RC Chalamila asema mjamzito anayegoma kununua gloves akajifungulie nyumbani. Hafai kuendelea kubaki madarakani

RC Chalamila asema mjamzito anayegoma kununua gloves akajifungulie nyumbani. Hafai kuendelea kubaki madarakani

Kaamua kutumia lugha fananishi. Ila pointi yake ni kuwa ni muhimu wateja wafahamu kuna KUCHANGIA huduma na sio porojo porojo.
Yeye hajabishia kuchangia bali kampigia Mkuu wa mkoa Ili kuelimishwa na Siyo kunyanyapaliwa

Huyo mama lazima atakuwa ni mwanaccm ndio sababu alipata ujasiri wa kumpigia RC
 
Kaamua kutumia lugha fananishi. Ila pointi yake ni kuwa ni muhimu wateja wafahamu kuna KUCHANGIA huduma na sio porojo porojo.
Na waelewe wasipochangia,dawa na vifaa vitaisha bila kupata fedha za kununua vingine.Hao wagonjwa watakaofuata watatibiwaje?Yaleyale ya mikopo ya JK na bodi ya mikopo elimu ya juu kutolipwa na kuzua tafrani tu.
 
Yeye hajabishia kuchangia bali kampigia Mkuu wa mkoa Ili kuelimishwa na Siyo kunyanyapaliwa

Huyo mama lazima atakuwa ni mwanaccm ndio sababu alipata ujasiri wa kumpigia RC
Mpaka kufikia kumpigia Mh, lengo lilikuwa ni kuchongea uongozi kwa Mamlaka.

Kama ingekuwa ni kupata ufafanuzi mbona hapo hapo hospitalini kuna kuwa na madawati ya malalamiko na maelekezo.

Ni muhimu watu wetu waelewe uhalisia juu ya huduma na namna ya kuchangia na sio porojo za bure.

Same mgonjwa akienda MNH akiambiwa alipie wala hapigi simu kwa mkuu wa Mkoa, why Temeke?!
 
Yeye hajabishia kuchangia bali kampigia Mkuu wa mkoa Ili kuelimishwa na Siyo kunyanyapaliwa

Huyo mama lazima atakuwa ni mwanaccm ndio sababu alipata ujasiri wa kumpigia RC
Unajua maana ya kunyanyapaliwa?Hajatengwa wala kudharauliwa na mtu.Amepewa uhalisia.Ni juu yake kusuka au kupiga panki.
 
Naomba Unitajie Makosa yako Binafsi naona Yuko Sahihi kabisa..
Tusichanganye siasa na Proffesional..

Hospitali haiwezi kuwa Na Vifaa Vyote na Daw zote kila Muda
WATANZANIA WAMEZOEA KUDANGANYWA!!!

TUPATE VIONGOZI MFANO WA CHALAMILA NA TUNTU LISSU KAMA 50 HIVI ITASAIDIA HII INCHI KUPENDA UKWELI!!!
 
Mpaka kufikia kumpigia Mh, lengo lilikuwa ni kuchongea uongozi kwa Mamlaka.

Kama ingekuwa ni kupata ufafanuzi mbona hapo hapo hospitalini kuna kuwa na madawati ya malalamiko na maelekezo.

Ni muhimu watu wetu waelewe uhalisia juu ya huduma na namna ya kuchangia na sio porojo za bure.

Same mgonjwa akienda MNH akiambiwa alipie wala hapigi simu kwa mkuu wa Mkoa, why Temeke?!
Wewe unadhani mama aliye Kwenye Uchungu Namba ya RC aliipataje?

Na unadhani kwanini Chalamila alipokea simu haraka na kutoa majibu ya Kwenye Kanga 🐼😂

Yajayo yanafurahisha
 
" Kamwambie mumeo anunue mkasi akuzalishe" Ni kunyooka au Taarabu?!! 🐼

Unaweza kukuta huyo mama na RC wanajuana vizuri tu ndio sababu wakapeana na Namba za Simu Sasa Chala anaona Wivu kinyonge 😂😂😂
Hatujui waliongea mangapi kabla ya kupewa sentensi hiyo.
NB;Chalamila ni msanii.Si ajabu katunga story ili apate mwanya wa kufikisha ujumbe.Kaa chonjo saa mbaya hii.
 
Kosa la jamaa ni kuongea ukweli kwa lugha ngumu ila ukweli ndo huo hospital hazina vifaa usipojisimamia ukawa huna hela unakufa kweli, shida ni kuwa tumezoea kuambiwa maneno Malaini yasiyo na ukweli, hapo angesema usichangie chochote vifaa vipo angepigiwa makofi lakini je ni kweli vifaa vipo? Jibu ni hapana siyo kweli.

Utaambiwa elimu ni bora na inatolewa bure usichangie chochote na waalimu hawaruhusiwi kuchangisha mchango wowote hata wa tuition je ni kweli elimu hiyo ina ubora huo ? Jibu siyo kweli ili mtoto wako apate elimu nzuri lazima kuna kitu uchangie ndo maana wao wanapeleka watoto wao shule za kulipia gharama kubwa.

Taasisi nyingi zinazotoa huduma hazijitoshelezi huo ndo ukweli hata kama Chalamila ataondolewa lakini hakuna kitakachobadilika utaendelea kuombwa pesa ya gloves, cha muhimu hapa ni kuyapokea hayo maneno ya ukweli mchungu na kutafuta mzizi kwanini gloves hazipo hapo hadi Rais anawajibu wa kujibu hilo pamoja na waziri wake wa Afya
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Albert Chalamila amewataka wananchi wa mkoa huo kuacha kuingiza siasa katika mambo yanayowahusu binafsi hasa katika Afya kwani hazitawasaidia badala yake zitawachelewesha na pia kuwa na madhara zaidi.

Akizungumza hivi karibuni na wanachi wa Temeke jijini Dar Es Salaam, Chalamila aliwaambia kuna vifaa vya hospitali inapowalazimu wanunue kwani sio wakati wote hospitali zitakuwa na vifaa kamili.

Chalamila alimuelezea mama mmoja mjamzito aliyempigia simu akilalamika kuambiwa na Daktari atoe shilingi elfu 50,000/= ili inunulie vifaa vya kumsaidia kujifungua ikiwemo gloves ambapo Chalamila alimwambia asitoe fedha aende nyumbani akajifungue.

Soma pia: Kauli tata za RC Chalamila kwenye matamko mbalimbali nchini

“mama mmoja amenipigia simu eti Baba nimeambiwa hapa hospitali wameishiwa gloves wameishiwa vifaa vitakavyonisaidia mimi kujifungua wamesema nilipe 50,000/= ili nichangie kwenda kununua vitu vitakavyonisaidia kujifungua”

Chalamila anasema baada ya mama huyo kutokuwa tayari kununua vifaa akamwambia aende akajifungue nyumbani “Nikamwambia Mama pole kwanza hiyo siyo haki toka nje chukua bajaji nenda zako nyumbani kamwambie mumeo achukue kisu na mikasi akusaidie kujifungua”

Aidha amefafanua lengo la kumwambia hivyo ni kwa sababu sio nyakati zote vifaa vipo na pia kuna nyakati inabidi mgonjwa aangalie hali yake kwanza na namna ya kujisaidia kabla ya kulalamika.

Hatujui waliongea mangapi kabla ya kupewa sentensi hiyo.
NB;Chalamila ni msanii.Si ajabu katunga story ili apate mwanya wa kufikisha ujumbe.Kaa chonjo saa mbaya hii.
Majibu ya Chalamila yamejaa Wivu uliotukuka kama Siku ile ya DAS Kisarawe enzi za Shujaa 😂😂😂
 
Bahati mbaya kwa kuendekeza ukada tunajikuta tunateua wagonjwa wa akili kwenye nafasi nyeti!
 
Ase uyo mzee kalopoka tu kuna vitu vinachosha ase asa ilo swala haikuwa na ulazima kupiga simu kwa mkuu wa mkoa
 
Back
Top Bottom