Adharusi
JF-Expert Member
- Jan 22, 2012
- 14,422
- 7,350
View: https://www.youtube.com/shorts/e-h8zzRwB44?feature=share
RC Chalamila nazani madaraka yamemlevya ..amekua akiwadharau sana watu wa kipato cha chini ,hana lugha mzuri kundi ili la watanzania wenye kipato cha chini .amewashambulia sana wanaume wauza uduvi na kuwaambia wataolewa .
Kumbuka wauza uduvi hao ni baba wa familia ,je wanarudi majumbani kwao wake ,watoto wanawachukuliaje hao wafanya biashara ndogo ndogo
Hizi dharau ambazo amekua akiwadhihaki wanaume au watu wenye kipato cha chini na mamlaka zimakaa kimya ni hatari sana kwa taifa letu.
Chalamila ambae kitaaluma ni Mwalimu, kabla ya kua RC alikua Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa ,kama ni mwana CCM maana yake anajua hali za watanzania zilivyo.
Amekua akitoa kashfa sana kwa watanzania wenye kupato cha chini ..watu watachoka.
Baadhi Wasaidizi wa Rais kazi yao kuwachonganisha watanzania na serikali yao,Ulimi umeendikwa sana kwenye biblia