RC Arusha na timu yake waonesha uwezo mdogo wa kuwaza kuhusu upangaji Machinga

RC Arusha na timu yake waonesha uwezo mdogo wa kuwaza kuhusu upangaji Machinga

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2018
Posts
539
Reaction score
3,507
Wataalamu wa serikali ya awamu ya tano wa Jiji la Arusha wameona wawapange wamachinga kwa mfumo huu
1. Soko la Mbauda litakuwa la nguo za mitumba.

2. Soko la Machame Luxury litakuwa la vyombo na vifaa vya umeme.

3. Soko la Ulezi litakuwa maalumu kwa nguo za dukani.

4. Soko la Kilombero kiwanja namba 68 litauza mbogamboga na Matunda tu.''

Ukisoma mchanganuo huu uliotolewa hapo utabaini Kuna tatizo lakufikiri Kama siyo ukosefu wa exposure katika ulimwengu wa Sasa ambao wakati au muda nikitu kinacholindwa Sana. Katika ulimwengu wa sasa Dunia inawaza namna bora yakupata huduma zote muhimu katika eneo moja. Walichofanya Arusha nikutuambia kwamba unatakiwa ununue nyanya point A upande daladala ukanunua kifaa Cha umeme point B then usafiri ukanunue nguo ya mtumba point C then usafiri ukanunue nguo ya special point D. Hii biashara ya wapi?

In simple logic walichopanda kufanya nikutathimini point A inabeba machinga wangapi then wagawe eneo kwa huduma zote, waende point nyingine waangalie mahitaji wafanye mgawanyo nk Kwa utaratibu huu mtu akiw Kilombero anapata bidhaa zote, akienda machame luxy anapata bidhaa zote so ni uamuzi uende soko gani.

Tujifunze kuumiza ubongo tuachane na matamko, lakini pia haiwezekani nchi nzima tuwaze kutatua tatizo kwa pamoja. Kila mkoa ukae utathimini na uje na solution tuachane na kukimbizana kuonekana Kama sisi wa kwanza kutekeleza maagizo.
 
Zipo supermarket Arusha nyingi zinauza vitu vyote sehemu moja, pia Kuna soko kuu na masoko ya mitaani Arusha karibu mitaa yote, ila hizo huduma zilizopangwa kama machinga acha zigawanywe tu.
 
Wamepongezwa? Let us be serious, unapongeza kutawanya huduma? Huyo aliyepongeza akawaulize shirika la posta kwanini Wanamradi wakuwakutanisha watoa huduma za posta pamoja waliozindua juzi?

Badala tuwaze kuokoa muda tunamp9ngeza mtu aliyekuja na mpango wakupotezea wananchi muda? Anajua umbali wa hayo maeneo yaliyotengwa Arusha? Sijui nani ametuloga.

Kama Kilombero panafaa kupokea machinga 1000 walichopaswa kufanya nikuelekeza machinga 200 wa mitumba, Mia mbili wa mbogamboga, Mia mbili special clothes nk then wanawaelekeza watengeneze vizimba Kama vilivyobunia na DC wa Morogoro. Kila anayesajiliwa anapewa eneo na kibanda chake.

Then wanaenda soko jingine ,siyo kuclasfy machinga kulingana na bidhaa zao. Wanunuzi watabaki kujazana karibu na stend ambapo bidhaa zinapatikana sehemu moja au vinginevyo watu watabaki mjini katikati wakiuza mikononi.
 
Back
Top Bottom