Msemaji Mkuu wa Serikali ameongea na Waandishi wa habari muda huu na kueleza kuhusu ratiba ya kuagwa kwa mwili wa hayati rais John Pombe Magufuli.
Mikoa ambayo ipo katika ratiba ya kuuaga mwili wa Hayati Rais Magufuli ni DSM, Dodoma, Mwanza na mazishi kufanyika Chato mkoani Geita.
Msemaji Mkuu wa Serikali Dr. Hassan Abbasi amebainisha hayo baada ya kikao kazi cha kupanga na kuratibu ratiba nzima ya kuagwa na mazishi ya hayati Rais John Pombe Magufuli. Kikao hicho kiliwahusisha mawaziri, manaibu mawaziri, makatibu wakuu na manaibu makatibu wakuu wa wizara.
Msemaji huyo wa Serikali amewataka wananchi wote kujitayarisha na kuendelea kutulia huku mipango yote ikiandaliwa.