RC Chalamila ahoji kama Bandari imeuzwa mbona soko la Ferry bado lipo. Asema waliopotosha wote wako ndani na wataendelea kukamatwa wakiibuka wengine

Kuna ambaye ameona hii ni hoja sahihi ya kwamba kwakua wavuvi wapo basi hapajauzwa?

Kuna uhusiano wa bandari na soko la Ferry?

Nafikiri RC ameharibu kuonyesha kwamba wanaokamatwa ni yeyote atakayetaka kuongelea ishu ya bandari.
Hakika ametusaidia kujua sababu ya kukamatwa kwa Watanganyika. Kumbe hakuna cha uhaini wala nini.
 
Halafu kweli Afrika tunahitaji kufanya utafiti kwa nini Watu weusi hatuendelei kama kiwango cha hoja zenyewe ndiyo hizi?
 
Hoja zijibiwe, kifungu kwa kifungu...

Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya β€˜Makubaliano’ na β€˜Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya β€˜Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
 
Jamaa wakati mwingine awe ananyamaza tu.

Kumbe bandari inahusika na kuuza samaki?!

Hiyo ndio akili ya Rais wa Mkoa wa Dsm
Hadi nimeshangaaa, uuzaji wa Samaki na bandari wapi na wapi? Halafu kitu kikiuzwa kwani watu mnafukuzwa hapo hapo? Aende Futuhi tu, panamfaa
 
"Wale wote waliosema bandari imeuzwa na wakakaa wakapotosha watu leo hii wako ndani wote na nimewaambia fanyeni fujo mnavyofanya nitashughulika na mtu mmoja mmoja," - Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila akizungumza ndani ya Supa Breakfast ya #EastAfricaRadio

 
Tundu Lissu: Hii ni akili au tope?
 
Chalamila na domo lake kama papa si ndio hili lilisema mbele ya jiwe linashukuru linalipwa mshahara mpaka linaweza kuwa na kamchepuko ama sio hili.
 
 

Attachments

  • IMG_1932.MP4
    10.7 MB
  • IMG_1931.MP4
    3.9 MB
  • IMG_1926.MP4
    14.7 MB
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…