Rasmi: Yanga yavunja Mkataba na Gamondi

Rasmi: Yanga yavunja Mkataba na Gamondi

Nilikua namuona injinia kama mtu smart kumbe nae ni wale wale tu (wapumbavu)

Kundi la wapumbavu ni kubwa

Mechi mbili unafukuza kocha? Unataka usifungwe mechi yoyote wewe ni nani?

Kocha ana takwimu nzuri unamfukuza kwa ushabiki wa kijinga

Pumbavu
Ni kweli, Yanga imepoteza mechi mbili tu tangu kuanza kwa msimu huu, likiwa ni jambo linaloweza kuonesha kuwa timu haijafanya vibaya.

Hata hivyo, kwa klabu kubwa kama Yanga, mafanikio yake hayapimwi tu kwa kushinda mechi, bali kwa namna inavyoshinda hizo mechi.

Kwa daraja la Yanga, mafanikio yake hupimwa kwa aina ya mchezo wake unaooneshwa, na matokeo kwenye mechi kubwa inazocheza.

Uongozi unaweza kuwa haujaridhika na mfumo wa uchezaji ikiwa mchezo hauko katika viwango vya kuvutia au kuwa tishio kimataifa.

Huenda haukuridhishwa na mfumo wa uchezaji wa Gamondi, matumizi ya wachezaji na mbinu, hata kama timu haijapoteza mechi nyingi.

Migogoro ya ndani kati ya benchi la ufundi, wachezaji, au uongozi inaweza kuathiri uchezaji au maamuzi ya utawala. Hali kama hizi mara nyingi hazionekani hadharani.

Je, huu uamuzi huu ni mzuri au mbaya?
Ikiwa uongozi wa Yanga una mpango mzuri wa muda mfupi na mrefu, pamoja na kocha mwenye uwezo wa kuleta mafanikio zaidi, mabadiliko haya yanaweza kuwa ya manufaa.

Kubadilisha benchi la ufundi katikati ya msimu kunaweza kuathiri morali ya wachezaji na utulivu wa timu, hasa ikiwa kocha mpya hatapata muda wa kutosha kujenga mfumo wake.

Kwa ujumla, uamuzi wa kuvunja mkataba unapaswa kuwa na msingi thabiti, kwa sababu una athari kubwa kwa mwenendo wa timu.

Mashabiki na wadau watakuwa wakisubiri kuona kama hatua hii itazaa matunda au kuathiri vibaya utendaji wa Yanga katika michuano inayokuja.

Ova
 
Mengine yote ni visingizio tu lakini ukweli ni kwamba ni aibu kumfukuza kocha kwa kipigo cha paka mwizi kutoka kwa Tabora united.
 
Bantu Lady saizi atakuwa amejifunika zake ushungi mweusi analia tu, Poleni ndo safari kuelekea msibani imeanza mjiandae kugaragara kwa vilio.
Wamefanya haraka sana, Gamondi alikuwa bado ni kocha mzuri. Kupoteza mechi mbili mfululizo, si sababu ya kumuondoa. Wao wanaelewa kinachoendelea, wangekaa naye na wachezaji.

Mimi bado chaguo langu kwasasa ni Gamondi. Wanakoenda watajua wenyewe. Tukibamizwa tena na tena, akili itawakaa sawa, watapunguza hii mihemko.
Ila wewe kweli Malaika wa Misukosuko 🤣🤣🤣🤣🤣🤣 eti nalia. Wabadilishe benchi la ufundi, si kocha, walio jikoni watanieewa.
 
Nilikua namuona injinia kama mtu smart kumbe nae ni wale wale tu (wapumbavu)

Kundi la wapumbavu ni kubwa

Mechi mbili unafukuza kocha? Unataka usifungwe mechi yoyote wewe ni nani?

Kocha ana takwimu nzuri unamfukuza kwa ushabiki wa kijinga

Pumbavu
Swala la Gamond na Yanga ni suala la kisiasa zaid, vilabu vya simba na Yanga vina impact kubwa sana kwenye siasa za nchi yetu, ukijaribu kuangalia kwa wiki kadhaa zilizopita habari na hoja kubwa zilikua ni kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa..
Na Jinsi serikali na Ccm walivoboronga kwenye hilo zoez na kupelekea wapinzani wengi kuenguliwa, upepo kwa ccm na serikali kiujumla ulikua mbaya, so kilicho fanyika kwa yanga ni maagizo kutoka juu timueni Gamondi ili kuzima mijadala yote kuhusu kasoro za uchaguzi wa Serikali za mitaa..
Na wanasiasa wa nchi hii walishajua Simba na Yanga huleta mijadala kuanzia vijiweni hadi media zote za habari. Karata muhimu ccm waliyo ona waitumie kuhamisha upepo ni viongozi wa Yanga walipokea maelekezo.. Kwa watu makini kama kina Eng Hersi isingekua rahisi kumfukuza Gamond kisa kafungwa match 2 tu na ukiangalia bado siku chache kabla ya ligi ya mabingwa kuanza kuchezwa..
Habari yote tangu jana nchini ni kutimuliwa gamond media zote na vijiwe mwendokasi hadi daladala habar inayo trend ni Gamond..
Habar za kasoro za uchaguz zimesha sahaulika watu wamedandia kwenye kutimuliwa Gamond..
 
Hapa umejibu kama nani? Kiongozi wa Yanga? Unahusika na mapato ya Yanga?

If not, shut the fu*k up!
Nimejibu kama mjukuu wa mangoma, unataka ujione unajua sana na unaweledi zaidi kuliko hao wanaosimamia taasisi ya Young Africans??? Tulizana dada huu mchezo hauhitaji shentepeee

Hallelujah!!!
 
Screenshot_20241118_114317_Instagram.jpg
 
Back
Top Bottom