Ratiba ya Ligi Kuu-Bara izingatie ubora miundombinu ya viwanja vinavyotumika kuchezewa mechi usiku, vingi havina ubora

Ratiba ya Ligi Kuu-Bara izingatie ubora miundombinu ya viwanja vinavyotumika kuchezewa mechi usiku, vingi havina ubora

DogoWaNjombe

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
3,284
Reaction score
7,708
photo_2026-02-23_18-48-26.jpg
Nimefuatilia mechi kadhaa hasa msimu huu2025/26 na msimu uliopita wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara, kumekuwa na ongezeko la mechi zinazochezwa usiku ili kuruhusu urushaji wa moja kwa moja kupitia Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kushirikiana na wadhamini na watangazaji.

Lengo kuu, ni kukuza thamani ya ligi na kuongeza mapato, Hata hivyo, uamuzi huu umeibua hoja kuhusu ubora na hadhi ya baadhi ya viwanja vinavyotumika kuchezea mechi za usiku.

Viwanja kama Jamhuri Stadium (Dodoma)Majaliwa Stadium (Lindi) wa KMC Complex(Dar) Meja Jenerali Isamuhyo (Dar) na Uwanja wa Ruangwa bado vinakabiliwa na changamoto za miundombinu, hasa mifumo ya taa kutokidhi viwango vya kimataifa, ubora wa nyasi, vyumba vya kubadilishia nguo na mandhari ya jumla ya uwanja.

Hali hii huathiri sio tu ubora wa mchezo bali pia taswira ya ligi inapokuwa hewani. Wakati mwingine unaona wachezaji wanapata shida wakiwa uwanjani, lakini wanakuwa hawana namna maana ratiba inakuwa imeshapangwa ili kuendana na matakwa ya mdhamini.

Ni toe wito wangu kwa TFF kupitia Bodi ya Ligi kuweka mbele ubora wa miundombinu kabla ya kuamua ratiba za usiku kwa misingi ya kibiashara. Maboresho ya viwanja yataongeza usalama, kuvutia wawekezaji na kulinda heshima ya ligi yetu ndani na nje ya nchi.Uwekezaji unaofanyika uendane na ubora wa miundombinu ya viwanja.
 
Taa za uwanja wa dodoma na ule wa meja general isamhyo ni hovyo kabisa,atleast ruangwa kule nampongeza mtani wangu majaaliwa.
 
Back
Top Bottom