RC Arusha Apiga Marufuku Ada ya Matumizi ya Vyoo Hospitali ya Mount Meru

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Kenani Kihongosi, amepiga marufuku kutozwa fedha kwa wananchi wanaotumia vyoo vilivyopo katika eneo la mochwari ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha-Mount Meru kufuatia malalamiko ya wananchi kwamba wamekuwa wakitozwa shilingi 200 kwa kila matumizi.

Akizungumza Agosti 12, 2025 wakati wa ziara yake fupi katika hospitali hiyo, Kihongosi ametembelea eneo la mochwari na kushuhudia mazingira ya utoaji huduma, kabla ya kutoa agizo la kusitishwa mara moja kwa malipo hayo.

Aibu seriKali ya CCM kufanya mavi ya wagonjwa kuwa kitega uchumi chake
 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Kenani Kihongosi, amepiga marufuku kutozwa fedha kwa wananchi wanaotumia vyoo vilivyopo katika eneo la mochwari ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha-Mount Meru kufuatia malalamiko ya wananchi kwamba wamekuwa wakitozwa shilingi 200 kwa kila matumizi.

Akizungumza Agosti 12, 2025 wakati wa ziara yake fupi katika hospitali hiyo, Kihongosi ametembelea eneo la mochwari na kushuhudia mazingira ya utoaji huduma, kabla ya kutoa agizo la kusitishwa mara moja kwa malipo hayo

Hatua hiyo imekuja baada ya baadhi ya wananchi kulalamikia gharama hizo, wakieleza kushangazwa na kutozwa kiasi hicho cha fedha katika taasisi ya umma

Mnamo Agosti 11, 2025, wakizungumza na Jambo TV nje ya chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali hiyo, baadhi ya wananchi walisisitiza kuwa hawapaswi kulipia huduma hiyo kwa kuwa hospitali ni mali ya serikali

“Serikali ituangalie. Leo nimeshangazwa mtu kutozwa shilingi 200 kutumia choo cha mochwari kwenye hospitali ya serikali? Hapana, kwa kweli si sawa,” alisema Elizabeth Joseph, mkazi wa Arusha

Kihongosi ameagiza uongozi wa hospitali hiyo kuhakikisha huduma ya vyoo inatolewa bure kwa wananchi na kuwataka wasimamie kwa ukamilifu utekelezaji wa agizo hilo, akisisitiza kuwa taasisi za umma hazipaswi kuwa kero kwa wananchi wanaohitaji huduma za msingi

Chanzo: Jambo TV
 
Back
Top Bottom