Rasmi: Yanga yavunja Mkataba na Gamondi

Rasmi: Yanga yavunja Mkataba na Gamondi

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
TAARIFA KWA UMMA

Uongozi wa Young Africans Sports Club unapenda kuutarifu umma kuwa umevunja mkataba na Kocha Mkuu wa kikosi cha kwanza, Angel Miguel Gamondi.

Vilevile, Uongozi wa Young Africans Sports Club, umesitisha mkataba wa kocha msaidizi wa kikosi cha kwanza, Moussa Ndaw.

Uongozi wa Young Africans Sports Club unapenda kuwashukuru Makocha hao kwa mchango wao ndani ya Klabu yetu na unawatakia kila la kheri katika majukumu yao mapya.

Tayari mchakato wa haraka wa kutafuta Makocha wapya wa kikosi chetu cha kwanza umeanza na unatarajiwa kukamilika hivi punde.​

Daima Mbele Nyuma Mwiko.

Imetolewa na
Ofisi ya Mtendaji Mkuu (CEO)
Young Africans Sports Club
15.11.2024

IMG_2038.jpeg


REKODI YA MAFANIKIO YA GAMONDI AKIWA YANGA

Kocha Gamondi alianza kukinoa kikosi cha Yanga katika msimu wa mwaka 2023/24 ambapo katika msimu huo aliweza kutetea ubingwa kwa msimu huo wa 2023/24

Aidha, ameweza kuchukua Ubingwa wa CRDB Federation Cup kwa msimu wa 2023/24 ambapo alimfunga Azam FC kwa mikwaju ya penati pale New Amani Complex Zanzibar

Ameifikisha Yanga katika hatua ya Makundi ya Klabu Bingwa Afrika mara mbili mfululizo. Mara ya kwanza msimu wa 2023/24 ambapo kwa miaka 25 Yanga ilikuwa haijawai kufika hatua hiyo na Gamondi aliifikisha baada ya kuiondoa Al Merreikh. Mwaka 2024/25 pia Gamondi ameiongoza Yanga kuingia hatua ya Makundi

Itakumbukwa kuwa kwa msimu wa 2023/24 Gamondi aliifikisha Yanga katika hatua ya Robo Fainali katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika ambapo aliondolewa kwa mikwaju ya penati na Mamelodi Sundowns

Aidha, kwa mwaka 2024 ameweza kuchukua Ubingwa wa Ngao ya Jamii kwa kuifunga Azam FC goli 4-1 ikiwa ni baada ya kuifunga Simba SC goli 1-0 katika hatua ya nusu fainali. Itakumbukwa pia msimu wa 2023 alifungwa kwenye fainali ya Ngao ya Jamii

REKODI ZA MICHEZO
Kwa ujumla Gamondi ameiongoza Yanga katika michezo 66 ambapo ameshinda michezo 53, amepoteza michezo 7 na kutoka Sare michezo 6.
  • Ligi Kuu NBC: Ameiongoza Yanga katika michezo 40; ameshinda 34, amepoteza 4 na kutoka sare 2
  • CRDB Federation Cup: Ameiongoza Yanga katika michezo 6; ameshinda michezo yote 6 bila sare wala kupoteza
  • Michezo ya CAF (Jumuisha hatua ya awali): Ameiongoza Yanga katika michezo 16; ameshinda michezo 10, amepoteza 2 na kutoka sare 4
  • Ngao ya Jamii: Ameiongoza Yanga katika michezo 4; ameshinda michezo 3, amepoteza 1 na hana sare
 
Nilikua namuona injinia kama mtu smart kumbe nae ni wale wale tu (wapumbavu)

Kundi la wapumbavu ni kubwa

Mechi mbili unafukuza kocha? Unataka usifungwe mechi yoyote wewe ni nani?

Kocha ana takwimu nzuri unamfukuza kwa ushabiki wa kijinga

Pumbavu
 
Nilikua namuona injinia kama mtu smart kumbe nae ni wale wale tu (wapumbavu)

Kundi la wapumbavu ni kubwa

Mechi mbili unafukuza kocha? Unataka usifungwe mechi yoyote wewe ni nani?

Kocha ana takwimu nzuri unamfukuza kwa ushabiki wa kijinga

Pumbavu
Mtu kapoteza mechi mbili wanafukuza kocha? Wenzetu wenye lig kubwa huko ulaya, kocha anaweza fungwa hata 10 matches but wapo naye?

I though hersi was smart than this
 
Back
Top Bottom