DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha, ameibua mjadala mkali wa kisiasa baada ya kudai kuwa baadhi ya wagombea wa kisiasa wamekuwa wakijaribu kumshawishi kwa fedha ili waweze kufanikisha ushindi katika kura za maoni kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.
Akizungumza mbele ya viongozi wa serikali, vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na wananchi wa mkoa huo, Chacha alitoa onyo kali kwa wagombea hao, akisema kuwa hatafumbia macho jaribio lolote la kuhujumu maadili ya utumishi wa umma kwa njia ya rushwa au ushawishi wa kifedha.
“Hakuna fedha zinazoweza kunibadilisha msimamo wangu. Nitahakikisha mchakato wa uchaguzi unafanyika kwa haki, amani na uwazi kwa manufaa ya wananchi wote wa Tabora,” alisisitiza Chacha.
Aidha, alisisitiza kuwa kama mtendaji mkuu wa serikali mkoani, jukumu lake ni kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru na wa haki, huku akiwataka viongozi wengine katika mkoa huo kuiga mfano huo kwa kutenda haki bila upendeleo au kuegemea upande wowote wa kisiasa.
Chacha pia alikumbusha kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, ameshatoa maelekezo kwa TAKUKURU kuhakikisha hatua kali za kisheria zinachukuliwa dhidi ya mtu yeyote atakayebainika kujihusisha na vitendo vya rushwa wakati wa uchaguzi.