RASMI: Singida Big Stars tumeinasa saini ya Abdulmajid Mangalo kutoka Biashara United

RASMI: Singida Big Stars tumeinasa saini ya Abdulmajid Mangalo kutoka Biashara United

Tumefanikiwa kupanda daraja hivyo tutacheza Ligi Kuu kuanzia msimu wa 2022/23.
Halafu nimekuambia uwashauri mabosi wako kumpa mkataba yule mfungaji bora wa Mbeya Kwanza wakati inapanda ligi kuu, ukanipuuza. Ni mfupi hivi, halafu ana mwili! Jina lake nimelisahau.

Anakimbia kama digidigi! Ni bahati mbaya walimu walikuwa hawampangi tu mara kwa mara. Ila kila alipopata nafasi, impact yake ilionekana. Mkimpa mkataba, atawasaidia sana kwenye ushambuliaji.
 
Nakuelewa, kweli ni mchezaji mzuri na Ligi Kuu inahitaji wachezaji wa aina hiyo. Hata hivyo wapo wachezaji wazuri wengi na hatuwezi kusajili kila mtu. Ngoja tuone hadi mwisho kama jicho letu limemuona na yupo kwenye orodha yetu basi tutamtangaza tu.
 
Hongereni, halafu kazeni msije mkachovye ligi kuu na kurudi mlipotoka

Singida United sijui imejifia wapi

Malengo yetu ni kufanya vizuri na kusalia Ligi Kuu kwa muda mrefu. Hatuna mpango wa kushiriki bali kushindana. Tunaamini kupitia usajili makini tunaoufanya na maboresho kwenye benchi la ufundi tutafikia malengo.
 
Tunao uwezo wa kumsajili mchezaji yoyote aliye sokoni, mzawa au mgeni, kama tu benchi letu la ufundi litakuwa na uhitaji nae.
Sasa nyie mnalo benchi la ufundi? Yani ukasajili Boxer ndiyo umuache Kapombe unasema benchi la ufundi limependekeza?
 
Napenda uwasilishaji wako, niwatakie mafanikio naamini kwa kasi hii Singida Big Star itakuwa Moto, najua mtafanya maboresho kidogo kwenye dirisha Dogo
 
Back
Top Bottom