kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Sio vizuri kutimuana kila wakati kwakuwa zoezi la kutimua watu linazaa kelele na bughudha nyingi kwa wananchi. Tulifurahia kuona watanzania wenzetu wafanyabiashara ndogondogo wameziachia barabara za magari na njia za miguu za watanzania wenzao walizokuwa wamezivamia kwa maslahi yao binafsi.
Lakini sasa hivi inasikitisha kuona machinga hawa wanaanza kurudi tena polepole mmojammoja kimyakimya kwenye njia za miguu. Watu hawa wanatabia ya kuambukizana ugonjwa wa kupanga vitu chini kwenye njia za waenda kwa miguu. Yaani anaanza mtu mmoja kupanga chini viatu 3 kutesti mitambo na akiona hali ni shwari anaongeza pea 3 kesho. Na wengine wakiona mwenzao kapanga chini bila kelele na yeye analeta bidhaa yake, na mwingine, mwingine hadi njia zote zinazibwa.
Leo hii ukipita pale Buguruni utaona wale wauza nets na mapazia walianza polepole mmojammoja na sasa karibia hali anarudi upya kama awali.
Ni vizuri surveillance iwe ya kudumu ili kupunguza kurudia upya zoezi lilelile baada ya muda mfupi. Pia ni vema watu watafute maeneo halali sasa ya kuanyia biashara ili kuepuka kurupushani karibu na uchaguzi.