RC Chalamila asema mjamzito anayegoma kununua gloves akajifungulie nyumbani. Hafai kuendelea kubaki madarakani

RC Chalamila asema mjamzito anayegoma kununua gloves akajifungulie nyumbani. Hafai kuendelea kubaki madarakani

Kiongozi unapopigiwa Simu na mpiga kura akakueleza tatizo Usimnyanyapae bali mchukulie Kwa Upendo

Alimjibu hivi mama aliye katika Uchungu wa kutaka kujifungua? 🐼

Kwako Mary Chatanda
HATUA IPI AU CHALAMILA ATOE HELA ZAKE MFUKONI AMNUNULIE VIFAA VYA KUJIFUNGUA???

JE, ATAWANUNULIA WANGAPI???

📌WAAMBIENI UKWELI HAO WAPIGA KURA WENU,KUWA WAJIPAMBANIE MNASEMA HUDUMA BURE KWENYE MAJUKWAA ILA KWENYE VITUO WANATAKIWA WACHANGIE😁😁😁.

MNGEKUWA MMEWAAMBIA TANGU MWANZO KUWA HUDUMA SIO BURE WALA ASINGEPIGA SIMU KUCHONGEA WAHUDUMU WA AFYA ANGELIPA KIMYAKIMYA LABDA ANGEPIGA KWA KUCHELEWESHEWA HUDUMA AU KUTUKANWA HAPO SAWA!!!

📌WATZ WA SASA SIO WA MWAKA 47 NJOONI NA HOJA ZENYE MASHIKO🤝🤝🤝

📌📌📌HATA KWENYE MIRADI(MWENDOKASI,SGR,HUDUMA ZA NDEGE,NK) HUKO KAMA SERIKALI HAIWEZI ISEME UKWELI NA IKUBALI SEKTA BINAFSI WAINGIE WAENDESHE.SERIKALI IBAKI KUWA REGULATOR WA NAULI NA UFANISI!!!
 
Wao si ndiyo wanasema kujifungua bure! ina maana inatakiwa wakati wote vifaa vya kuwezesha kujifungua vinakuwepo wakati wote sasa hizo blah blah zinamhusu nini huyo mama!?
Halafu gloves za 50k ni zipi hizo, maana hata kile kibegi cha kujifungulia msd ni 22k maduka ya kawaida ni 25k sasa hiyo 50k ni ya nini yote hiyo, ndiyo maana huyo mama alishtuka anataka kupigwa sasa huyu mkuu wa mkoa hata afikirii anaona labda huyo mama hana uwezo
 
Wewe unadhani mama aliye Kwenye Uchungu Namba ya RC aliipataje?

Na unadhani kwanini Chalamila alipokea simu haraka na kutoa majibu ya Kwenye Kanga 🐼😂

Yajayo yanafurahisha
Na unafikiri aliepiga simu ni mgonjwa?!
 
CHALAMILA AMEONA HAKUNA HAJA YA KUENDELEA KUDANGANYA RAIA.

AMEAMUA ANYOOKE KAMA RULA😁😁😁UKIAMUA KUBEBEA MIMBA UWE UMEJIPANGA.MAMBO YA KUZAA ZAA HOVYO WAKATI HUWEZI KUITUNZA MIMBA WALA MTOTO NI UMASIKINI WA FIKRA NA AKILI.

NCHI TAYARI INA WATU MILLIONI 60 UNAKUTA MTU BADO ANAZAA HOVYO WAKATI YEYE MWENYEWE KUJIHUDUMIA HAJIWEZI.

📌📌TZ HATUNA UPUNGUFU WA WATU.WATU WAJIFUNZE KUZAA KWA MPANGO.
Mkuu million 60 unaona wengi.?
 
Na hilo jambo la kuhifadhi vifaa vya kujifungulia pamoja na fedha za akiba wajawazito na ndugu zao husisitizwa sana kabla hawajafikia hatua ya kujifungua.Hapo ni kipi kilikuwa kigeni?Kujilalamisha tu hao watu kidumavu kwenye akili.
Huyo ni wale wapambe nuksi na amepigwa KO!!! atakuwa ni wale ndugu wanaoshinda wamevaa nguo za kijani hawatakagi kufanya kazi za kuingiza vipato(wazee wa kamserereko)kila mahali wao wanajitambilisha kama MAKADA😁😁
 
Mbna kaongea uhalisia kabisa mi sioni kosa sema watanzania tunapenda soft language

Sema shida ipo ni wakina nani ndio waliwazoesha wananchi matibabu ya bure hapa ndio shida ilipoanza sasa washazoea
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Albert Chalamila amewataka wananchi wa mkoa huo kuacha kuingiza siasa katika mambo yanayowahusu binafsi hasa katika Afya kwani hazitawasaidia badala yake zitawachelewesha na pia kuwa na madhara zaidi.

Akizungumza hivi karibuni na wanachi wa Temeke jijini Dar Es Salaam, Chalamila aliwaambia kuna vifaa vya hospitali inapowalazimu wanunue kwani sio wakati wote hospitali zitakuwa na vifaa kamili.

Chalamila alimuelezea mama mmoja mjamzito aliyempigia simu akilalamika kuambiwa na Daktari atoe shilingi elfu 50,000/= ili inunulie vifaa vya kumsaidia kujifungua ikiwemo gloves ambapo Chalamila alimwambia asitoe fedha aende nyumbani akajifungue.

==================================================

Mwenye direct connection amfikishie mama SSH ujumbe huu, atuondolee huyu MTU hapa dsm, ampeleke Rauha akalinde wanyama, hafai kuwa kiongozi

View attachment 3214512
Chalamila bwana , akiwa uraiani mtu bomba sana , akiwa Rc wa Mbeya aliwahi nibeba kwenye msafara wake toka Iringa , mtu poa sana, ila wasiwasi wangu may be anapigaga cha Arusha nini?

alie karibu na Makonda ebu mwambieni atujuze tafadhali
 
📌📌NDO MFANYE KAZI HAMNA MBELEKO,UKIBEBA MIMBA UWE UMEJIPANGA KAMA HUWEZI KONDOM ZIPO SHILINGI BUKU TU UNAPATA KITU HAKICHANIKI😁😁😁

#NO FREE LUNCH,HAPA DUNIANI!!!
Nikuulize swali rahisi tu, unajuaje kama yule mama baada ya kubeba ujauzito ule, mumewe alipata ajali na bodaboda akafa?? Sasa kiongozi unapotoa kai kama ile huyo mjane atajisikiaje?? Chungeni kauli zenu Mungu yupo na hadhihakiwi. Usijione mjanja kuwa nacho leo ukamdharau na kumdhihaki asiyenacho leo kwani hujui kesho yako.
 
Chalamila bwana , akiwa uraiani mtu bomba sana , akiwa Rc wa Mbeya aliwahi nibeba kwenye msafara wake toka Iringa , mtu poa sana, ila wasiwasi wangu may be anapigaga cha Arusha nini?

alie karibu na Makonda ebu mwambieni atujuze tafadhali
Chalamila havuti bhangi ila ni Ule Ulanzi wa utotoni Ili alale

Watoto watundu walikuwa wananyweshwa Mkangafu badala ya Mtogwa 😂😂😂
 
Hivi kwani kujifungua kwenye hospitali za serikali bado ni bure?
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Albert Chalamila amewataka wananchi wa mkoa huo kuacha kuingiza siasa katika mambo yanayowahusu binafsi hasa katika Afya kwani hazitawasaidia badala yake zitawachelewesha na pia kuwa na madhara zaidi.

Akizungumza hivi karibuni na wanachi wa Temeke jijini Dar Es Salaam, Chalamila aliwaambia kuna vifaa vya hospitali inapowalazimu wanunue kwani sio wakati wote hospitali zitakuwa na vifaa kamili.

Chalamila alimuelezea mama mmoja mjamzito aliyempigia simu akilalamika kuambiwa na Daktari atoe shilingi elfu 50,000/= ili inunulie vifaa vya kumsaidia kujifungua ikiwemo gloves ambapo Chalamila alimwambia asitoe fedha aende nyumbani akajifungue.

==================================================

Mwenye direct connection amfikishie mama SSH ujumbe huu, atuondolee huyu MTU hapa dsm, ampeleke Rauha akalinde wanyama, hafai kuwa kiongozi

View attachment 3214512
Huyu jamaa ni mjinga na jitu la hovyo kabisa. Unaposema hivyo kama kiongozi unapeleka taswira Gani kwa hospitali za kitanzania? Si kila sehemu tutaambiwa dawa hakuna
 
Back
Top Bottom