stakehigh ili kujua kama kweli kuna Foreign Money Exchange Market fuatana na mimi na weka ujuaji pembeni , kubali kujifunza.
Kwanza soko ni nini?
Najua unajua maana ya soko ni sehemu watu wanaposanyika kuuza na kununua au mfumo unaowakutanisha watu kuuza na kununua , mpaka hapa najua unajua hivyo sitoenda kwa undani zaidi bali nitakuelezea ki mifano maana ya soko na umuhimu wake.
Chukulia huu mfano:
Mama Joy anaenda sokoni na kilo mbili za mchele kwa ajili ya kuziuza akiwa na malengo baada ya kupata kiasi cha pesa anunue maharagwe, lakini kabla ya kufika sokoni njiani anakutana na Mama Aisha ambae yeye amebeba Maharagwe kilo mbili pia kwa ajili ya kuuza ili anunue mchele , Mama Joy anamshauri Mama Aisha kwanini wasiende sokoni na wabadilishane bidhaa zao , wazo la Mama Joy ni zuri lakini Mama Aisha anakumbuka kipindi hicho ni cha uvunaji wa mpunga hivyo kiasi che mbele kilichopo sokoni kimeongezeka( supply imeongezeka ) na kuna uwezekano wa gharama ya mchele kushuka , lakini licha ya hivyo Mama Aisha hajui thamani halisi ya maharagwe yake kwa siku hio sokoni, hivyo anamkatalia Mama Joy wazo lake na kumwambia wafike kwanza sokoni ili wajue kilo moja ya Maharagwe inauzwa kiasi gani na ya Mchele kiasi gani , kishingo upande Mama Joy anakubali wanafika sokoni..
Wote kwa pamoja wanaulizia kilo ya mchele inauzwa kiasi gani wanaambiwa kutokana na wingi wa mchele sokoni kuliko wanunuzi(High supply), kilo ya mchele imeshuka kutoka 2000 mpaka 1000 , wanaulizia tena kilo ya Maharagwe inauzwa kiasi gani wanaambiwa kilo ya maharagwe kutokana na kuwa kidogo sokoni na wanunuzi kuwa wengi(High Demand)thamani yake imepanda kutoka 2000 thamani ya soko(Market price) wiki iliopita mpaka 4000 kwa siku hio(Real time market price).
Mama Aisha anachekelea wakati Mama Joy ananuna , lakini licha ya kununa kwake bado anahitaji maharagwe na pia licha ya Mama Aisha kuchekelea bado anahitaji mchele.
Wanarudi kwenye mazungumzo na Mama Aisha anamwambia Mama Joy yupo tayari kumpatia nusu ya Maharagwe yake achukue kilo mbili zake za mchele maana ndio thamani yake kulinganisha na maharagwe. Mama Joy anakubali kishingo upande.
Lakini kabla ya makubaliano yao kukamilika anatokea mtoza ushuru wa soko anawaambia makubaliano yao yatafanyika baada ya kulipia ushuru kama sheria ya soko, lakini kwakuwa hawana hela anawaambia atachota nusu kikombe cha mchele kutoka kwa Mama Joy na nusu kikombe cha maharagwe kutoka kwa Mama Aisha. Wote wanakubali na biashara inaishia hapo”
Unajifunza nini kupitia huo mfano:
Kwanza kabisa utagundua kwamba kabla hawajafika sokoni walikuwa wakijua thamani ya maharagwe ni sawa na thamani ya Mchele , lakini uelewa wa biashara wa Mama Aisha unamfanya kukataa, kwasababu anajua Sokoni ndio sehemu yenye mkusanyiko wa wanunuzi(Buyer) na Wauzaji(Seller) hivyo thamani ya bidhaa zao itategemeana na Demand na Supply ya siku hio na kudetermine price ya bidhaa zao.
Pili kwasababu Mama Joy hakutaka kupoteza muda wa kukaa chini na kuuza mchele akaamua kufanya Exchange ya kilo mbili za mchele wake na nusu ya mchele wa Mama Aisha.
Tatu kabla ya kufanya biashara yao ya mabadilishano akatokea mtoza ushuru(Kwa niaba ya Serikali) akapunguza kiasi cha Mama Joy anachopata na kiasi cha Mama Aisha anachopata..
Kwahio hapa jambo la msingi utagundua kwamba soko ni sehemu iliotumika kupima Demand and Supply ili kudetermine Price ya mchele na Maharagwe , bila soko Mama Joy na Mama Aisha wasingejua thamani ya bidhaa zao.
Lakini je hii ndio stori nzima ya kujua thamani ya kitu sokoni?.
Jibu ni HAPANA kwasababu licha ya kwamba mchele umeshuka thamani kutokana na kuwa kipindi cha mavuno lakini siku nyingine ya Soko Mama Joy anaweza kukuta mchele umepanda thamani kuliko wiki iliopira, anaulizia sababu anaambiwa, usafirishaji wa mchele kuja sokoni umekuwa mgumu kutokana na hali ya hewa , Serikali imepandisha bei ya mafuta na sababu nyingine ambazo ni nje ya soko.
Hapo bwana
stakehigh nimekuelezea ili uone umuhimu wa soko na ujue kwamba Soko ni kama mzani wa kujua Demand and Supply na kisha kurecommend price.
Sasa chukulia mama Joy ni mara yake kwanza kwenda sokoni na njiani hakukutana na Mama Aisha mwenye Maharagwe , kwasababu soko ni kubwa hajui wapi aende ili ampate Mama Aisha ampe Maharagwe , wakati akishangaa shangaa anakutana na Dalali(Broker), Mama Joy anamwambia Dalalali shida yake na dalali anamwelewa na anamwambia Mama Joy hali halisi ya thamani ya mchele kulinganisha na Maharagwe na Mama Joy anakubali lakini Dalali anamwambia kwamba Mtoza ushuru atakukata nusu kikombe cha mchele wako na pia na yeye atachota nusu kikombe ili kulipia muda wake na Mama Joy anakubali kupoteza kikombe kizima cha mchele kuliko kupoteza muda wa kuhangaika soko zima.
Dalali akifika kwa Mama Aisha anafanya hivyo hivyo atamwambia nimekuunganisha na mnunuzi hivyo nipe kiasi che hela au nichote nusu kikombe cha maharagwe , kumbuka muda huo Mama Aisha ashamlipa mtoza ushuru nusu kikombe hivyo kishingo upande anakubali dalali(Broker) achote nusu kikombe kwasababu ya ameunganishwa na mnunuzi. Hatimae biashara inafanyika wote wanapata faida na kujua mambo meingine
Kwa mantiki hio Broker(Dalalali) hamiliki soko bali ameamua kulitumia soko kujitengenezea faida , huyu Dalali (Broker) hafanyi hivyo kiholela yupo sokoni kutokana na kupata kibari kutoka kwa Mamlaka na kiasi anachokata kwa huduma yake ni kwa madili yote.
Ofcourse hapa utakutana na madalali ambao sio waaminifu na watatengeneza njia za kupata zaidi ya kile walichpangiwa kupata.
Sasa chukulia Broker(Dalali) anaamua kumrahisishia Mama Joy asije sokoni bali ametengeneza platiform ya kumfanya Mama Joy kuingia sokoni bila kwenda sokoni kimwili na kukata commision yake juu juu, chukulia tu kitu kama hicho ili uelewe tukiingia kwenye udalali wa soko la hela.
Sasa ukienda kwenye Real Estate Market utakutana na Dalali , ukienda kwenye Stock Market utakutana na Broker , ukienda kwenye Currency Market utakutana na Broker.
Kazi yake Broker ni kukuelezea uhalisia wa soko ulivyo na kisha kukuambia ni kiasi gani atakata kukuunganisha aidha na mnunuzi au muuzaji na dili likikamilika biashara inaisha hapo , yeye hamiliki soko wala hatengenezi soko , kazi yake ni kujipatia faida kutokana na Soko.
Sasa bwana stakehigh twende kwenye Forex Market je ni kweli kuna Forex Market?.
Jibu hapa ni NDIO , kuna Forex Market , kwanini kuna Forex Market chukulia huu mfano mwingine.
“Chukulia Juma amepata ofa ya kwenda Marekani , Ofa hio inajumuisha kuombewa Visa na gharama za nauli peke yake , vitu vingine kama maradhi na chakula atajitegemea, kwasababu Juma ndoto yake ni kwenda Marekani anavunja Kibubu na kugundua ana milioni mbili na laki tano za kitanzania . Kutokana na mahesabu yake anaona inamtosha kula bata la siku mbili Marekani na kugeuza, anaanza maandalizi ya safari lakini anagundua kwamba hawezi kutumia hela zake za kitanzania nchini Marekani kujipatia huduma hivyo anapanga kuzibadilisha ziwe Dollar ,kwasababu ni msomi anajua wapi atapata Dollar hivyo anaenda benki anaomba kupatiwa dollar , mtoa huduma anamwambia Dollar zimeisha, Juma hakati tamaa anaenda Duka la kubadilishia hela anaomba Dollar anaambiwa pia Dollar zimeisha na jibu lile linamkatisha tamaa kwasababu hizo ndio sehemu pekee ambazo alijua anaweza kupata Dollar, anajaribu kumbembeleza mtoa huduma ampatie Dollar maana anasafari lakini anamwambia Dollar zimeisha na hana , wakati akiwa amekata tamaa mtoa huduma anamwambia kuna Kuna Dalali(Broker) ambae ni wa kuaminika na anajua watu binafsi ambao wanauza Dollar kama vipi amuunganishe nao , Juma anafurahi na kukubali kuunganishwa na Broker, Baada ya kukutana na Broker Juma anaulizwa ana kiasi gani anataka kubadilisha anamwambia milioni mbili na laki tano , Broker anamuuliza tena unajua Dollar moja ni sawa na Tanzania shilingi ngapi , Juma anajibu Dola moja ni sawa na 2300TSH Dalali anamkatalia anamwambia dolla moja ni sawa na 2500TSH, Juma anaona kabisa hapa nataka kupigwa lakini Dalali anamwambia thamani ya Dollar zidi ya Tanzania shilingi imepanda angalia hili ni mfumo ambao unarekodi miamala yote ya mabadilishano ya Dollar na hela ya Kitanzania na hapa inaonyesha uhitaji wa Dollar ni mkubwa kuliko hela ya kibongo ndio maana thamani yake imetoka 2300TSH mpaka 2500 TSH, Broker anamwambia kama Haamini apige simu benki ulizia au kule dukani alikotokea , Juma anafanya hivyo na anapewa majibu hayo hayo na anakubali.
Broker anamuuliza tena Juma , unajua nakata shilingi ngapi kama nitakuunganisha na mtu anaeuza hizo Dolla, Juma anamuuliza unakata kiasi gani?, anaambiwa anakata(Transactions fee) Tsh 100 kwa kila Dolla moja hivyo atafanya mabadilishano ya Dollar moja kwa Shilingi 2600TSH , Juma yuko desparate maana ana safari hivyo anakukubali”
Sasa je katika hio Scenerio ni wapi Broker anamiliki soko?: jibu ni kwamba Broker hamiliki Soko bali yeye kazi yake ni kuomba benki au Financial Instutions kumuonyesha taarifa za Soko ili amuonyeshe mteja wake kukamilisha dili.
Kwanini aombe Benki au Financial institutions , jibu ni kwamba wale wafanyabiashara wakubwa au Investors(Big Players) wakitaka kufanya importations au exportations za bidhaa au wakitaka kufanya investiment kutoka nchi moja kwenda nyingine miamala hii hurahisishwa na benki na hizo taasisi nyingine za fedha, lakini hizi taasisi zimejiunganisha dunia nzima na kutengeza mfumo unaoitwa Forex Market kwa ajili ya kupima Demand na Supply ya hela husika na mwisho wa siku kuset exchange rates , sasa hapa kuna sababu za nje ya soko ambazo hufanya Demand kuwa kubwa kuliko supply au Demand kuwa ndogo kuliko Supply juu ya hela flani, sababu hizi ni kama vile Interest rates(Riba) , Inflations(Mfumuko wa bei), Uchumi, Export and import na mengineyo..
Kwa maana kwamba Juma hata kama taarifa zake za kubadilisha fedha zisirekodiwe hana impact kubwa sokoni kwasababu , wenye impact ni wale ambao wanahamisha kiasi kikubwa cha pesa kutoka nchi moja kwenda nyingine.
Mfano:
Chukulia una mabilioni kadhaa ya hela katika benki ya Kitanzania unataka kwenda kuzihifadhi Kenya kwasababu benki kuu ya Kenya wametangaza ongezeko la riba ambayo ni kubwa kuliko Tanzania, kitendo cha kuwasiliana na benki ya Tanzania na kuwaambia wahamishe hela zako kwenda Kenya maana yake ni kwamba benki itahitaji kuzibadilisha hela zako kwanza ziwe hela za kikenya ndio wazitume , huu muamala hufanyikia sokoni (interbank Market)na husimamiwa na mifumo ya kimalipo ya kimataifa kama SWIFT.
Sasa katika huu mfumo muamala ukifanikiwa matokeo yake upande wa Kenya Liquidity itaongezeka na upande wa Tanzania Liquidity itapungua.
Hii Liquidity itaonekana dunia nzima na ikitokea kuna investors wengine wako interested kuhifadhi hela zao Kenya Liquidity ya hela ya kikenya itaongezeka na kusababisha Exchange rates kubadilika.
Hivyo wewe mteja wa Rejareja utatumia exchange rates ambazo zinaamuliwa na Big players maana hawa ndio wanafanya Demand and supply ibadilike lakini wakati huo huo Central Bank ya Kenya imecheza nafasi kubwa hapo
Ameongeza interest rate kwa ajili ya kuimarisha sarafu yake , ameongeza interest rates kwa ajili ya kupunguza mfumuko wa bei , ameongeza interest rates kwa ajili ya kureduce Consumer spending na sababu zingine.
Tujiulize kama hakuna Forex Market nini kingetokea ?
Kwanza kabisa benki kuu za nchi zingejitengezea thamani ya hela yao wanavyotaka na hii ingepelekea biashara kuathirika mno au kutofanyika kabisa kwasababu biashara zitahangaika kuhedge zidi ya flactuations ya sarafu na kusababisha ugumu wa kufanya Cross -border Transactions na hii inapelekea hingh Volatiliy kwenye exchange rates na kupunguza liquidity kwenye Global Market.
Yapo mengi yatatokea kama kusingekuwa na soko la sarafu la Dunia ambalo huamua thamani
Kumalizia ndugu
stakehigh misconception yako ipo kwa Broker na mimi nakuambia Broker hana umiliki wa soko.
Foreign exchange(forex) market ni Decentralized , kitu pekee ambacho broker anaweza fanya ni kumanipulate soko lakini halimiliki , kazi ya Broker(Dalali) ni kuunganisha muuzaji na mnunuzi , kurahisishia watu kuingia sokoni kupitia platform kama vile MT4,MT5,Ninjatrader , cTrader, Tradingview, Saxobank(SaxotraderGO) na nyingine nyingi.
Hizi platform zinapata real time data kutoka kwenye soko la sarafu la dunia , ofcorse kuna Broker wameamua kutengeneza masoko yao wenyewe mfano halisi ni soko la synthetic Binary options , lile ni soko ambalo Broker katengeneza kwa kutumia Computer kwa kuigizia soko halisi lilivyo , usifananishe soko la sythetic Binary options na Real Forex Market.
Je Central bank zinatrade currency jibu ni ndio wana trade ila sio kwa ajili ya kutengeneza faida , wanachofanya ni foreign exchange intervations kwa ajili ya kuinfluence thamani ya sarafu yao , hizi intervations zinafanyika ni aidha kwa njia ya moja kwa moja kwa kutumia tools kama vile , Spot makert intervations , Forward market intervations , Currency pegging ,Currency swapping , Floats management, Reserve management N.k
Indirect intervations kwa njia za Monetary policy , Open market operations , Communication , QE na mbinu nyingine nyingi tu.
Je Commercial bank zinafanya trading?:
Jibu ni ndio wanafanya trading kwa ajili ya malengo tofauti tofauti ikiwemo kurahisisha miamala ya wateja wao kwa kuwa mtu kati baina ya muuzaji na mnunuzi , Benki ndio Market makers kwenye forex market kwa kununua hela ikiwa katika bidding price na kuuza kwa Ask price na kufaidika na Spread ya pair ya hizo hela, Wanafanya pia kitu kinaitwa Proprieatary trading hapa wanatengeneza akaunti na kutrade kwa malengo ya kupata faida, Wanafanya risk management pia kwa njia ya kuhedge risk , Ukitaka pia kufanya forex moja kwa moja na benki bila ya kumhusisha Broker inawezekana pia , bank nyingi za kibiashara zina huduma ya kutengenezea wateja wao Forex trading account na kuwafanya waingie sokoni kama kawaida.
Mjadala ilikuwa ni kukujibu je Forex market ipo na nimekujibu hivyo naishia hapa.