RC Chalamila: Kama huwezi kuishi kota za Magomeni, hamia Vingunguti

RC Chalamila: Kama huwezi kuishi kota za Magomeni, hamia Vingunguti

Wananchi wa magomeni Kota wengi wao ni walalahoi, hawawezi ku afford gharama za kuishi pale, tumepoteza hela walitakiwa wajipate kwanza...ukweli mchungu kumeza
 
Kila siku naona malalamiko kwenye ofisi yangu kutoka kwa wakaaji wa Magomeni kota mara wanalalamika bili ya Maji ni kubwa wameshindwa kulipa wengine wanalalamika kwamba bili ya taka imekuwa kubwa wakati hizo taka wanazalisha wenyewe hii inaonesha wameshindwa kukaa kwenye hizo kota.

Nashauri kama mtu ukiona huwezi kukaa kwenye majengo ya TBA ya Magomeni basi hama uende Vingunguti"

View attachment 3050335
Kwa hiyo vingunguti ndo wanakaa watu ambao hawawezi ishi maghorofani, hapo mkuu wa mkoa ameteleza kabisa
 
Wenye experience ya kuishi kwenye haya majengo ya pamoja, especially yale premium, Service & utility charges huwa ni shilingi ngapi kwa mwezi?.
 
Hii kiburi ya RC Chalamila inatoka wapi? Hivyo ndivyo alivyowajibu wananchi wa Magomeni Magorofa ambao hawawezi kulipa kodi ya taka


My Take:
Rais Samia huyu Chalamila anakuharibia Dar es Salaam big time
 
Huyu naye amezidi kuropoka ropoka sana,siku zake zinahesabika..... yaani Tz unajiuliza hatuna watu smart Kweli kuwa viongozi mpaka tuwe na wajinga wajinga tu? Sijui Tz tumemkosea nini Mungu 😔
 
Wananchi wa magomeni Kota wengi wao ni walalahoi, hawawezi ku afford gharama za kuishi pale, tumepoteza hela walitakiwa wajipate kwanza...ukweli mchungu kumeza
Hivi kwa nini wasiwajengee nyumba ndogo za kawaida hata za vyumba vitatu maeneo kama Mabwepande,Bunju au Tegeta
 
Japokuwa ni mropokaji hasa akishavuta kitu cha Njombe, lakini katika hili yuko sahihi, sasa wanataka nani awalipie umeme, maji na gharama za kuzoa taka wakati wenyewe ndiyo watumiaji? Malalamiko yao ni hayana mantiki kama yamewashinda ya Magorofani wauze wakajenge Chanika.
 
Back
Top Bottom