RC Chalamila: Kama huwezi kuishi kota za Magomeni, hamia Vingunguti

RC Chalamila: Kama huwezi kuishi kota za Magomeni, hamia Vingunguti

Wamepewa Bure kwa miaka Mitano.
Wanalipia Service Charge 30,000 kwa Mwezi na kulipia Umeme wa Jengo na hivyo gharama ni Kama 50,000 kwa Mwezi.
Baada ya miaka 5, itabidi wazinunue au wauze kwa watu watakaokuwa wanataka kununua.
Ndiyo maana hata Magufuli alisema kabisa baada ya miaka 5, wengi watauza.
Ila kuna makandokando mengi hapo Magomeni Kota.
Makandokando gani mkuu? Hebu funguka
 
Huu ndio ukweli ambao wengi hawatapenda kusikia, ila hili la maji, nilisikia Waziri akiliongelea!

Hapo Magomeni Manji alitaka kupaendeleza, JPM akaamua kufanya siasa, akatangaza kuwajengea hao wananchi nyumba hizo ili kumkomesha Manji, wakati mezani kulikuwa na option ya kuwafidia waondoke. Tangu lini serikali kuu ikajengea mwananchi wa kawaida nyumba?!

Sasa wameshakuwa kama watoto, wanalia lia kwa kila kitu, hata wakishindwa ku-pass wind, watalalamika, kuna siku watasema hakuna sehemu ya kuchezea kigodoro, serikali iwafikirie kuwajengea.

Its possible hata design ya mradi huo haukulenga wale wenye maisha ya kuunga unga, unit title inahitaji wanaojiweza, wanakuwa na uongozi au mfumo wa kulipia gharama za pamoja.. waanze kulipia kodi ya majengo na ardhi
Manji tapeli yule uliza alivyojikombea hela kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii
 
Kila siku naona malalamiko kwenye ofisi yangu kutoka kwa wakaaji wa Magomeni kota mara wanalalamika bili ya Maji ni kubwa wameshindwa kulipa wengine wanalalamika kwamba bili ya taka imekuwa kubwa wakati hizo taka wanazalisha wenyewe hii inaonesha wameshindwa kukaa kwenye hizo kota.

Nashauri kama mtu ukiona huwezi kukaa kwenye majengo ya TBA ya Magomeni basi hama uende Vingunguti"

View attachment 3050335
Chalamila mimi binafsi kuna vitu huwa nampinga humu waziwazi bila siri humu jamii forums

Kwa hili kaongea yuko sahihi mia kwa mia waende vingunguti namuunga mkono

Kuna maeneo na majengo wanatakiwa kuishi watu wa kuekeweka wenye vipato vya kueleweka sio wapikia majiko ya mkaa au kuni

Kaongea ukweli mia kwa mia
 
Ila huyu jamaa ukimpa kisu akutoboe akwepeshi anamaliza 😂haya ndugu zangu tuamie vingunguti mara moja
 
Tovuti ya TBA, ukurasa wa "Sisi ni Nani" unaanza kwa kusema "Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ni taasisi ya serikali chini ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi".

Sasa hapo utasemaje si shirika la serikali chini ya wizara?

Serikali ilikuwa haina haja ya kuwa na hilo shirika la TBA na hiyo sehemu ilitakiwa kuwa na nyumba za makampuni ya watu binafsi.

Pia, serikali ingeweza kuweka sheria kwamba kwa kila units fulani za nyumba zitakazojengwa, kuwe na units fulani za low income housing kuhakikisha watu wa kipato cha chini nao wanapata fursa ya kuishi mjini.

Kwa mpango huo, serikali ingejiondoa kwenye kazi za kuwa landlord, kama alivyotaka Mkapa alipouza mashirika ya serikali na kugawa nyumba zake, na watu wa kipato cha chini wangekuwa na nafasi bado ya kuishi mijini.

Ndiyo watu wanavyofanya hivyo.

Sasa sisi serikali yetu haijui inaenda au inarudi, mara inauza nyumba kwa sababu haitaki kuwa na nyumba, mara inajenga nyumba.

Ujinga mtupu.
Wakala wa Majengo hakutakiwa ajenge ila awe Mkaguzi na hiyo Kazi ilitakiwa apewe NHC ambaye hadi Leo ndiyo anajenga Dodoma nyumba nyingi tu.
Shida ni kwamba kipindi cha Magu, Kazi zote za Ujenzi alipewa TANROADS na TBA.
Haikujalisha wana uwezo au hawana.
Sasa hivi TBA wapo hoi hata kumalizia nyumba za Magomeni Kota hawana uwezo na eneo wanalo kubwa bado.
Wangelipewa NHC....

Hilo eneo waliishi hao wenyeji na waliahidiwa patajengwa na watapewa nyumba zao tena.
Manji akaja kwa UJANJA wake na kulichukua eneo ili afanye yake. Hili halikuwa halali kabisa. Ni Sawa leo pale Ilala Kota uondoe watu na ujipange ujenge Gorofa halafu aje Mjanja mmoja alichukue eneo na kufanya Mali yake....

Kuna Siasa nyingi bado zipo hapo.
 
so hii service charge ya 30,000 ndo wamewekewa vitasa
nayo inawachenga?
Yaani hata hii 30,000 huwa hawataki kulipa kwamba ni kubwa. Na ndicho anakiongea RC.
Nina uhakika hata wakisema 5,000 kuna watu watalalamika bado kwamba ni kubwa. Ndiyo maana wanaambiwa wahamie kusiko na Service Charge.
 
Kila siku naona malalamiko kwenye ofisi yangu kutoka kwa wakaaji wa Magomeni kota mara wanalalamika bili ya Maji ni kubwa wameshindwa kulipa wengine wanalalamika kwamba bili ya taka imekuwa kubwa wakati hizo taka wanazalisha wenyewe hii inaonesha wameshindwa kukaa kwenye hizo kota.

Nashauri kama mtu ukiona huwezi kukaa kwenye majengo ya TBA ya Magomeni basi hama uende Vingunguti"

View attachment 3050335
Mwamba yuko sahihi,
 
uhalisia Magomeni Kota wamezidi, nishaenda hapo kutafuta appartment (2023). Nlichokikuta hapo nilishangaa sana.

1. Nje muonekano wa majengo ni mzuri sana, ndani ni kubaya kupitiliza. Jiko na Sehemu za kufulia zipo nje ya appartment na zipo kwa pamoja. Hapo unakuta mtu kaloweka nguo week zipo nje, harufu hatari.

2. Ndani kumejaa harufu ya jasho, nadhani ni shida ya maji. Nje kuzuri ukiingia ndani harufu kali.

3. Jiko lipo nje, ukipika kila jirani atajua unapika nini, hakuna usalama as jiko lina dirisha la nuavu ambapo majiko ma4 ya majirani wa wing moja yote yapo sehemu moja. Ndio mwanzo wa ushirikiana na kutupiana madawa/sumu.

4. Serikali ilichemka sana, ingewalipa tu hao watu wa magomeni kota mapema, na anayetaka ingia ndani ya appartment angeingia kwa masharti inayotaka serikali.

5. Appartment nyingi hazina Master Bedroom. TBA mlitaka unafuu wa kijinga.
 
BTW;
Kawe pale kwa Mwamposa, napo watu walishagawana. Akaja Magufuli na kulirudisha eneo kwa NHC.
Sasa hivi NHC wanajenga nyumba pale na naambiwa watu wanazinunua hata kabla hazijaisha.
Hizi za karibu na Kawe Beach nazo amepewa kampuni ya Mhindi azimalizie ila ndiyo zinakwenda hadi 600M. na watu wananunua sana tu.
Ukiwa Kiongozi, ni heri ufanye kitu na ukaharibu kuliko kuogopa kufanya ili usilaumiwe.
 
Waje huku Vingweta, taka unachimba shimo unafukia, maji tuna visima vyetu vifupi pindua pindua nje nje.
 
BTW;
Kawe pale kwa Mwamposa, napo watu walishagawana. Akaja Magufuli na kulirudisha eneo kwa NHC.
Sasa hivi NHC wanajenga nyumba pale na naambiwa watu wanazinunua hata kabla hazijaisha.
Hizi za karibu na Kawe Beach nazo amepewa kampuni ya Mhindi azimalizie ila ndiyo zinakwenda hadi 600M. na watu wananunua sana tu.
Ukiwa Kiongozi, ni heri ufanye kitu na ukaharibu kuliko kuogopa kufanya ili usilaumiwe.
That last line is SUPER POWERFUL!
 
Back
Top Bottom