Ratiba za masomo kuongezewa muda wa masaa mawili kutakuwepo na malipo ya ziada kwa walimu?

Ratiba za masomo kuongezewa muda wa masaa mawili kutakuwepo na malipo ya ziada kwa walimu?

Masaa ya kufanya kazi kwa muajiriwa wa serikalini mwisho ni 8 yani kuanzia saa 2 hadi saa 10

Wao walipewa favour tu kua wakae masaa 6 sa naona wamejisahau wameamua kubadili favour waliyopewa kua sheria
 
Ndugu yangu. Nilianza kazi ya ualimu katika hizi shule za kata za serikali nikitokea shule ya private. Kama unavyojua shule za private ni nginja ngija. Mnaamka saa 12 asubuhi mnawasimamia watoto katika program mbali mbali hadi saa 4 usiku wanakwenda kulala. Mshahara ulikuwa mzuri mixa na viposho na tubahasha twa hapa na pale. Nilipo kuja serikali nikaendelea na ule moto. Waalim niliowakuta wakaniambia dogo uta sizi kama sio kufleti. Aisee sikuchukua hata miez 6, nikawa kama wao.

Hayo matamko yanaishia kwenye vyombo vya habari. Njoo huku kijijini uone waalim wanaenda shuleni saa 4 asubuhi, yaan ni shidaaa tena kuna siku hatuendi kabisa shuleni nashinda shamba nalima.
Siwezi kujila. Kama posho ipo napiga mzigo kama haipo saa 7 mchana nachora
Hahahaha we mwl. Mzoefu
 
Mimi sioni tatizo maana shule nyingi hasa za gvt watoto hutoka SAA nane na nusu wwkati muda wa kazi no SAA tisa na nusu,hivyo walimu tunaiibia serikali SAA limoja,sasa kufikia SAA 10 na nusu ni saa limoja tu limeongezeka

Changamoto iko kwa watoto hasa sisi tunaofundisha vijijini ,mtoto ataweza kukaa darasani kwa almost teni hours bila kula? Maana shule nyingi ni za kutwa

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
Mkuu huwa unanikumbusha novel ya Unanswered Cries iliyoandikwa na Osman Conteh
 
Kwa kukusaidia tu usipende kuanika plan zako kama umekusudia kufanya hivyo fanya kimya kimya usijekuingia matatani
Kaka nimekusoma. Ujue waalim tuna machungu mtu asikwambie. Ukifatilia mishahara yetu huwezi mruhusu mwanao asome ualimu. Mtu anafanya kazi bandarini mkoa wa dar anapewa housing allowance. Mm huku nakaa nyumba inavuja mpaka nastaafu siipati hiyo kitu. Ujue kuna mambo yameota mizizi hii awamu ya tano na watu wapo kimya kabisa
 
Kwa kutoka sa 10 hakuna tatizo.
Pia kuongezewa mshahara kwakweli haipo maana walimu walipata mishahara kwa kipind hawafanyi kazi yoyote. Wizara inachoangaika hapo ni kufidia muda ulopotea ili ratiba iende sawa.

NADHANI BORA MWALIMU UNGEHOJI HIVI, JE RATIBA YA HADI SA KUMI WANAFUNZI WATAWEZA? WAKATI SHULE NYINGI NIZA KUTWA NA WANAFUNZI HAWALI SHULENI?

Msije kuwa mnalazimisha wanafunzi wanabaki hadi sa 10 hali ya kuwa asubuh hata chai hakupata akiwahi shule alafu anatoka sa kumi na twajua wengi wakiondoka hawapewi hela yoyote ya kusema kuwasaidia hata mihogo, Hapa ndo tunatengeneza wanafunzi kuanza njia za kujitafutia ili kukidhi mahitaji yao ,hali ya kuwa njia za mwanafunzi kujitafutia hasa upande wa kike sio Salama.
Tuwe na watoto kwa malengo na kuweza kuwahudumia mahitaji muhimu
 
Mimi sioni tatizo maana shule nyingi hasa za gvt watoto hutoka SAA nane na nusu wwkati muda wa kazi no SAA tisa na nusu,hivyo walimu tunaiibia serikali SAA limoja,sasa kufikia SAA 10 na nusu ni saa limoja tu limeongezeka

Changamoto iko kwa watoto hasa sisi tunaofundisha vijijini ,mtoto ataweza kukaa darasani kwa almost teni hours bila kula? Maana shule nyingi ni za kutwa

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
Hiyo changamoto sio ya vijijini Tu hata mjini ipo sana.Muda wa jioni watoto wengi wanatoroka hawakai darasani.
 
Walipwe overtime ya nini, mbona wamelipwa miezi mitatu bila kufanya kazi, na mwezi wa tatu walifanya nusu mwezi wakalipwa full[emoji848]
Kuna mahali huelewi na au unafanya makusudi kwa choyo iliyokuwa nayo juu ya walimu! Mwalimu ni mwajiriwa wa kudumu na kwa mujibu wa Sheria za ajira anazo stahiki zake mama likizo za namna zote ambazo akienda mshahara wake hausimami! Hata wakati wa majanga walistahili kulipwa kwa mujibu wa mkataba huo wa kudumu wa ajira kwani wao hawakuamua kubaki majumbani Bali mwajiri wao!

Pia mwl ni mtumishi pekee anayefika ofisini saa 12:30asubuhi na kuondoka kuanzia saa 9:30 alasiri! Kimahesabu ni masaa 10 kwa siku badala ya masaa 8. Sasa ukiyaongeza masaa 2 ya waziri maana yake afanye kazi masaa 12 kwa siku Jambo ambalo ni kinyume Cha Sheria na kumkomoa huyu mwl.

Ndio maana nikamuuliza waziri mhusika pamoja na mwajiri ambaye ni serikali na chama Chao (cwt) watolee ufafanuzi wa jinsi ya kumwezesha huyu mwl anayefanyakazi kwa masaa 12 anafidiwaje muda wake wa ziada? Hayo ya watoto wataishije shuleni nawaachia wazazi wao wawasemee!
 
Kuna mahali huelewi na au unafanya makusudi kwa choyo iliyokuwa nayo juu ya walimu! Mwalimu ni mwajiriwa wa kudumu na kwa mujibu wa Sheria za ajira anazo stahiki zake mama likizo za namna zote ambazo akienda mshahara wake hausimami! Hata wakati wa majanga walistahili kulipwa kwa mujibu wa mkataba huo wa kudumu wa ajira kwani wao hawakuamua kubaki majumbani Bali mwajiri wao!..
Naona watu wengi wanaliongelea Sana hili la walimu kulipwa mshahara ilihali walikua hawaendi kazini.Chakujiuliza walipanga wenyewe wasiende kazini?Nawaonea huruma tu wanafunzi wakutwa kama watafanikiwa kukaa mpaka huo muda bila kula.
 
Jana ulikuwa Sikh ya mtoto wa Afrika.
Siku chache zijazo, na hata awali, watoto wanashinda njaa na kiu shuleni.
He utulivu na ushiriki wa watoto kwenye masomo umefikiriwa?
Punda afe mzigo wa bwana ufike.
Sidhani kama wamefikiria kabisa hili, mazingira ya shule nyingi siyo rafiki na hilo agizo.
 
Ujue ukitaka kufanya jaribio fanya kwa waalim . Wao ni wapokeaji sana. Nauliza. Kama mihula imebadilishwa kwa kuongeza siku za masomo ya nini kuongeza saa za kazi???
Ujue kuna wizara inakurupuka sana hii. Sema effects kuonekana sio muda mfupi. Yaan kuna kipindi zilikuja hadi combi za CBM, sijui BRN na mbwembwe zake ilifia wapii
 
Sawa mwalimu
Mimi ni mwalimu. Wakat watoto wapo nyumbani nilikuwa natoa kazi watoto wafanye na nasahihisha madaftar karibua elfu moja kwa wiki. Hilo lilikuwa agizo la katibu tawala wa mkoa niliopo.

Sasa hayo masaa mawili ya ziada yapo kisheria na posho inatakiwa iwepo. Vinginevyo naona kama wanapigia mbuzi gitaa. Sina mpango wa kukaa mpaka muda huo. Mm ikifika saa 7 mchana nachora nipo geto.
 
Waalimu wanaotoka kazini saa nane Wanamuibia muajiri,muda wa mtumishi kufanya kazi unaisha saa kumi.
Halafu hiyo ni kasunba ya baadhi ya mikoa,nimeishi Kilimanjaro na Kusoma huko,shule zote ratiba ni Mpaka saa kumi.
 
Waziri wa Elimu katia waraka na ratiba mpya za mihula ya shule jana.

Ndani ya waraka huo kaongeza muda wa masaa mawili kwenye RATIBA za shule yaani zianze SAA 2:00 asubuhi hadi SAA 10:00 jioni badala ya SAA 8:00 mchana.

Katika kuongeza huku hakuzungumzia malipo ya ZIADA (overtime) kwa walimu ambao no watekelezaji na wasimamizi wa RATIBA hiyo.

Nauliza je, amesahau kuwa muda wa kazi kwa mwajiriwa wa umma unaishia SAA 9:30 alasiri? Kama kaongeza muda wa kazi haoni kuwa Kuna haja ya kumlipa ZIADA huyu mwalimu kwani naye muda wake wa kazi hautofautiani na wafanyakazi wa kada nyinginezo?

CWT na hata serikali watoa majibu ya kama KUTAKUWEPO na malipo ya ziada na kinyume chake kutaleta mgogoro wa kikazi kati ya mwajiriwa na mwajiri.
Waalimu walipokuwa nyumbani walikuwa hawalipwi? Ifikie wakati tuwe tunasaidiana.

Sent from my LM-Q710(FGN) using JamiiForums mobile app
 
Mimi ni mwalimu. Wakat watoto wapo nyumbani nilikuwa natoa kazi watoto wafanye na nasahihisha madaftar karibua elfu moja kwa wiki. Hilo lilikuwa agizo la katibu tawala wa mkoa niliopo.

Sasa hayo masaa mawili ya ziada yapo kisheria na posho inatakiwa iwepo. Vinginevyo naona kama wanapigia mbuzi gitaa. Sina mpango wa kukaa mpaka muda huo. Mm ikifika saa 7 mchana nachora nipo geto.
Hebu kuweni na wito jamani!!

Unataka mpaka kufundisha watoto ushurutishwe na magufuli?

Tunajua pesa ni muhimu lakini kazi unayofanya ni muhimu zaidi kuliko hayo makaratasi!

Si ajabu elimu imekuwa ya hovyo kwa sababu watu wamekuwa watumwa wa hela mpaka wanasahau majukumu yao!

Wanasiasa wanafakamia fedha, serikali inafakamia fedha, mafisadi yanafakamia fedha, watumishi wanafakamia fedha.... majitu yote yamekuwa mafisi!

Hebu fanya kazi yako kwa upendo.
 
Waziri wa Elimu katia waraka na ratiba mpya za mihula ya shule jana.

Ndani ya waraka huo kaongeza muda wa masaa mawili kwenye RATIBA za shule yaani zianze SAA 2:00 asubuhi hadi SAA 10:00 jioni badala ya SAA 8:00 mchana.

Katika kuongeza huku hakuzungumzia malipo ya ZIADA (overtime) kwa walimu ambao no watekelezaji na wasimamizi wa RATIBA hiyo.

Nauliza je, amesahau kuwa muda wa kazi kwa mwajiriwa wa umma unaishia SAA 9:30 alasiri? Kama kaongeza muda wa kazi haoni kuwa Kuna haja ya kumlipa ZIADA huyu mwalimu kwani naye muda wake wa kazi hautofautiani na wafanyakazi wa kada nyinginezo?

CWT na hata serikali watoa majibu ya kama KUTAKUWEPO na malipo ya ziada na kinyume chake kutaleta mgogoro wa kikazi kati ya mwajiriwa na mwajiri.
...but wakati shule zimefungwa si wamelipwa mishahara kama kawaida? Kumbuka kada nyingine za ajira ziliendelea na kazi wakati walimu wakipumzika katika kipindi chote cha corona.

Mawazo yangu tu.....najaribu kuwa fair

But overtime zinategemea mkataba wa ajira...kama ipo, ipo tu.
 
Back
Top Bottom