Suzy Elias
JF-Expert Member
- Nov 9, 2021
- 1,067
- 6,200
Hayo ameyasema wakati wa kikao cha ndani cha siasa kilichohudhuriwa na makamu mwenyekiti wa CCM bara bwana Kinana.
===
“Mkoa huu hauendelei kwa sababu nyingi, ila sababu kubwa ni hata ninyi ndugu zangu wahaya, wanyambo mnaoishi hapa kwa kweli kuna muda bado hatujajitambua kwamba tupo kwenye ushindani.”
“Tukipita hapa hata siku za kawaida mpaka saa 3 maduka hayajafunguliwa. Sasa unajiuliza, duka linafunguliwa saa tatu. Inamaana mnalala sana au mnafanyaje? Sasa na ninyi mbadilike, fungueni duka mapema ili tuingie kwenye ushindani.”
“Jambo lingine linalokwamisha mkoa huu pia Mhe. Makamu mwenyekiti, Kila mmoja hapa kwenye mkoa huu huwa ni mwanasheria, mnapenda sana kubishana. Eeeeh…Mambo mengi wanapenda kiingereza kingi kingiii, sasa naomba niwaambie, sitaki kiingereza waa sitaki makaratasi”
“Nataka namna gani utakavyo tumia elimu yako kuibadilisha kuwa maendeleo kwa wanakagera. Basi.”