Pre GE2025 Rasmi sasa Rais Samia kaamua kuwa bora zaidi. Je, atamuunga mkono Mpina?

Pre GE2025 Rasmi sasa Rais Samia kaamua kuwa bora zaidi. Je, atamuunga mkono Mpina?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Bulelaa

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2024
Posts
1,342
Reaction score
3,247
Ni dhahiri sasa mama kaamua kufanya na kudhihirisha ubora wake, japo kuwa baadhi ya watendaji wake hawaendi kama anavyotaka yeye, na wao bila ya mijeredi na kushurutishwa, hawafanyi kazi kabisaa zaidi ya mapambio tu

Ukiachia mbali mapungufu machache kwake, Ndani ya sakafu ya moyo wa SSH, kuna matunda mazuri juu ya nchi yetu, shida ni waliomzunguka, na kwa bahati sasa amekwisha wafahamu vema, hawampi shida

Mh.Rais, apongezwe kwa kuwatema kina Nape na Makamba na sasa Makamu mwenyekiti wake kumruhusu ajihudhuru, ni jambo la kupongezwa sana

Makamu mwenyekiti wake bwana Kinana, ndiye mwalimu wa vijana hao amba Rais kawatema kwenye baraza lake, nasema Rais apongezwe kwa sababu, Kinana hakupaswa ajihudhuru nafasi yake mapema kiasi hiki baada tu ya vijana wake kutumbuliwa, alipaswa ajipe muda kwanza ili kujenga utulivu kidogo ndani ya chama, na kwa sababu hakufanya hivyo, hata yeye Kinana, kwa watu tuliosoma Cuba, tunapata jibu moja kwamba, ameomba kujiondoa kwenye nafasi hiyo ndani yake kukiwa na hway nyingi, kwa sababu vijana wake kuondolewa kwenye nyadhifa zao,

Na kwa tarifa tu ni kwamba, timu hiyo ya watu watatu, haijawahi kuaminiwa na watanzania hata chembe, maana wana makando kando mengi kiasi cha kutia kichefuchefu

Na kwa kuwza sasa Rais ameonyesha kutaka kufanya mambo kizalendo na kwa haki huku akiutanguliza Utabzanzania mbele, Tunamsihi sasa amuunge mkono na mh Mpina katika kutetea watanzani kwenye mambo ya ufisadi

Mungu ibariki TANZANIA
 
CCM umakamu mwenyekiti wanatakiwa kumpa Mpina , angalau anaweza leta ushawishi kidogo ndani ya chama ,
 
Usha ambiwa wasomali kwenye kilimo wako vziuri una ota ndoto za mchana
 
Back
Top Bottom