PakiJinja
JF-Expert Member
- Jan 16, 2012
- 11,689
- 25,848
View: https://www.youtube.com/shorts/e-h8zzRwB44?feature=share
RC Chalamila nazani madaraka yamemlevya ..amekua akiwadharau sana watu wa kipato cha chini ,hana lugha mzuri kundi ili la watanzania wenye kipato cha chini .amewashambulia sana wanaume wauza uduvi na kuwaambia wataolewa .
Kumbuka wauza uduvi hao ni baba wa familia ,je wanarudi majumbani kwao wake ,watoto wanawachukuliaje hao wafanya biashara ndogo ndogo
Hizi dharau ambazo amekua akiwadhihaki wanaume au watu wenye kipato cha chini na mamlaka zimakaa kimya ni hatari sana kwa taifa letu.
Chalamila ambae kitaaluma ni Mwalimu, kabla ya kua RC alikua Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa ,kama ni mwana CCM maana yake anajua hali za watanzania zilivyo.
Amekua akitoa kashfa sana kwa watanzania wenye kupato cha chini ..watu watachoka.
Baadhi Wasaidizi wa Rais kazi yao kuwachonganisha watanzania na serikali yao,Ulimi umeendikwa sana kwenye biblia
Ujumbe niliouelewa happa ni kwamba vijana wenye shughuli za aina hiyo na wanaoingiza kiasi hicho cha pesa na kupelekea kuyaona maisha ni magumu sababu ya kutoweza kumudu gharama zake, wengi wao huishia kuolewa.
Tufanye makisio, ni vijana wangapi wa kitanzania katika level yoyote ile ya maisha waliyopo hawawezi kumudu gharama za maisha hayo? Tukishapata idadi yao, hapo tunaweza tukapata makisio ya Vijana wa kiume ambao wameamua 'kuolewa' ili waweze kumudu gharama za maisha, pia tutapata idadi ya wale ambao wapo hatarini 'kuolewa' ili wasije wakachapika kimaisha.
Alichokiongea Chalamila ni uhalia. Tumekuwa tukipiga kelele sana kuhusu kuongezeka kwa matendo ya kishoga, sasa tumejua kwamba kumbe 'Shetani' ana singiziwa sana kuwa ndiye chanzo, kumbe uhalisia ni vipato vidogo, tamaa na ugumu wa maisha...now you know.