GE2025 RC- Chacha Agomea Millioni 5 za mtia nia amchana Makavu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha, ameibua mjadala mkali wa kisiasa baada ya kudai kuwa baadhi ya wagombea wa kisiasa wamekuwa wakijaribu kumshawishi kwa fedha ili waweze kufanikisha ushindi katika kura za maoni kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.

Akizungumza mbele ya viongozi wa serikali, vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na wananchi wa mkoa huo, Chacha alitoa onyo kali kwa wagombea hao, akisema kuwa hatafumbia macho jaribio lolote la kuhujumu maadili ya utumishi wa umma kwa njia ya rushwa au ushawishi wa kifedha.

“Hakuna fedha zinazoweza kunibadilisha msimamo wangu. Nitahakikisha mchakato wa uchaguzi unafanyika kwa haki, amani na uwazi kwa manufaa ya wananchi wote wa Tabora,” alisisitiza Chacha.

Aidha, alisisitiza kuwa kama mtendaji mkuu wa serikali mkoani, jukumu lake ni kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru na wa haki, huku akiwataka viongozi wengine katika mkoa huo kuiga mfano huo kwa kutenda haki bila upendeleo au kuegemea upande wowote wa kisiasa.

Chacha pia alikumbusha kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, ameshatoa maelekezo kwa TAKUKURU kuhakikisha hatua kali za kisheria zinachukuliwa dhidi ya mtu yeyote atakayebainika kujihusisha na vitendo vya rushwa wakati wa uchaguzi.
Your browser is not able to display this video.
 
Kwa Nchi km hii watu km hawa hua hawapendwi kihivyo sababu watu wengi hawapendi kuambiwa ukweli na hawapendi kunyooshwa, haya sasa mwambie hapo asimamie No Reform No Election atakwambia hakuna mwaka wa uchaguzi uchaguzi haujafanyika maana hilo ni takwa la kitaifa
 
Huyu RC mnafiki tu. Mbona hajazigomea pikipiki na baiskeli za Samia?
 
Liongo
 
Viongozi wazuri wataendelea kutokea kanda ya ziwa.

Hii kanda ya Pwani ni Viongozi wapuuzi watupu.
Hongera RC Chacha japo nyumbu watapinga.
 
Angejaribu 20, huyo hakuwa amejIpanga vizuri
 
Your browser is not able to display this video.
TABORA – Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha, ameibua mjadala mkali wa kisiasa baada ya kudai kuwa baadhi ya wagombea wa kisiasa wamekuwa wakijaribu kumshawishi kwa fedha ili waweze kufanikisha ushindi katika kura za maoni kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.

Akizungumza mbele ya viongozi wa serikali, vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na wananchi wa mkoa huo, Chacha alitoa onyo kali kwa wagombea hao, akisema kuwa hatafumbia macho jaribio lolote la kuhujumu maadili ya utumishi wa umma kwa njia ya rushwa au ushawishi wa kifedha.

“Hakuna fedha zinazoweza kunibadilisha msimamo wangu. Nitahakikisha mchakato wa uchaguzi unafanyika kwa haki, amani na uwazi kwa manufaa ya wananchi wote wa Tabora,” alisisitiza Chacha.

Aidha, alisisitiza kuwa kama mtendaji mkuu wa serikali mkoani, jukumu lake ni kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru na wa haki, huku akiwataka viongozi wengine katika mkoa huo kuiga mfano huo kwa kutenda haki bila upendeleo au kuegemea upande wowote wa kisiasa.

Chacha pia alikumbusha kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, ameshatoa maelekezo kwa TAKUKURU kuhakikisha hatua kali za kisheria zinachukuliwa dhidi ya mtu yeyote atakayebainika kujihusisha na vitendo vya rushwa wakati wa uchaguzi.

Chanzo: Habari Leo
 
Mimi sielewi. Mkuu wa Mkoa anahusika vipi na uchaguzi wa ndani wa chama cha siasa?

Amandla...
Swali zuri hili...

Labda kwa sababu nyakati hizi wakuu wa Mikoa na Wilaya wengi wao ni makada wa Ccm
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…