Siitetei serikali;
Ukitaka kufanikiwa hapa Tanzania, sahau kuwa una haki ya kuungwa mkono na serikali, fanya mishe zako kwa juhudi.
Tanzania tuna rasilimali na fursa nyingi sana. Ardhi ipo haina kazi, tupambaneni vijana.
Fuga, lima, fanya biashara n.k
Ukienda mpanda kuna maeneo sasa hivi tunavyoongea wanauza shilingi 250,000/= tu kwa ekari moja. Unaweza kupata eneo lako hata ekari kumi ukatumia kukupa pesa.
Nimeenda Kenya mara kadhaa, nikiri kuwa wenzetu ni wachapa kazi kuliko sisi. Vijana wa kitanzania wanawaza kula bata na ngono badala ya kazi. Matokeo yake ni kulalamikia serikali kuomba ajira hafifu za unesi, ualimu. N.k
NB. Ukishindwa kitoboa hapa Tanzania, huwezi kutoboa kwenye nchi yoyote Afrika mashariki.