RC Chalamila aongoza wananchi kufanya usafi - Dar es salaam

RC Chalamila aongoza wananchi kufanya usafi - Dar es salaam

Venus Star

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2018
Posts
26,519
Reaction score
78,311
Na Mwandishi Wetu

-Asema Tanzania inaingia kwenye historia nyingine ya kuwa mwenyeji wa Mkutano mkubwa wa Marais wa Afrika
1737794059487.png

-Atoa taarifa ya kufungwa kwa baadhi ya barabara siku chache ambazo ugeni utakuwa katika Mkoa huo

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Januari 25, 2025 ameongoza mamia ya wananchi wa Wilaya ya Ilala kufanya usafi katika eneo la uwanja wa ndege wa Kimataifa Mwl JK Nyerere barabara ya Terminal One kuelekea mjini (City centre) ikiwa ni maandalizi ya mapokezi ya ugeni mkubwa wa Marais wa Afrika ambao wanatarajia kuwasili kuanzia leo.

RC Chalamila amesema Tanzania inaingia kwenye historia ya kuwa mwenyeji wa mkutano mkubwa wa Marais wa nchi za Afrika kujadili masuala ya Nishati ambao utafanyika tarehe 27-28/01/2025 katika ukumbi wa JNICC Jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo unakuja na fursa nyingi za kiuchumi kwa Mkoa na Taifa kwa ujumla ambapo Mhe Mkuu wa Mkoa amewataka wakazi wa Mkoa huo kuzitumia vizuri fursa hizo.

Aidha RC Chalamila amesisitiza umuhimu wa kuweka Mkoa katika hali ya usafi nyakati zote za ugeni huo ukiwa katika mkoa wetu na mara baada ya kuondoka tabia ya usafi iwe ni utamaduni wa kila siku kwa kila mtu.
1737794091219.png

Vilevile RC Chalamila amesema kwa kuwa ugeni huo ni mkubwa baadhi ya barabara zitafungwa kwa siku chache ambazo ugeni huo utakuwepo katika Mkoa wetu.

Mwisho Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe Edward Mpogolo ameshiriki pia katika zoezi hilo la kufanya usafi akiwa ameambatana na viongozi wengine wa Wilaya hiyo.
 
Kwa hiyo mitaa inatakiwa kuwa safi wakati tukitembelewa na marais wengi tuu!!??
Hii nchi tuna viongozi vilaza na wapenda show - offs kuliko maelezo.
 
Yaani RC amekaa mkoa wenye resources zote lkn amekosa ubunifu, hy ya usafi tena wakati wa ugeni ndo anaweza!..... Makonda na Mtaka watabaki kuwa best RC's ever hawa kina Mwagito waendelee na Cheka show!
Kwahiyo unataka asifanye usafi? 🤣 🤣 🤣 Bange ni mbaya sana. Utatumia cha Arusha au Malawi?
 
Yaani RC amekaa mkoa wenye resources zote lkn amekosa ubunifu, hy ya usafi tena wakati wa ugeni ndo anaweza!..... Makonda na Mtaka watabaki kuwa best RC's ever hawa kina Mwagito waendelee na Cheka show!
Eti Makonda!? Unachekesha kweli.
 
Back
Top Bottom