Ray Asema Yeye Ndiyo Msanii Tajiri Kuliko Wote Hapa Bongo

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304
Star wa filamu nchini Vicent Kigosi "Ray" amesema kuwa yeye ana pesa na mali nyingi na hakuna msanii yeyote wa Tanzania awe wa filamu au muziki anayemfikia sema hapendi tu kujitangaza kama baadhi ya mastaa wenzake akidai ni ulimbukeni. "hakuna msanii anayenizidi uwezo kuanzia mali na hata fedha niko mbali sana mimi, hata gari ninalotembelea hakuna msanii aliyenalo kama ingekuwa ni mtu wa kujisifusifu na kutafuta sifa za kijinga jamii ingejua" alisema star huyo wa filamu za Oprah, Sobbing Sound, Hard Price na Handsome Wa Kijiji akizungumza na gazeti moja.

Ray vile vile aliamua kurusha kombora kwa wabaya wake wasiopenda maendeleo yake kwa kusema "wanaongea sana majungu, fitina na vitu ambavyo havipo kuhusu mimi, mimi ni jembe, kwanini wasiangalie maisha yao? leo msanii unateta nae dakika hiyo hiyo anageuza maneno hayo kuwa majungu, acha nikae peke yangu nifanye issue zangu"
 
Mhh movie pekee ndiyo imeleta fweza,au maana tumesikia mengi kumhusu,manake waarabu wananunua figo/kucha/kabang kwa pesa nyingi...
 
Tunaomba tu usije kuwa teja... Tutajua mali zako halisi
 
Aziweke mali zake hadharani tujiaminishe kama kweli na njia halali aliyotumia kuzipata. Mwenzake masanja aliweka mali zake wazi na kusema amezipataje kuondoa uvumu oooh muuza unga....

Sasa Ray majungu kwake mengi.. muuza unga ooh anagawa ile kitu kabang.. Ajisafishe basi....

Weka wazi hapa... Je kuuza sura tu ndo umekuwa tajiri?
 
Hivi kwenye ile nyumba ya mamaake alishahama?
 
Lakini hapana hawezi kumzidi Masanja.
Mwenzake kilimo kimemtoa sana.
 

Mwambie aache upuuzi na ushamba, na akue ki celebrity, wenye mijiela uwa hawajisifii. Feza tu zinaongea na watu wa pembeni wakiwapambanisha bila wao kuwajari.
 
Mimi nina kanuni moja; mtu akisema ana hela wakati hizo hela hazionekani zinafanya nini/zimefanya nini, huyo ni -------- wa kutupwa. Hela ya chumbani haiongezeki hata siku moja, mtu hata akiwa na milioni mia saba kama ameziweka, wewe mwenye lkaki tatu waweza mpita muda wowote.
 
Mambo mengine bora mtu ukae kimya tu utahesabiwa una busara otherwise ni kujiaibisha
 
Nijuavyo mimi MAPAPARAZI huwa hawasubiri kuambiwa chochote na celebrity..kama ana thamani hiyo (if he/she worth it) watajua tu....hawotosubiri uitishe press conference useme.......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…