RC Chalamila: Mkiendelea kuchanganya Dini na Siasa huko mbele patatokea mtawala atakayeamua kufunga makanisa yote na hamtamfanya chochote!

RC Chalamila: Mkiendelea kuchanganya Dini na Siasa huko mbele patatokea mtawala atakayeamua kufunga makanisa yote na hamtamfanya chochote!

Jf kuna watu wana maisha magumu sana na makasiriko yao hapa ndio sehemu ya kurelease. Sasa Chalamila kipi kibaya alichokiongea ambacho kinastahili matusi anayoporomoshewa hapa? Hopeless kabisa.
 
Huyu si ndie alisema hakujaaliwa hekima wala busara?
Tuwapuuze watu waliokosa hekima na busara.
 
Kiongozi wa dini kuhamasisha waumini wa kanisa husika kuchapa kazi,kulipa kodi,kuchangia maendeleo,kuacha kutenda uhalifu nk siyo kufanya siasa?
 
Wakoloni na wafanya biashara za utumwa walichanganya dini na siasa ikawasaidia kututawala kwa urahisi kabisa.
 
Anaota huyo akaulize Idd Amin kilichomkuta hadi akapinduliwa uasi ulianzia kanisani baada ya kunyanyasa kanisa na kuua Askofu Luwun na viongozi wa dini kibao kuwa hataki makanisa anata kuislimisha Uganda kwa pesa na jeuri aliyompa Ghaddafi ya msaada wa pesa na kijeshi aue Ukristo.Uganda kilichomkuta Chalamila anajua

Hapo Zambia tu Raisi aliyepita Edgar Lungu alikuwa mnyanyasaji wa dini ndogo hakuna kama yeye alitaka dini wabaki wakatoliki tu makanisa mengine akiwafanyia kitu mbaya wakajiunga na kuanzisha harakati za kumtoa .Zambia sasa hivi ina Raisi Msabato Raisi Hichlema

Chalamila anaonyesha kalewa madaraka

Hapo alipoongelea kanisa la TAG sio watoto wadogo .Mjinga sana huyo.

Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa aliitoka hapo Mchungaji Dk Kipilimba , Spika wa Bunge Dk Tulia ACkson ni muumini wa TAG

Kiongozi mkuu wa Mahakama Professor Ole Gabriel ni TAG hivi anaelewa maana ya kufuta makanisa?

Kachoka uongozi huyo na sehemu aliyoongelea sio sahihi sana kwake kwa mustakabali wake wa kisiasa

Anamtishia nyau nani mjinga huyo
Kanisa ni Kristo
Nani anauwezo wa kumaliza!!
 
RC Chalamila amewakumbusha Wananchi kutochanganya Dini na Siasa kwani Kanisa na Serikal ni Wabia.

Chalamila Alikuwa akihubiri kwenye mkutano wa Kanisa la TAG na amewakumbusha kuwa Msajili wa Makanisa Yote ni Serikali hivyo ni vema wakalielewa hilo Siku zote.

Chalamila amesema haipendezi kuona Kanisa linajiingiza kwenye Siasa na Kufanya Uchochezi kwani Utulivu wa Kanisa ndio Utulivu wa Serikali.

Kanisa lisiwe kama vyama vya Siasa ambavyo baada ya kuruhusiwa Kufanya Mikutano badala ya kuhubiri Sera Zao wao wanaporomosha Matusi.

Nawatakia Sabato Njema 😀😀
MAKANISA yafanye siasa ZA IBADA tu ZA kumwabufu na kumhmidi MUNGU, NA sio Siasa KWA kisingizio cha IBADA.

BORA MH MKUU WA MKOA amelisemea HILO na Mimi naungana NAYE kwa ASILIMIA 100
KIKUBWA tu ANASHAURIWA asiwatishie WATU IBADA, huko ni kugumu mno kwa sababu anaweza kuwa anagusa kitu KINGINE kabisa AMBACHO VIONGOZI walio wengi huwa hawawezi kukigusa kabisa
 
Kwanini asizungumzie msikiti na makanisa kwa pamoja kama kweli alilenga kujenga hoja yenye kuleta maana.?

Hoja yake imekaa kichawachawa, kumfurahisha aliyepo hapo juu kwa kutaja makanisa. Mtu anakuwa na kichwa kikubwa kama tikiti ila kina kosa akili, inakuwaje hii..?
Point nene.
 
RC Chalamila amewakumbusha Wananchi kutochanganya Dini na Siasa kwani Kanisa na Serikal ni Wabia.

Chalamila Alikuwa akihubiri kwenye mkutano wa Kanisa la TAG na amewakumbusha kuwa Msajili wa Makanisa Yote ni Serikali hivyo ni vema wakalielewa hilo Siku zote.

Chalamila amesema haipendezi kuona Kanisa linajiingiza kwenye Siasa na Kufanya Uchochezi kwani Utulivu wa Kanisa ndio Utulivu wa Serikali.

Kanisa lisiwe kama vyama vya Siasa ambavyo baada ya kuruhusiwa Kufanya Mikutano badala ya kuhubiri Sera Zao wao wanaporomosha Matusi.

Nawatakia Sabato Njema [emoji3][emoji3]
Kama siasa na dini haziendani naombeni mnijibu kwanini viongozi wa siasa wana apishwa kwa vitabu vya dini .....
 
Viongozi wa dini wengi wana maono, wakiona kiongozi anaefaa waache kuwaambia waumini wamchague? Watakuwa wameingilia siasa? Wasifichue ufisadi? Dini na siasa ni maisha ya watu, kiongozi wa dini anapaswa kukumea maovu katika jamii.

Sent from my SM-A042F using JamiiForums mobile app
 
MAKANISA yafanye siasa ZA IBADA tu ZA kumwabufu na kumhmidi MUNGU, NA sio Siasa KWA kisingizio cha IBADA.

BORA MH MKUU WA MKOA amelisemea HILO na Mimi naungana NAYE kwa ASILIMIA 100
KIKUBWA tu ANASHAURIWA asiwatishie WATU IBADA, huko ni kugumu mno kwa sababu anaweza kuwa anagusa kitu KINGINE kabisa AMBACHO VIONGOZI walio wengi huwa hawawezi kukigusa kabisa
Wakati huo maCCM wakielendelea kunenepeana kama nape , uovu ukifanyika unauthiri kila mtu mwenye dini na siyekuwa na dini kwa hiyo kila mtu aukemie kwa nafasi yaeke au kiongozi wa dini au mmachnga
 
Back
Top Bottom