RC Chalamila: Mbowe aliona shetani, majeneza na vifo lakini Rais Magufuli alimuona Mungu na kuishinda Corona

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Albert Chalamila amesema katika kuikabili Corona mh Mbowe wa Chadema aliona shetani, majeneza na vifo ndio maana aliogopa na kukimbilia chumbani kujificha yeye na kundi lake.

Lakini Rais Magufuli alimwona Mungu akazipeleka haja zetu mbele zake, Mungu akatupigania nasi tumeuona mkono wa Mungu ukiitokomeza Corona.

Chanzo: Ayo tv

Maendeleo hayana vyama!
 
Uyu kaondoka jana soma apo
IMG_20200529_145118.jpg
 
Nasikia kuna mtu alijifungia hukoooo na kuhama mji. Hakutoka huko hadi ......

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Albert Chalamila amesema katika kuikabili Corona mh Mbowe wa Chadema aliona shetani, majeneza na vifo ndio maana aliogopa na kukimbilia chumbani kujificha yeye na kundi lake.

Lakini Rais Magufuli alimwona Mungu akazipeleka haja zetu mbele zake, Mungu akatupigania nasi tumeuona mkono wa Mungu ukiitokomeza Corona.

Chanzo: Ayo tv

Maendeleo hayana vyama!
 
Hata kama amekufa mtu mmoja kwa covid 19 ..serikali imekosea
 
Chalamila,Magufuli si mtoto mdogo.Anajua sifa za kweli na kejeli pia.Anachofanya Chalamila ni kejeli na kama hamjui Magu amuulize Kangi Lugola.Pamoja na mauno yote lakini alitimuliwa kwenye kadamnasi.

Jambo la pili viongozi wateule waangalie kauli zao.Magu alikaa 50 days nyumbani kwao,nyumbani kwaosio Ikulu je Mbbowe alikaa siku ngapi?Kauli zenu zinamfanya Raisi aingizwe katika malumbano ya kijinga
 
Tamko la "Mungu kaitokomeza Corona" hapa kwetu ni kupotosha watu wasiendelee kuchukua tahadhali ya kujikinga na janga hili.

Janga hili lipo. Viongozi waendelee kuwahimiza watu wanaowaongoza kujikinga na maambukizi na siyo vinginevyo.
 
Wasikilizeni mataifa mengine. Waliosoma hadithi ya Abnwasi na aibu ya mfalme kutembea akiwa amevaa utupu ataelewa.
 
Huyo naye amezidi kusifia wanaume wenzake hadi kero! Sijui mke wake anamchukuliaje maana si kwa kusifu huko!
 
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Albert Chalamila amesema katika kuikabili Corona mh Mbowe wa Chadema aliona shetani, majeneza na vifo ndio maana aliogopa na kukimbilia chumbani kujificha yeye na kundi lake.
Tatizo lako Chalamila unakurupuka sana. Nenda tena kasome kwenye chuo cha uongozi (By Dr Bashiru Ally Kakurwa)
 
Chalamila yuko sahihi mtu yeyote muovu mwenye mashetani huona tu Yale ambaye Mungu wake shetani anataka kufanya . Chadema Mungu wao shetani ndio maana waliona tu matendo ya shetani tarajiwa

Mtu wa Mungu humwona tu Mungu hata ndani ya Moto.Shadrak meshaki na Abednego walimwona Mungu kwenye Moto japo Moto ulikuwepo hawakuona Moto vivyo hivyo Daniel ndani ya Tundu la Simba hakuona Simba japo walikuwepo alimuona Mungu

Magufuli ni mtu wa Mungu kwenye Corona hakuona corona alimuona Mungu tu japo corona ilikuwepo na tumeshinda Kama taifa

Chadema na miamini mishetani mienzie akina Askofu Bagonza wa KKKT na Askofu Niwermugizi wa Katoliki waliona mashetani tu na vifo visivyohesabika wakafungia Hadi watu wasiabudu kanisani

Hongera mtu wa Mungu Maguifuli .

Pepo Mbowe,pepo chadema, pepo Niwermugizi,pepo Bagonza toka kwa jina la Yesu
 
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Albert Chalamila amesema katika kuikabili Corona mh Mbowe wa Chadema aliona shetani, majeneza na vifo ndio maana aliogopa na kukimbilia chumbani kujificha yeye na kundi lake.

Lakini Rais Magufuli alimwona Mungu akazipeleka haja zetu mbele zake, Mungu akatupigania nasi tumeuona mkono wa Mungu ukiitokomeza Corona.

Chanzo: Ayo tv

Maendeleo hayana vyama!
Maendeleo hayana vyama
 
Covid 19 yupo Tena anaua kwa Kasi sana.

Mwingine kafariki Jana usiku Ni mtumishi wa umma katoka seminani dodoma. Dalili zote za kovid ingawa mpaka Sasa hawajasema Sababu zilizo pelekea kifo chake .

Chukua tahadhari!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom