Ratiba ya kuagwa mwili wa hayati Rais Magufuli; Mikoa minne kuuaga mwili, kuzikwa Chato

Ratiba ya kuagwa mwili wa hayati Rais Magufuli; Mikoa minne kuuaga mwili, kuzikwa Chato

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
24,941
Reaction score
28,869
Msemaji Mkuu wa Serikali ameongea na Waandishi wa habari muda huu na kueleza kuhusu ratiba ya kuagwa kwa mwili wa hayati rais John Pombe Magufuli.

Mikoa ambayo ipo katika ratiba ya kuuaga mwili wa Hayati Rais Magufuli ni DSM, Dodoma, Mwanza na mazishi kufanyika Chato mkoani Geita.

Msemaji Mkuu wa Serikali Dr. Hassan Abbasi amebainisha hayo baada ya kikao kazi cha kupanga na kuratibu ratiba nzima ya kuagwa na mazishi ya hayati Rais John Pombe Magufuli. Kikao hicho kiliwahusisha mawaziri, manaibu mawaziri, makatibu wakuu na manaibu makatibu wakuu wa wizara.

Msemaji huyo wa Serikali amewataka wananchi wote kujitayarisha na kuendelea kutulia huku mipango yote ikiandaliwa.
 
Huyu jamaa bado yuko ofisini? Anapaswa afukuzwe kazi mara moja.

Yaani siku zote mzee haonekani hadharani, kumbe mzee anaumwa mahututi, yeye kakaa kimya, sasa mzee amekufa ndio anakuja kutupa ratiba ya mazishi. Sasa ili iweje?

Maiti ina faida gani kwetu kuliko mtu mwwnye uhai?
 
Hivi si shughuli zote za kawaida za serikali zinaendelea kama kawaida?
 
Geita na Mwanza ni karibu karibu sana... Binafsi naona ingekuwa Mbeya, Dodoma Mwanza na Lindi... Geita isihesabike kwa vile ndo atakakozikwa
 
Isingetosha kuaga DSM na Chato tu? Au Dodoma na Chato tu? JPM hakupenda matumizi makubwa ya pesa za walalahoi. Hiki kinapendekezwa kufanyika sio "magufulification" kabisa
Pamoja na korona kuendelea kututandika,ni kama vile hatujifunzi chochote!

Badala ya kupunguza mikusanyiko ili kupunguza kiwango cha usambaaji wa kirusi ndio tunaongeza mikusanyiko.

Sisi ngozi nyeusi ni vichwa maji kwelikweli!
 
Back
Top Bottom