Ray Asema Yeye Ndiyo Msanii Tajiri Kuliko Wote Hapa Bongo

Ray Asema Yeye Ndiyo Msanii Tajiri Kuliko Wote Hapa Bongo

Star wa filamu nchini Vicent Kigosi "Ray" amesema kuwa yeye ana pesa na mali nyingi na hakuna msanii yeyote wa Tanzania awe wa filamu au muziki anayemfikia sema hapendi tu kujitangaza kama baadhi ya mastaa wenzake akidai ni ulimbukeni. "hakuna msanii anayenizidi uwezo kuanzia mali na hata fedha niko mbali sana mimi, hata gari ninalotembelea hakuna msanii aliyenalo kama ingekuwa ni mtu wa kujisifusifu na kutafuta sifa za kijinga jamii ingejua" alisema star huyo wa filamu za Oprah, Sobbing Sound, Hard Price na Handsome Wa Kijiji akizungumza na gazeti moja.

Ray vile vile aliamua kurusha kombora kwa wabaya wake wasiopenda maendeleo yake kwa kusema "wanaongea sana majungu, fitina na vitu ambavyo havipo kuhusu mimi, mimi ni jembe, kwanini wasiangalie maisha yao? leo msanii unateta nae dakika hiyo hiyo anageuza maneno hayo kuwa majungu, acha nikae peke yangu nifanye issue zangu"

Mwenyenazo hasemi......
 
Uyu kijana nakumbuka enzi hizo anaanza anza ndio kijana niliyekua namfahamu kwao kukiwa na pesa kidogo ya kubadirishia mboga na chumvi...hivyo kama kweli wakati anatafuta za kwake na alikua makini basi atakua na pesa ya kutosha tu
 
Sawa, tuchukulie ray ni tajiri, je, kwa utajiri wake kaifanyia nini jamii?
Mengi, Bahresa, Abood na wengineo watasemaje?
 
Duuhh live arv zinatumika hapa na vp na zembwela mbona mnamtaja sana
 
Back
Top Bottom