyote hapa duniani ili adhoofike,walimfanyia Kila huka za kumfanya aonekane ametengwa lakini mwamba katoboa.
West inawauma sana hii,hata Mimi ingeniuma.
 
Euro yenyewe ilishindwa kufanya hayo maajabu
 
Rais wa Urusi, Vladimir Putin, wakati yupo kwenye mkutano mkuu wa BRICS uliofanyika Kazan aliwashangaza washiriki kwa kugawa sampuli za noti mpya za Benki ya BRICS, ishara inayodaiwa kuwa mwisho wa enzi kwa Dola ya Marekani kama sarafu ya akiba duniani.

Noti hizo za BRICS, ambazo zimeonekana kwa mara ya kwanza katika hafla hiyo ya kimataifa, zimeibua mjadala mkubwa kuhusu mustakabali wa mfumo wa fedha wa dunia.

Sarafu hiyo mpya inasemekana kuungwa mkono na bidhaa halisi kama dhahabu na mafuta, tofauti na Dola ya Marekani ambayo ni sarafu ya "fiat" isiyo na dhamana ya moja kwa moja ya mali.



Sarafu ya BRICS Kuipiku Dola ya Marekani?

Wachambuzi wanaeleza kuwa uzinduzi wa sarafu ya BRICS huenda ukawa mwanzo wa kipindi kipya cha kutoitegemea Dola ya Marekani katika biashara za kimataifa.


Wanaonya kuwa sarafu hiyo mpya inaweza kupunguza sana ushawishi wa kiuchumi wa Marekani ulimwenguni, hasa kutokana na ukweli kwamba nchi nyingi zinaweza kuacha kutumia Dola kama sarafu ya kibiashara.

 
Back
Top Bottom