Sijapewa username bado
JF-Expert Member
- Aug 15, 2024
- 1,775
- 2,891
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Thobias Andengenye, ametoa wito kwa viongozi wa dini, vyombo vya habari na asasi za kiraia kushiriki kikamilifu katika kutoa elimu ya uraia juu ya umuhimu wa kupiga kura na kudumisha amani katika kipindi hiki cha uchaguzi.
Akizungumza katika harambee ya ujenzi wa Kanisa la Kipentekoste FPCT lililopo Majengo, Kigoma, ambapo alimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan, amewataka viongozi hao kutumia nafasi zao kuwahamasisha wananchi kushiriki kikamilifu kwenye zoezi la uchaguzi kwa njia ya amani na utulivu ili kudumisha mshikamano wa kitaifa.
Aidha, Mkuu wa Mkoa Andengenye amechangia kiasi cha shilingi milioni thelathini kama mchango wa Rais katika ujenzi wa kanisa hilo ambapo pamoja na mambo mengine amesisitiza uwepo wa mshikamano wa kidini na kijamii kama msingi wa maendeleo na amani ya taifa.