RC Antony Mtaka kumsema Waziri mbele watoto umekosea. Kama watoto wakimdharau, watamheshimu nani?

RC Antony Mtaka kumsema Waziri mbele watoto umekosea. Kama watoto wakimdharau, watamheshimu nani?

Najua huyu jamaa yangu hawezi kubaki ofisini ila ni kama katupiwa kagundu maana siyo kwa kuongea kule. Mpaka muda huu tuna kikao cha dharura kujadili ni nini kimempata rafiki yetu na mwana jamii wetu?
Wakimuondoa ndio watakuwa wanaizika ccm
 
Ameteleza kwa kusema ukweli! Binafsi nawakubali sana watu wanaosema ukweli.

Hayo mambo ya kubembelezana na kufichiana madhaifu, yalishapitwa na wakati.
Eti mtu kuongea ukweli anakosea Magufuli mwenyewe alikuwa akiwazalilisha tu mbona walikuwa hawasemi

Makonda, PolePole, Wakina,Gambo, happi na Sabaya walizalilisha watu wangapi?

Kwani waziri kuzalilishwa yeye sio MTU kama watu wengine?

Hawa watu hawajielewi kabisa

Wakina mollell mpaka walisema Mbowe anahusika na shambulio la lissu bila ushahidi ila mpaka Leo wapo offisini?

Nchi hii tuna watu wa ajabu sana
 
Binafsi nimepata fursa ya kutazama clip moja ikimuonyesha mheshimiwa mkuu wa mkoa wa Dodoma akiongea nawananchi kuhusu suala la kambi za masomo ya ziada kwa wanafunzi wakati wa likizo.

Kama mwananchi nimesiitishwa na baadhi ya maneno yaliyotumika pale.

Hoja yangu hapa sio SAHIHI au KUTOKUWA SAHIHI kwa tangazo lile la mheshimiwa waziri wa elimu.

Hata mimi binafsi, natofautiana na tangazo lile la kusitisha camp za masomo wakati wa likizo kwa watoto wetu.

Tatizo lililopo hapo ni lugha, iliyotumiwa na mheshimiwa mkuu wa mkoa wa Dodoma kwenye kufikisha ujumbe wake kwa wananchi

Je kulikuwa na ulazima gani kwa mheshimiwa mkuu wa mkoa, kusema kuwa aliyetoa/ waliotoa tangazo lile, alifanya/walifanya hivyo kwa kuwa tu mtoto/ watoto wake wanasoma nje ya nchi?

Maana ya kauli hiyo inaweza kuwa.

Kwamba kuwa watu tuliowapa/ waliopewa dhamana ya kusimamia elimu nchini kwetu, hawana uchungu wa elimu yetu, kwa sababu tu watoto wao wasoma nje ya nchi.

Kauli hiyo sio kwamba tu inamdhalulisha mteule wa Rais, bali pia inaweza kuwa inamkosea heshima hata aliyemteua yeye mheshimiwa mkuu wa mkoa Dodoma.

Kama ningekuwa mimi ndio mkuu wa mkoa wa Dodoma.

Ningewaambia wananchi, nyie endeleeni na utaratibu wa kuweka kambi za masomo ya ziada, wakati sisi kama uongozi wa mkoa, tunaendelea kufanya mawasiliano na wenzetu wa wizara ya elimu.

Uongozi ni dhamana, ni dhamana kubwa, ni muhimu sana kwa kiongozi kuchunga ndimi zao, pale wanapozungumza na wananchi/ umma.
Mkuu wa mkoa kazungumza kama mwananchi wa kawaida.

Tunapowaambia katiba mpya ni muhimu mtuelewe tunaona mbali 100 miles kuliko nyinyi.
 
Prof. Ndalichako yupo sahihi. Maisha si kupekua karatasi tu, kuna maisha mengine na mtoto anapaswa kuyajua na kujifunza.
TATIZO LIPO KWENYE MUUNDO WA WIRAZA YA ELIMU KWA UJUMLA.
KADIRI YA MUUNDO WA SASA HATA DEO ANAWEZA KUMFOKEA WAZIRI NA DEO ASIFANYWE CHOCHOTE.
HAKUNA MUUNGANIKO BAINA YA WIZARA NA ELIMU YA MSINGI/SEKONDARI.
 
Una hakika watoto wa Mtaka wanasoma kayumba?

Yule alikuwa anatafuta sifa za kijinga kwa wananchi hata kama alikuwa na pointi, ila alivuka mipaka ya uwasilishaji wa ujumbe wake.
Lakini si kasema ukweli ?
 
Una hakika watoto wa Mtaka wanasoma kayumba?

Yule alikuwa anatafuta sifa za kijinga kwa wananchi hata kama alikuwa na pointi, ila alivuka mipaka ya uwasilishaji wa ujumbe wake.
Hiyo haihusiani na hoja yake hata kama watoto wake wanasoma private ila hoja yake ni kujari na watoto wa wengine wawe na muda wa kutosha kusoma ili wafaulu

Kuliko waziri ambaye hana uchungu huo
 
Prof. Ndalichako yupo sahihi. Maisha si kupekua karatasi tu, kuna maisha mengine na mtoto anapaswa kuyajua na kujifunza.
TATIZO LIPO KWENYE MUUNDO WA WIRAZA YA ELIMU KWA UJUMLA.
KADIRI YA MUUNDO WA SASA HATA DEO ANAWEZA KUMFOKEA WAZIRI NA DEO ASIFANYWE CHOCHOTE.
HAKUNA MUUNGANIKO BAINA YA WIZARA NA ELIMU YA MSINGI/SEKONDARI.
Umenikumbusha mbali sana DEO,miaka hiyo nikiwa mwalimu😂😂😂😂
 
Kutokusoma shule ya kata sio kosa wala jinai. Kama waziri au mtu yeyote ana uwezo wa kumpeleka mwanae shule iliyo bora zaidi sio jinai.

Waziri anetoa tamko kwa jambo lililo katika mandate yake hivyo hakukosea.

Unapolilia utawala wa sheria unatakiwa umaanishe na usifanye unafiki.

Hayi makambi kuna wazazi wengi tu hawayataki .
Kwani ambaye ataki analazimishwa? Pumbavu kweli ambaye hataki anaacha watoto wanataka kusoma

Acha upumbavu wako simiyu ya 2014 na simiyu ya 2021 kielimu zipo sawa? Kama sio sawa unajua ni kwanini?

Wewe najua Huyo waziri ni mkeo au mama yako toeni upumbavu wenu hapa
 
Kwani ambaye ataki analazimishwa? Pumbavu kweli ambaye hataki anaacha watoto wanataka kusoma

Acha upumbavu wako simiyu ya 2014 na simiyu ya 2021 kielimu zipo sawa? Kama sio sawa unajua ni kwanini?

Wewe najua Huyo waziri ni mkeo au mama yako toeni upumbavu wenu hapa na akifukuzwa kazi huyu jamaa nawahakikishia hii serikali haifiki 2025
Mpuuzi mkubwa wewe.
 
Nimefedheheshwa sana na kauli ya mkuu wa mkoa wa Dodoma ndugu Antony Mtaka juu ya kuwataka wadau wa elimu na wananchi wa Dodoma kutotii muongozo wa wizara ya elimu wa kutaka wanafunzi wote masomo yaishe saa 9 alasiri.

Kwanza mkuu wa mkoa amepotoka kwa kutaka watu wasome muda wote bila kupumzika na ili atambue hilo anapaswa kujua kuwa Katazo lile linawasaidia walimu na wanafunzi kupumzika, kufanya shughuri zingine za kijamii n.k.

Elimu inatambua muda wa kupumzika ndiyo maana kila Aristotle, Maria Montisori na wengine wengi walihimiza mfumo wa mihula ili watoto wawe na uwezo wa kuyatambua maisha ya nje ya kitaaluma.

Kutokana na katazo la wizara ambalo kisera ni muongozo ni wazi wadau wote wa elimu wanafahamu umhimu wa wake kwa watoto wetu. Mkuu wa mkoa ni mtekelezaji wa maagizo na msimamizi wa sheria mkoani kwake, kupinga kwake tamko hili ni wazi amekosa busara na tayari ameshaota kiburi.
Nilikuwa namheshimu sana lkn kwa hili,Hapana hata kidogo,Hat a kama Ana hoja lkn hawezi kutumia lugha ya kejeli,na kashfa kumkashifu kiongozi mkuu kama w azri. Suala la kusoma kwa ratiba ni la kisera.yeye analazimisha tu kutafuta kiki.
 
1 Dorothy Gwajima
2. Ndalichako
3. Mwigulu Nchemba
4. Prof Kitila
5. Prof Kabudi
6. Ndugulile.


Kwenye hiyo orodha tulipigwa waziwazi
Hasa huyo doroty gwajima, mollel, wapumzishwe haraka watu wanapuputika ka wizara imelala tu mbona ummy mwalimu alikuwa active kipindi kile na watu wakawa serious.
Huyo ndalichako si ndo alikuwa anakuja na mtaala wa historia mpya kwa kiswahili kuanzia la kwanza Hadi chuo kikuu wakati wanajua history ipo ka somo. Naona naye apunzishwe tu Kwa kweli
 
Kuna mtu amemfanyia uchawi Mtaka ili apigwe chini, siamini Kama Ni akili yake kuongea yale Mshana Jr
 
Back
Top Bottom