Wandugu mkae mkijua usd inaenda kuanguka na kupoteza umaarufu katika soko la Dunia.
Nitaeleza Kwa lugha nyepesi ili watu wasio wachumi wenzangu mnielewe.
Pesa kubwa duniani.
Kabla ya Euro kulikua Kuna Paund na USD.
Euro ilianzishwa baadae sana mwishoni mwa miaka ya 90.
Kwa Sasa kwa umaarufu Euro imeifunika Paund ya Uingereza.
Kwa Nini USD inaenda kupoteza nguvu umaarufu na kuanguka baada ya ujio wa fedha ya BRICS?
Haihitaji kua na elimu ya uchumi kuelewa hili.
Iko hivi.
Hakuna asiejua kua, USD ndio fedha pekee inayotumiwa na watu wengi zaidi ama nchi nyingi zaidi hapa duniani kwa ajili ya kubadilishana kati ya fedha na bidhaa.
Sasa iwapo itapatikana fedha nyingine ambayo imeundwa kutoka kwenye nchi zenye idadi kubwa sana ya watu hapa duniani,mfano china ,India, Brazil,Urusi na nchi nyingine.
Na Kuna nchi nyingi zimeonesha kiu ya kujiunga,
Kwa maana hiyo nchi zote hizo zitaachana na matumizi ya USD katika kufanya biashara baina Yao,yaani baina ya nchi wanachama wa BRICS .
Kwa Hali hiyo,dola itakua imepoteza umaarufu na nguvu.
Mfano,mtu akitaka kununua bidhaa kutoka nchi mwanachama wa BRICS,nchi muuzaji itamuambia alipe kwa fedha ya BRICS badala ya USD,
Hapa USD itakua imepeoteza umaarufu na nguvu.
Matumizi ya USD yataenda kupungua kwa sababu nchi nyingi sana zitaacha kuzitumia USD kama chombo Cha kubadilishana bidhaa.
Sasa kama nchi zitaachana na USD kwa Hali ya kawaida haiwezi kubaki na thamani ileile.
Kwa mfano Sasa hivi ukitaka kununua kitu chochote nje ya nchi,kama
vile kununua magari ama bidhaa nyingine kutoka Japan,china,India,Urusi,south Africa,Saudi Arabia,Iran,Dubai, Malaysia, Singapore, Korea kusini, Philippines, Taiwan, Israel,Canada n.k ni lazima ulipie kwa USD,.
Lakini BRICS currency ikija, nchi nyingi zitahamia kwa fedha ya BRICS,
Huo pia utakua ni mwanzo wa kupoteza umaarufuwa USD.
Kwa lugha rahisi kabisa kama fedha ilikua inatumiwa na nchi nyingi,nchi nyingine nyingi zikaamua kuachana nayo hakika thamani yake haiwezi kubaki kama ilivyokua mwanzo.
Hata hivyo kitakachotokea
Nadhani watu wengi hapa wanatakiwa watofautishe kati ya USD kushuka thamani na USD kupoteza umaarufu.
Kwa mtazamo wangu naamini USD haitashuka thamani,Bali itapoteza umaarufu.
USD itabaki na thamani yake,kwa sababu hata Marekani yenyewe itakua inauza bidhaa zake kwa USD,
ingawa nayo italazimika kununua bidhaa kutoka kwa BRICS members kwa kutumia fedha ya BRICS.
Wakati Sasa hivi ukienda kununua bidhaa Marekani utalipa kwa USD na Marekani ikija kununua bidhaa kwako italipa kwa USD .
Anguko lingine la USD ni haitatimika Tena kama fimbo kuzichapia nchi hasimu wa Marekani
Hapa nguvu ya USD itakua imekwisha kabisa.
Hali hii ndio iliikumba Pound ya Uingereza.
Kabla ya kuanzishwa kwa euro,pound ya Uingereza ilikua maarufu sana,lkn Sasa hivi imebaki na thamani yake lkn sio maarufu kama euro.
Mtazamo wangu.