Rayvanny atakiwa kuilipa Wasafi Milioni 50 baada ya kufanya shoo kwenye ndoa ya Bilnas

Rayvanny atakiwa kuilipa Wasafi Milioni 50 baada ya kufanya shoo kwenye ndoa ya Bilnas

Watu wanasahau maana ya mkataba, it is binding by the law, Rayvann nadhani anaelewa hili kabisa maana kakaa pale muda mrefu, mengine ni kumtafutia tu Diamond lawama zisizo na msingi.

Ukishaingia mkataba ni wajibu wako kuzisimamia, kuziheshimu na kuzifuata terms na standards zilizomo humo ndani
Ni kweli,ila hata Ile ya Karl peters na Mangungo wa msovero Ilikuwa mikataba!
Tatizo ni mikataba ya kinyonyaji!
 
Ingawa inaseamekana Rayvan ameikacha lebo ya Wasafi lakn kuna mambo walikuwa hawajamalizana kimkataba hivyo hakupaswa kufanya show au kihudhuria tamasha au msiba wowote maana Kila tukio tajwa hapo juu lazma liwe na baraka za wasafi kukiuka Jambo moja kat ya Hilo utapigwa faini kulingana na tukio

Hivyo bwana Rayvan kabla mkataba hajavunja rasmi yeye alienda kutumbuiza kwenye ndoa ya Bilnas na Nandy

Inasemekana kuvunja mkataba na WCB na Milioni 800 ukijumlisha na faini ya juzi jumla Milini 850

Hata bwana Harmonize inasemekana alilipa Milioni 5 baada ya kihudhuria msiba wa Ruge Mutahaba bila ruksa kutoka WCB

Source: Leo Tena - Clouds FM

UPDATES

Hatimaye kijana amemalizana rasmi na WCB sasa yupo huru Kama msanii anayejitegemea baada ya kulipa mil 850 Jana

Funzo kwa vijana mkataba n kitu Cha kukiheshimu kwan uliingia mwenyewe bila kushurutishwa

Hongera RAYVAN sasa ndio utaiona rangi halisi ya mziki wa Tanzania
Hongeea Rayvan
 
Ni kweli,ila hata Ile ya Karl peters na Mangungo wa msovero Ilikuwa mikataba!
Tatizo ni mikataba ya kinyonyaji!
Nadhani kinachowafelisha hawa wasanii mpaka tunakuja kuwalaumu mwishoni ni pale hii mikataba wanapopewa wanakuwa na njaa sana, ukijumlisha na ndoto za kuonekana kideoni, show za hapa na pale na mademu wakali wanasaini tu bila kuwa na mwanasheria baadae ndio inawafunga

Tukumbuke mkuu, “ignorance of the law is no excuse”
 
Back
Top Bottom