Ratiba inaendelea: Waraka wa TEC unasomwa leo kwa mara ya tatu

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Unaweza kujiuliza kwanini TEC wakachagua kuusoma waraka wa kupinga kugawa bandari za Tanganyika kwa DPW kwa wiki sita na si pungufu ama zaidi?

Hili limekaa kiroho na kihesabu zaidi.. Dunia inaendeshwa na tarakimu na hesabu kupitia kanuni maarufu ya MAGAZIJUTO (BODIMUS)!

Mara sita inawakilisha siku sita za uumbaji, yaani siku sita za wiki.. Jumatatu mpaka Jumamosi! Kwahiyo ilipaswa waraka usomwe kila siku kwa siku sita mfululizo, lakini wanaosomewa ni waumini na waamini kanisani na siku pekee ya kuweza kuwasomea katika wingi wao ni siku ya ibada ambayo ni Jumapili

Kwahiyo ndio maana zikatengwa Jumapili sita mfululizo za kusomewa waraka husika, na leo hii ni Jumapili ya tatu

Waraka mpaka sasa umeonesha mafanikio makubwa sana! Dondoo zilizoandaliwa kisomi na kwa weledi mkubwa hazikutoka nje ya mstari wa katiba ya taifa

Zimejitokeza taasisi, vikundi na watu binafsi waliojaribu kuukosoa na kuupinga waraka lakini wakashindwa vibaya sana, kwakuwa badala ya kukosoa ama kupinga kilichomo kwenye waraka husika, wao wakaishia kutoa shutuma, kutuhumu na kukejeli watu binafsi, taasisi iliyoandaa waraka, imani ya waandaaji nk

Hawa wote walikuwa na haki kamili ya kufanya hivyo kwa mujibu wa katiba yetu, kakini kuna kila dalili kwamba hawakusukumwa na uzalendo na dhamira njema bali kwa maelekezo maalum na kwa malipo! Mbaya zaidi wakakurupuka sana na kuongea ujinga mtupu kisha haoo wakasepa zao kukinga mikono!

TEC hawakutetereka kwenye hilo na wala hawakuthubutu kunyanyua mdomo kujibizana nao! Walibaki na focus yao kukamilisha ratiba.. Na wanatambua wazi kwamba debe tupu haliishi kutika..!

Waraka wenye manufaa kwa watanganyika wote bila kujali
Itikadi zao
Imani zao
Makabila yao
Kipato chao nk nk unaendelea kusomwa leo kwa mara ya tatu, na ili kukamilisha ratiba bado mara zingine tatu. Wanaotumwa kuujibu kwa malipo wajitahidi kuujibu kwa hoja na si vioja

Watanganyika sio wapumbavu! Tunajitambua!!!!
014ab9329eb5b0ecf142dcdf7b743548.jpg
 
TEC hawakutetereka kwenye hilo na wala hawakuthubutu kunyanyua mdomo kujibizana nao! Walibaki na focus yao kukamilisha ratiba.. Na wanatambua wazi kwamba debe tupu haliishi kutika..!
Pengine nina uwezo mdogo sana wa kufikiri (sio kosa langu kwani elimu ni ndogo sana) lakini lazima niseme kuwa Sehemu hiyo inaonyesha ni kwa namna gani fasihi ni ngumu sana. Unaweza kujipanga weee kuachia kombora mara hamadi unakuta fasihi imebadilisha uelekeo wa kombora lako na kukurudia mwenyewe🤣🤣🤣
.......it fuckks you back just the same way it fuckks others!

● waraka unasomwa kwa mara ya ngapi vilee?!!! Hizo sio kelele?!! Uwafikie ujumbe huu huko?!!!

● Mama Samia Suluhu Hassan, The Mother of Modern Tanzania, amesema chochote mpaka sasa?!!! Atumie ujumbe huu kudescribe wapiga kelele?!! Hapana, hawezi kwani ye ni kiongozi na amestaarabika.

Mimi nasema usomwe hadi October 2030 atakapomaliza muda wake.
 
Lazima ujue TEC ni wasomi wa mambo ya dunia pia sio wengine wababaishaji wanakalia kujiita dokta na profesa wakati hata ukimuuliza logic ya muundo wa serikali hajui. Ndio maana wanajiamini sana maana wale jamaa hawana elimu ya dini tu. Kama katibu wao yule Kitima amesoma mambo ya constitutional lawa sasa utambabaisha nini. Ndio maana hata wanasiasa uchwara wanawaogopa.
 
Pengine nina uwezo mdogo sana wa kufikiri (sio kosa langu kwani elimu ni ndogo sana) lakini lazima niseme kuwa Sehemu hiyo inaonyesha ni kwa namna gani fasihi ni ngumu sana. Unaweza kujipanga weee kuachia kombora mara hamadi unakuta fasihi imebadilisha uelekeo wa kombora lako na kukurudia mwenyewe[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
.......it fuckks you back just the same way it fuckks others!

● waraka unasomwa kwa mara ya ngapi vilee?!!! Hizo sio kelele?!! Uwafikie ujumbe huu huko?!!!

● Mama Samia Suluhu Hassan, The Mother of Modern Tanzania, amesema chochote mpaka sasa?!!! Atumie ujumbe huu kudescribe wapiga kelele?!! Hapana, hawezi kwani ye ni kiongozi na amestaarabika.

Mimi nasema usomwe hadi October 2030 atakapomaliza muda wake.
Mama na wengine wote wanasikia sana..ndo sifa moja wapo ya kuwa kiongozi...na uongizi unatoka kwa Mungu..Mama mwenyewe alisema anasikia lkn hajibu..hakusema hafanyii kazi yasemwayo...ukiona wewe unaona ni sawa watu kusema na wewe hujali basi huna sifa ya uongozi...but kwa upande wa serikali wanasikia na wanafanyia kazi yenye ukweli hata kama hawasemi hadharani
 
Usomwe hadi Oktoba 2025

Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
 
Huo ni uongo mnaongeza chumvi ili kusambaza sumu kwa raia, wewe usijifanye una akili kuliko wa bunge wote Tanzania na wewe sio mtaalamu wa mikataba.
 
Back
Top Bottom