RC Antony Mtaka kumsema Waziri mbele watoto umekosea. Kama watoto wakimdharau, watamheshimu nani?

Hilo povu la nini mkuu!

Acha matusi na vitisho. Serikali hii haiwezi kushindwa kufika kwa sababu ya mtu mmoja! Hayo ni masihara kabisa.

Hoja ya msingi ni kuwa Mtaka amekosea sana kumshambulia waziri mwenye dhamana ya elimu hadharani . Waziri ndie msimamizi wa sera ya elimu na miongozo. Waziri alikuwa anatekeleza wajibu wake.

Kutokana na kadhia hii,bosi wao,raisi wa jamhuri ya muungano ya tanzania ataamua mwenyewe atakavyoishughulikia. Akiamua kutimua Mtaka. Mtaka na wewe hamna cha kumfanya.
 
Kwani ni wapi kwenye katiba utakiwi kupiga alichokisema waziri? Wewe ukiwa kiongozi?
 
Kumuwajibisha (kumuondoa ofisini) mtu kama Mtaka,kwa mtazamo wangu,ni jambo lisilokubalika duniani wala mbinguni.Huyu ni lulu,tujifunze kusikia ukweli mchungu.
 
Hata Antony Diallo nae alifanya hivi hivi. Unawatwanga wanafiki wa magufuli ngumi za uso za kutosha tu!

Halafu baadae unajitokeza kuomba radhi ya uongo na kweli, huku ujumbe ukiwafikia wahusika na sisi watazamaji kwa usikivu mkubwa.
 
Mamlaka aliyotumia sio yake, angekua mbunge sawa. Mbunge ndio mwenye haki ya kuzungumza hadharani kama hivyo na isingeonekana ni kosa.
Acha kupotosha mkuu.unajua majukumu ya mkuu wa mkoa wewe?

Ni mwakilishi wa mkuu wa nchi katika mkoa wake.mkoa ukifaurisha mkuu wa nchi anapata kura nyingi pia.mkuu wa mkoa anasimamia utekelezaji na maboresho ya huduma kwa watu.ndiyo maana hoja ile ya majimbo inaleta mashiko.Wale waliotutangulia watusaidie kidogo kuelewa zamani kulukuwaga na watu wanaitwa Ma Regional Development Director,sijui waliishiaga wapi wale.na majuku yao yalikuwa ni nini? lkn nahisi ndicho hicho anachofanya Mtaka.Namuona mtaka ni zaidi ya RC.

Sema pia nakubaliana na wewe angeweza pia kusema hoja zake bila kuendelea kusisitiza kwamba wasimsikilize waziri.angeweza kuongea kwenye vikao vyao vya ndani vya mkoa.
 
Naelewa sasa kwa nini 'EMOTIONAL INTELLIGENCE' ni one of the key skill waajiri wanahakikisha wanaoomba kazi wanayo.

Bado tunasafari ndefu.
 
Kweli kabisa we call it insubordination
 
Kweli sikuamini kama ni RC nimjuaye tangu SIMUYU,,,,,,MABAEGE KAKA SASA UMESIFIWA its true unaanya kazi nzuri mnooo...ila kwa hili noooooo...UMEOMBA MSAMAHA NGOJA TUONE KAMA MAMA NA YEYE ATAPOKEA aliwanya jamani MEBEGA MABEGA
Kapandisha sana mabega juu...huyu Mtaka
mama inabidi achukue mkasi wake ayapunguze
 
Najua huyu jamaa yangu hawezi kubaki ofisini ila ni kama katupiwa kagundu maana siyo kwa kuongea kule. Mpaka muda huu tuna kikao cha dharura kujadili ni nini kimempata rafiki yetu na mwana jamii wetu?
Hakupiga bapa kweli....
 
Kwani alikuwa anaongea na watoto?
 
Kasome katiba utaelewa vizuri bwasheee. Waziri na mbunge wanaweza kufokeana. Lakini sio RC. Ndio maana akina Gambo waliachana na URC, mbunge anaweza kusema chochote atakacho.
Kwa taarifa yako, waziri na RC wako level moja !
 
Huyo mjita akili hana anajua yeye ndo mwenye akili wengine hawana maana. Huyo waziri ni mkubwa kwake kicheo na kiumri pia kwa maadili ya kiafrika huyo ni kama mama yake,Alishindwa kumpigia simu au kuomba mda wa kuonana nae na kuweka mambo sawa.
Kwa upande mwingine Mtaka alishawahi kusikika akiwaambia wakuu wa wilaya waache barehe ya madaraka ,je yeye hiyo siyo barehe ya madaraka?
Watanazia inapofikia hatua mtu kapotoka nilazima aambiwe ukweli ili aweze kujiafunza na ukweli huo usemwe bila kupepesa macho kwa manufaa ya kizazi hiki na kijacho.
Kwa tabia yake ya kuwaambia watotot wampuuze mama maana yake waziri hata kama akitokea mbele ya watoto hao aweze hata kuzomewa maana hana maana kwao.
Kitu cha msingi kwa Mtaka ajitafakari kuwa yeye ni kioo cha jamii, lakini pia inabidi apingane na asili ya kabila lake ya sifa na ujuaji usiokuwa na maana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…